Nimeipenda. Nzuri sana hangaika dunia hii inahitaji juhudi binafsi. Nitachangia kesho mchana.
John Kennedy wa USA aliwahi sema "Don't ask what the USA has done for you,but rather ask yourself what have you done for USA"
Kaka yangu nishakukaribisha(Facebook) uje kuchukua hope itatosha!
Tupo pamoja mkuu, ila tu labda ungesogeza deadline ili kwa wale wenye nia ya kukuchangia na kwa sasa wanasubiri mwisho wa mwezi waweze kukuunga mkono wakati unapofika wa mishiko. kisha Baada ya hapo ni ushauri wangu kuwa uwezekano ni mkubwa kuwa pesa zitakuwa hazijakamilika, lakini kile ambacho utakuwa umejaaliwa kukikusanya mpaka wakati huo wewe anza tu mchakato wa mambo madogo madogo. na kadri unavyowahakikishia wana Jf hatua ulizofikia na kuwathibitishia lazima watajitokeza wafadhili zaidi na hata hao waliokwisha toa huenda wakaingiwa moyo wa kutoa zaidi.
Kila La kheri.
Mkulima mwenzio,
Kitope
Kaka nishatuma mchango wangu, na muwakilishi wangu kanambia umempigia, je ni kweli ? Mwisho wa mwezi ntatoa nyingine inshaAllah tukiwa hai na panapo uzima
Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
Nashukuru Mkuu ASRASMA, nimepokea mchango wako; natanguliza shukrani kwa ahadi yako.