Niyonzima atua Simba

Niyonzima atua Simba

Status
Not open for further replies.
Simba Koko kwa kujifariji. Na ipo siku utakuja uzi hapa kuwa Simba Koko wamemsajili Manji
 
Unajua Niyonzima anaweza kweli kuja Simba kwa sababu moja kubwa ... Yanga watapanda ndege moja tu kucheza na timu ya Misri wakirudi ndo basi tena...

simba watapanda ndege mbili kulifata libolo na chipumbu ya msumbiji
 
Ungekuwa unanifahamu physically nadhani ndio ungeamini...nakueleza kuwa Niyonzima unayemtaja hapa sio Haruna aliyetokea APR
Umesema kweli, anayetajwa hapa sio Haruna aliyetoka APR, ni Haruna aliyetoka Yanga
 
Yanga bab kubwa mchukueni muone maangamizi..muanze upya ujenzi wakikosi,kwanza sidhani kama atathubutu kucheza tim ambayo msimuujao mashindano yake makubwa ya kimataifa ni kagame hatahuko kwenyewe future is not clear kwasimba

laikini aliweza kuthubutu kucheza Yanga msimu huu ambao masindano makubuwa yalikuwa kombe la Mpainduzi itakuwa Simba mwakani mkuu...
 
Simba waache kumendea wachezaji wa YANGA na kama wanataka kuimalisha kikosi chao wafanye usajili kutoka
LIBOLOOOOOO FC.
 
Simba waache kumendea wachezaji wa YANGA na kama wanataka kuimalisha kikosi chao wafanye usajili kutoka
LIBOLOOOOOO FC.

AAH SIMBA MNAUTANI NYIE, LIBOLOOOOO FC LILIKUWA NI KWA AJILI YA MALKIA WAO WA NYUKI, Ah ah
 
Umesema kweli, anayetajwa hapa sio Haruna aliyetoka APR, ni Haruna aliyetoka Yanga

Naona nawe unajifurahisha kama mwenzako...anyway tusiongee sana Mungu atujaalie uzima...na tutakumbushana hizi posts zetu.
 
mkuu tuombe iwe kweli pia tumchukue na kiiza na Okwi akirudi itakuwa bomba zaidi....

da mi mdau wa simba damu damu lakini kwa okwi kurudi simba da naona ni jambo lisilowezekana aisee..
 
MEWEKWA MEI 24, 2013 SAA 5:00 ASUBUHI
HATIMAYE kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuichezea Yanga SC na klabu hiyo asubuhi ya leo imetangaza rasmi kuongeza mkataba na mchezaji huyo wa zamani wa APR na Rayon za kwao.
Kulikuwa kuna mvutano mkubwa kati ya Yanga SC na Haruna juu ya mkataba mpya na kiungo huyo ilikuwa aondoke kesho kurejea kwao, bila kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo, kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Simba SC imemtengea dau la Sh. Milioni 70 na Azam FC pia inamtaka kwa dau nono zaidi, Yanga imekubali kila alichoomba Haruna katika mkataba mpya na wamemalizana.

source: BIN ZUBEIRY
 
Uongozi wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom klabu ya Young Africans leo umekata mzizi wa fitina kwa kiungo mchezeshaji kutoka nchini Rwanda Haruna Niyonzima kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili kufuatia kumalizika kwa mkataba wake awali.
Akiongea na waandishi wa habari makao ya klabu ya Yanga, katibu mkuu Lawrence Mwalusako amesema wameamua kumuongezea mkataba mchezaji huyo kufuatia kuuhitaji mchango wake kwani katika kipindi chake cha miaka miwili ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kutoa mchango mkubwa.
Mwalusako amesema kumekua yakiongelewa mengi juu ya mchezaji wetu Niyonzima, baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikitoa taarifa za kupotosha juu yake ukweli leo umedhihirika kwamba Niyonzima ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuitumikia kwa miaka miwili.
Haruna Niyonzima alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza Julai 2011 akitokea katika timu ya APR nchini Rwanda ambapo katika miaka yake miwili aliyoichezea timu ya Yanga amefanikiwa kuisadia kupata makombe mawili ya ubingwa wa Ligi Kuu 2012-2013 na Kombe la Kagame 2011-2012.
Naye Niyonzima amesema anawashukuru wanachama, washabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga kwa kuwa naye muda wote, Yanga ni nyumbani kwangu kwani najisikia furaha kuichezea timu hii na malengo yangu ni kuisadia ili iweze kufanya vizuri katika upatashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Abdallah BinKleb amesema palikua na propaganda nyingi juu ya Niyonzima, lakini ukweli ndio huu Niyonzima ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili.
"Tunautambua mchango wake alioutoa kwa miaka mwili kwani ameweza kutupatia vikombe viwili vya Ligi Kuu ya Vodacom na Kombe la Kagame hivyo tumemuongezea mkataba wa miaka miwili tena ili aendelee kutoa mchango wake na kuisadia timu katika michezo ya kimataifa" alisema BinKleb

source: NIYONZIMA AONGEZA MIWILI YANGA nyzima.jpg nyzima.jpg nyzima.jpg nyzima.jpg
 
Haya Sasa semeni nyie Simba Koko. Mnachonga sana wakati meno kwishnehi:yell:
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom