Niwezeshe kutimiza ndoto yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niwezeshe kutimiza ndoto yangu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mgombezi, Jun 3, 2012.

 1. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndugu Wana-Jamii

  Ni matumaini yangu mnaendelea vyema na shughuli za kila siku, pamoja na changamoto mbalimbali zinazotukabili. Kwa wale tunaofahamiana kwa kukutana ua namna yeyote ile; MALILA, LAT, KANYAGIO, THE FINEST, na wengine ambao nisingeweza kuwataja wote, habari za siku nyingi…..!!!; kwa muda mrefu sikupatikana sana katika jukwaa hili kama MGOMBEZI, hii ilitokana na harakati zangu za kuhamia hapa mjini Dodoma.

  Mitandao ya kijamii imetumika katika kutuunganisha, hivyo basi kila wakati ni vyema kuangalia au kutafuta jinsi ambavyo mitandao hii inaweza kutumika katika kuleta maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa jumla; kama inavyotumika JAMII FORUM. Kupitia mtandao wa FACEBOOK ambao vijana wetu wengi wamejikita huko niliamua kuanzisha kundi (Group) linaloitwa WAJASIRIAMALI KWELI, kwa lengo la kushirikishana elimu ya ujasiriamali na kupeana mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika kuanzisha shughuli za uzalishaji mali. Kwa wale wanaotembelea Facebook watakuwa wanaelewa kwamba kwenye FACEBOOK kuna option ya kuunda kundi na kujitengenezea Page. Nimeona ni vyema kuleta mawazo haya pia kwa "Great Thinkers", ambapo naamini nitapata michango ya kutosha.

  WAJASIRIAMAILI KWELI: Log In | Facebook

  Dhana ya UJASIRIAMALI katika jamii yetu inaelekea kupoteza mwelekeo au uhalisia. Naamini utaungana nami kwamba mtazamo wa wengi juu ya MJASIRIAMALI, ni pamoja na kununua bidhaa za kichina na kupita nazo mtaani kuuza au hata kama amepanga mahali kuuza. Kwa hiyo basi dhana ya UJASIRIAMALI ni kununua na kuuza (trading), jambo ambalo ninaona kama tunapoteza mwelekeo.
  DSC04117.JPG

  Hiki ni kikundi cha wajasiriamali wakionyesha bidhaa zao; lakini bidhaa nyingi zilizopo ni kutoka china.

  MAANA YA UJASIRIAMALI:

  Neno ujasiriamali linatokana na maneno mawili ambayo ni UJASIRI na MALI. Hivyo maana ya ujasiriamali ni kuwa na: -

  • Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata mali;
  • Uwezo wa kutambua fursa za biashara haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza; na
  • Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara.

  Kwa hiyo mjasiriamali:


  • ni mtu ambaye ana sifa na uwezo wa kutambua mapema fursa za kutengeneza faida na mwenye kuunganisha nguzo kuu za uzalishaji mali (nguvu kazi, mtaji na rasilimali);
  • ni mwanzilishi wa wazo na mwenye maono ya mbali ya jinsi ya kufanya biashara, uwezo wa kupanga, kuratibu na kutekeleza wazo lake na kufikia mafanikio;
  • pia ni mwenye kujiamini, kujituma kwa muda mrefu, kukubali makosa na kujisahihisha, mbunifu na mwenye kuwa tayari kutumia vizuri uwezo na maarifa ya watu wengine

  Tunaweza kusema hizi ndizo NGUZO kuu tatu (3) za MJASIRIAMALI:


  1. Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata mali;
  2. Uwezo wa kutambua fursa za biashara haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza; na
  3. Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara.

  Hivyo basi mtazamo wa WAJASIRIAMALI KWELI ni kujenga uwezo wa kutekeleza nguzo hizi miongoni mwetu, hasa kwa vijana ambao tunawategemea katika shughuli za uzalishaji mali; kama tusemavyo "VIJANA NDIO TAIFA LA KESHO". Tutajengana kwa kupeana elimu ya ujasirimali na mbinu mbalimbali katika kushinda vikwazo mbalimbali.

  Msemo tunaotumia…, - "TIMIZA NDOTO ZAKO KWA KUCHANGIWA MTAJI" Je una maana gani?

  MTAJI NI NINI?

  Mtaji ni uwezo unaoweza kutumika katika kuzalisha mali au kuongeza kipato. Kuna usemi unasema "MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE", kwamba nguzu za mtu zaweza kutumika katika uzalishaji au kuongeza kipato. Katika kuanzisha biashara uwezo huu unaweza kutokana na nguvu alizonazo mtu; kwa maana ya uwezo binafsi juu ya kile anachotaka kufanya, pamoja na rasilimali atakazohitaji.

  DHANA YA KUCHANGIWA MTAJI:

  Watu wengi wamekuwa na mawazo mazuri katika kuanzisha biashara lakini kikwazo kikubwa ni MTAJI. Katika kutekeleza nguzo namba tatu (3) ya Mjasiriamali; "Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara". Nimeamua kutumia dhana ya kuchangiana katika kutekeleza wazo la mtu binafsi katika kuanzisha biashara.

  Jamii yetu imekuwa na utamaduni wa kuchangiana katika kutimiza lengo la mtu binafsi; hii imekuwa ikitumika katika kufanikisha sherehe mbalimbali za ndugu au jamaa au rafiki zikiwemo za kuzaliwa, ubatizo, kipaimara, maulidi, harusi n.k. Kwamba mtu anakusanya watu wachache ni kuwaeleza haja ya kufanikisha jambo lake na kuwataka ndugu au jamaa au marafiki kumchangia kwa hali na mali katika kufanikisha jambo hilo.

  Hivyo basi kutokana na utamaduni huu ambao tumekuwa tukitumia katika kufanikisha sherehe na shughuli nyingine za kijamii, tunaweza kutumia sasa utamaduni huu katika kutekeleza malengo ya mtu binafsi ambaye anataka kuanzisha shughulli za uzalisha mali au biashara kwa kumchangia mtaji.

  Mitandao ya kijamii imetumika katika kutuunganisha, hivyo basi muungano huu tunaweza kuutumia vyema katika kuangalia mahitaji ya wengine katika kutimiza ndoto zao.

  Mchango tunaoweza kumpatia mtu ni pamoja na mawazo yetu katika kuboresha wazo husika na rasilimali zinazohitajika.

  MRADI WA MAJARIBIO (PILOT PROJECT):

  Nikiwa kama mwezeshaji wa kujitegemea, nimeamua kutekeleza wazo langu kwa vitendo kwa kuliwakilisha kwenye jamii kwa lengo la kuomba michango yao, kupitia "NIWEZESHE CAMPAIGN".

  KILIMO CHA MAPAPAI – STAN'S PAPAYA

  Kumekuwa na uhitaji mkubwa wa mapapai katika mji wa Dodoma na hata sehemu nyinginezo za nchi kutokana na utafiti mdogo niliyofanya, Bei ya papai katika maeneo mengi ya nchi inakadiriwa kuwa Tsh. 1000 – 3000, hapa Dodoma ni kati ya Tsh 2000 – 3000. Nikiwa kama mjasiriamali nimeona vyema kutumia uhitaji huu kama fursa ya biashara kwa kuanza kilimo cha mapapai ili kwa sehemu niweze kuchangia uzalishaji wa bidhaa hii, ambapo itasaidia pia kupunguza bei katika soko. Dhamira yangu ni papai kumfikia mlaji kwa bei kati ya Tsh. 500 – 1000. Vile vile nimehamasika kuanzisha kampeni ya matumizi ya mapapai, ikiwa ni pamoja kulitumia kama tunda na bidhaa nyinginezo zitokanazo na papai. Unaweza kutembelea page yangu kupitia mtandao wa FACEBOOK ambapo utapata dondoo za matumizi ya papai na mengineyo. Stan's PaPaYa | Facebook

  workplan4.png

  Ili niweze kuanzisha mradi huu nahitaji kiasi cha fedha Tsh. 5,920,000, ambapo mchango wangu binafsi zitakuwa gharama za uendeshaji zitakazo gharimu kiasi cha Tsh. 950,000/=. Hivyo basi mchango wa fedha ninao hitaji kutoka kwa jamii ni kwa ajili ya gharama za uanzishaji (start-up fund), ambazo ni Tsh. 4,970,000/=. Natafuta watu 1000 kutoka katika jamii watakaoweza kunichangia Ts.4970/= kila mmoja.

