Elie Mpanzu asaini mkataba mpya wa miaka miwili Simba

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,308
Reaction score
18,481
Klabu ya Simba imemuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wake Elie Mpanzu ambao utafikia tamati msimu wa 2026/2027.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba leo, Jumatatu Machi 23, 2026 Mpanzu amesaini mkataba huo mbele ya Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji na Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo, Zubeda Sakuru.

Mpanzu anakuwa mchezaji watatu kuongeza mkataba mpya kuelekea msimu mpya wa mashindano 2026/2027 katika kikosi cha Simba.

Benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker limeidhinisha kuongezwa kwa mkataba wa nyota huyo raia wa DR Congo na nyota wengine ambao tayari wameongezwa mikataba kuelekea msimu mpya wa mashindano ni mlinzi wa kati, Rushine De Reuck na kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma.

1774256194055.png

1774256215111.png
 
Ally Kamwe is typing........
 
Anajua kucheza na akili za watu, baada ya mkataba anarudi kwenye umachachari wake
 
Mpanzu kwa sasa amebakiwa na jina tu. Inashangaza kuona Mzee Clotus Chama anaanza, halafu yeye anasugua benchi!
 
Yale mapenzi yake na yanga yameishia wapi kama alivyokuwa akisema mchambuzi wenu Hans Raphael
 
Pale mtu wa kusajili dirisha kubwa ni striker tu. Timu ibaki hivyo hivyo
 
Huyu si walisema ana mapenzi na Yanga na kwamba msimu ujao atakipiga jangwani?
 
Mo mjanja sana wakati Simba inasuasua alikuwa kimya ila baada ya upepo kubadilika tayari kajitokeza kwa kifupi yeye ndio chanzo cha mfarakano Simba na sasa hivi wataanzakumwimba yeye.
 
Back
Top Bottom