  Nawatafuta watu hawa kupitia mitandao ya kijamii (JAMII FORUM na FACEBOOK) pamoja na jamaa inayonizunguka.
  Unaweza kuwakilisha Mchango wako kupitia:

  TIGO PESA - 0714 460528 or M - PESA - 0757 941044

  (Mwisho ya kupokea michango tarehe 30/06/2012)

  Taarifa za kupokelewa kwa michango na utekelezaji wa mradi hatua kwa hatua zitawakilishwa kupitia:

  JAMII FORUM - Business & Economic Forum, Katika post hii
  FACEBOOK - Stan,s PaPaYa Stan's PaPaYa | Facebook
  WAJASIRIAMALI KWELI Log In | Facebook

  NB: Ikiwa upo ndani ya Mji wa Dodoma, unaweza kutoa order ya Mapapai na kufanya malipo ya awali. Kiwango cha chini ni mapapai kumi (10) na kila papai utalipia Tsh.500/=

  Naomba kuwasilisha..............!!!, Natanguliza Shukrani.......!!!

  MAHITAJI YA MRADI:


  A: UWEKEZAJI

  I: RASILIMALI

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MAHITAJI[/TD]
  [TD]MAELEZO[/TD]
  [TD]KIASI[/TD]
  [TD]BEI[/TD]
  [TD]JUMLA[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Ununuzi wa Shamba[/TD]
  [TD]Heka[/TD]
  [TD]1[/TD]
  [TD]1,000,0000/=[/TD]
  [TD]1,000,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Ujenzi wa Nyumba ya Wafanyakazi[/TD]
  [TD]Nyumba[/TD]
  [TD]1[/TD]
  [TD]700,000/=[/TD]
  [TD]700,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 5"]VIFAA VYA UMWAGILIAJI – Umwagiliaji kwa njia ya matone (Drip irrigation systems)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Bomba – ¾ inch (pvc)[/TD]
  [TD]Mita[/TD]
  [TD]1500[/TD]
  [TD]1000/=[/TD]
  [TD]1,500,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Tank la Maji[/TD]
  [TD]1000 Lita[/TD]
  [TD]1[/TD]
  [TD]160,000/=[/TD]
  [TD]160,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Pump ya kusukuma maji[/TD]
  [TD][/TD]
  [TD]1[/TD]
  [TD]300,000/=[/TD]
  [TD]300,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Bomba la kuvuta maji[/TD]
  [TD]Mita[/TD]
  [TD]5[/TD]
  [TD]10,000/=[/TD]
  [TD]50,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Bomba la kupeleka kwenye Tank[/TD]
  [TD]Mita[/TD]
  [TD]20[/TD]
  [TD]3,000/=[/TD]
  [TD]60,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Ujenzi wa Mnara wa Tank[/TD]
  [TD][/TD]
  [TD]1[/TD]
  [TD]300,000/=[/TD]
  [TD]300,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 4"]JUMLA[/TD]
  [TD]4,070,000/=[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  NB: KILIMO CHA UMWAGILIAJI:
  Kilimo cha umwagiliagi kwa njia ya matone (Drip Irrigation System), ambapo mabomba (mipira) itapita kataka kila shina la mche na kudondosha matone ya maji yanapohitajika.  II: UPANDAJI

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MAHITAJI[/TD]
  [TD]MAELEZO[/TD]
  [TD]KIASI[/TD]
  [TD]BEI[/TD]
  [TD]JUMLA[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Maandalizi ya Shamba[/TD]
  [TD]Heka[/TD]
  [TD]1[/TD]
  [TD]100,000/=[/TD]
  [TD]100,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Mbole – Samadi ya Ng'ombe[/TD]
  [TD]Tani[/TD]
  [TD]10[/TD]
  [TD]10,000/=[/TD]
  [TD]100,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Manunuzi ya Mbegu[/TD]
  [TD][/TD]
  [TD]1000[/TD]
  [TD]500/=[/TD]
  [TD]500,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Upandaji wa Mbegu[/TD]
  [TD][/TD]
  [TD]1000[/TD]
  [TD]200/=[/TD]
  [TD]200,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 4"]JUMLA[/TD]
  [TD]900,000/=[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  III: UENDESHAJI

  NB: Kutokana na mbegu itakayotumika Mche wa papai utachukua Miezi sita (6) mpaka kuanza uzalishaji.

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MAHITAJI[/TD]
  [TD]MAELEZO[/TD]
  [TD]KIASI[/TD]
  [TD]BEI[/TD]
  [TD]JUMLA[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Mfanyakazi (miezi 7)[/TD]
  [TD]Miezi[/TD]
  [TD]7[/TD]
  [TD]100,000/=[/TD]
  [TD]700,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Gharama Nyinginezo[/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD]250,000/=[/TD]
  [TD]250,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 4"]JUMLA[/TD]
  [TD]950,000/=[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  JUMLA YA MTAJI = Tsh. 5,920,000/=

  B: JINSI YA KUPATA MTAJI:

  Mtaji nategemea kupata kwa kuchangiwa na wana-jamii kama ifuatavyo:

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MCHANGO BINAFSI – Gharama za Uendeshaji[/TD]
  [TD]950,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]MCHANGO WA WANA-JAMII – Rasilimali + Upandaji[/TD]
  [TD]4,970,000/=[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]JUMLA[/TD]
  [TD]5,920,000/=[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Hivyo Basi Wana-Jamii = 1000
  Kila mmoja anaweza kunichangia = Tsh. 4,970/=

  ***********************************UPDATES***********************************

  A: HATUA ZA UTEKELEZAJI:

  31/May/2012 - Upatikanaji wa eneo/shamba huko Michese, bado halijalipiwa.  B: MICHANGO KUTOKA KWA JAMII:

  [TABLE="width: 587"]
  [TR]
  [TD]S/NO[/TD]
  [TD]ID[/TD]
  [TD]AMOUNT[/TD]
  [TD]DATE[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1[/TD]
  [TD]Bakari Kawiza[/TD]
  [TD]5,000[/TD]
  [TD]29-May-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2[/TD]
  [TD]Fadhili Chitanda[/TD]
  [TD]5,000[/TD]
  [TD]29-May-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3[/TD]
  [TD]Amkawewe[/TD]
  [TD]5,000[/TD]
  [TD]4-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]4[/TD]
  [TD]Kaunga[/TD]
  [TD]10,000[/TD]
  [TD]4-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]5[/TD]
  [TD]Rose Lusinde[/TD]
  [TD]10,000[/TD]
  [TD]5-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]6[/TD]
  [TD]Malila[/TD]
  [TD]10,000[/TD]
  [TD]7-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]7[/TD]
  [TD]Miundombinu[/TD]
  [TD]20,000[/TD]
  [TD]9-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]8[/TD]
  [TD]Mary Msemwa[/TD]
  [TD]6,000[/TD]
  [TD]10-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]9[/TD]
  [TD]Leonard Kisenha[/TD]
  [TD]5,000[/TD]
  [TD]11-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]10[/TD]
  [TD]Kibanga Ampiga Mkoloni[/TD]
  [TD]20,000[/TD]
  [TD]11-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]11[/TD]
  [TD]Kitokota[/TD]
  [TD]10,000[/TD]
  [TD]13-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]12[/TD]
  [TD]Asrams[/TD]
  [TD]5,000[/TD]
  [TD]17-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]13[/TD]
  [TD]Jalala[/TD]
  [TD]10,000[/TD]
  [TD]20-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]14[/TD]
  [TD]Muhinda[/TD]
  [TD]10,000[/TD]
  [TD]20-Jun-12[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD]Total contributions as today:[/TD]
  [TD][TABLE="width: 92"]
  [TR]
  [TD="class: xl67, width: 92, align: left"]131,000[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD]Total Amount Requested:[/TD]
  [TD]4,970,000[/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD]Balance:
  [/TD]
  [TD]-4,839,000[/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  dah!.....mkubwa!kwa sasa nikupe pongezi za kuwa na mawazo mazuri sana,ntarudi tena ila chukua saluti!
   
 3. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nakushukuru Mkuu, Ruhazwe Jr; nategemea mchango wako.
   
 4. K

  KISWAHILI Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umejipanga!!
   
 5. asrams

  asrams JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 4,017
  Likes Received: 1,387
  Trophy Points: 280
  Hongera sana kaka, inshaAllah utafanikisha lengo lako. Je kuna nafasi ya kununua hisa??


  Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
   
 6. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kaka, wakati utakapofika basi nitaweza kutangaza kuuza hisa; kwa sasa niwezeshe.....!!!.
   
 7. asrams

  asrams JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 4,017
  Likes Received: 1,387
  Trophy Points: 280
  Bila shaka kaka. Nipo nje ya nchi lakini ntakuwezesha kabla ya tar.15 inshaAllah


  Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
   
 8. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kaka....., karibu nyumbani...!!!
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  JF is food for thought. Nimejifunza mengi sana kwenye uzi wako, sijui nikupe zawadi gani ya kukufaa.
  Wastaafu na wale wote wanaokaribia kustaafu, pia wale wasio na ajira wewe ni mwalimu wao mzuri.
   
 10. REX

  REX JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kaka hongera sana,naamin kwa mwenye uwezo wa kuelewa amekuelewa.big up bro!
   
 11. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu Bujibuji, Nashukuru; bali mchango wako wa NIWEZESHE itakuwa zawadi kubwa na utakuwa umechengia wengi kujifunza.
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  dah ... very exciting project ..... think of processing pawpaw/papaya beverage (smooth juice or hard liqueur)

  utatoka mkuu

  anyways ..... count me in on your charity fundraising list ..... !
   
 13. l

  len Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hongera sana Mgombezi kwa mawazo yako mazuri sana, wewe kweli ni mjasiriamali. Tarajia mchango wangu wakati wowote na ninaamini utakuwa ukitupatia feedback ya maendeleo ya mradi.
   
 14. m

  muhinda JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 337
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Nafurahi sana kuchangia mambo ya aina hii, sio harusi.
  count me in.
  Ila mkuu tuna uhakika gani kama kweli upo serious au unakusanya pesa ya kula ulabu tu?
   
 15. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nakushukuru Mkuu LAT, kwa mchango wako wa mawazo katika kuboresha wazo hili; nitafanyia kazi ushauri wako. Nategemea kupokea kutoka kwako, Niwezeshe.....!!!
   
 16. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nashukuru Mkuu LEN; nitakuwa nawakilisha taarifa za kupokea michango na hatua za utekelezaji hapa jamvini.
   
 17. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nashukuru Mkuu MUHINDA, hii ni moja kati ya changamoto tuliyonayo katika jamii yetu; kwani kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakitafuta michango ya fedha kwa matumizi yasiyo sahihi. Nakuahidi mchango wako kutekeleza lengo husika na utapokea taarifa.
   
 18. M

  Malila JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kunikumbuka, huku Dar mimi nakimbizana na jamii farm ya siku zile pale Lunch Time. Tumefikia pazuri kwa sasa, na june hii tunatia wanyama wa kwanza. tuombee na sisi tunakuombea, nitafutie mbegu ya papai fupi.
   
 19. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nashukuru Mkuu Malila; Kwa kweli ninawakumbuka sana kwa changamoto tunazoendelea kupeana, napata update za KILIMOTZ; Pongezi za pekee kwako kwa kazi njema unayoendelea nayo,nawatakia kila la kheri kwa hatua mliyofikia, nitaungana nanyi baada ya kupata utulivu kidogo hapa makao mapya. Baada ya kuotesha mbegu ninazotarajia, nitakupa matokeo yake na baada ya hapo nitaweza nitakushauri njia sahihi. Nategemea mchango wako, Niwezeshe......!!!
   
 20. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,125
  Trophy Points: 280
  Mkuu muleta maada kwanza kabis nikupongeze sana make hizi ndo moja ya investment ambazo zinaweza watoa WATANZANIA, kama kuna uwekezaji wenye tija moja wapo ni huu wa kwako, na kinacho takiwa ni kuwa na VISION nzuri, Na ni bora na wengine tukawa tunajifunza kutoka kwa jamaa hapa, mleta maada hata akipresent hii proposal yake mahali fulani watu wanaweza kumuelewa,

  - Ni bora watanzania tuachane kabisa na Biashara za uchuuzi ambazo hazina tija kabisa na tujikite kwenye project za aina hii na zinginezo ambazo zinatija kwa Taifa,

  - Na vitu kama hivi ndo vinatakiwa kupewa kipa umbele badala ya jamii kuwekeza kwenye Anasa, kama Harusi zisizo kuwa na Tija kwa Taifa, na kiwango anacho omba mlete thread ni kidogo sana ambacho hata Ndugu, jamaa na marafiki wangeweza kuchangia lakini Ndugu, Jamaa na marafiki hawawezi changia kwa sababu hakuna ulaji kwao, hapo mleta thread angetangaza kuoa zingeisha patikana

  -ok mkuu nitafanya process nitakutumia, ingawa kwa sasa niko mbali kidogo, ila nitakutumia mchango
  ,
   
Loading...