Hapo kwe Msamaha kiukweli Mungu aingilie Kati... SIJAWAHI kumsamehe kwa matukio hayo mawili niliyotaja kule juu.. na ndio mana Huwa yanarudi kichwani na kunikosesha Amani.Psychological mumeo atakuwa kalelewa na single mama, au single father, kama sio hivyo kalelewa kwa bibi au kwa ndugu ....... kuna kitu kinapungua kwenye uzani hasa wa mapenzi huyo jamaa alikosa mapenzi ya baba na mama utotoni kama aliyapata basi baba yake alikuwa mkatili anachokufanyia ni input aliyopata utotoni kiufupi watu wa aina hii hawajali hisia za wake zao wala wapenzi wao anachokifanya nikulipiza upendo alioukosa na ngono.
Cha kukushauri:
Achilia msamaha na Mwambie ukweli kumuumiza utaumiza uzao wako na wanao watakuwa kama baba yao maana watakosa malezi ya baba na mama mvumilivu kama wewe wanaume wengi wanafanana usiondoke leo wanao wala usiweke nia mbaya kwa mumeo lia na Mungu wako asimamie ndoa yako ya serikali.
#usiondoke umemudu kwa miaka minne talk to God ,Mungu aendelee kukutia nguvu na uvumilivu.
Ndio, 100%Mkuu mkeo angekuweka kwenye situation aliyopo mleta mada kwasasa ungeufuata huu ushauri wako?
Na unapataje ujasiri wa kumpiga na kumfungia nje mkeo mwenye mtoto mdogo huku mtoto wako akiwa ndani??. Hiki kitendo alichofanya mume wa mtoa mada sio upunguani ee??Mtoa mada a focus na kazi, malezi ya watoto wake, Huyo wa Arusha alikuwa mvuta bangi.
Unapataje ujasiri wa kukata mikono au kuua binadamu mwezio kama sio upunguani wa akili?
Kaa utafakari mustikabari wa watoto wako na Familia yakoLakini hatufanyi kwa KUPENDA wanaume wanatusukuma tufanye hivyo..
Mimi nilijiapiza sitatolerate vipigo hata kama ni kofi,sivumilii. Nimekulia sehemu ambayo wanawake wanapigwa na waume zao hadi wanakufa, kwangu mimi mwanaume anaempiga mwanamke namchukulia kama muuaji tu na muuaji havumiliwi anakimbiwa.Dah. Pole sana. Nafikiri ushapata la kufanya hadi sasa. Tusitolarate vipigo jamani. Watoto mwachie atalea kama ulivyoamua. Kumkomoa kwa kuondoka unaweza kua humkomoi vile vile maana kuna wanandoa wengi tu wanatamani wake zao wasepe wenyewe sio wawatimue. Loh.
Asante sanaKila siku nasema humu,msaliti hua hasamehewi hata siku moja,haijalishi huyo msaliti ni wa jinsia gani,
Kitendo cha kusema ulifunga nae ndoa ya kiserikali bila ndugu kuhusika kina ashiria kua hiyo ndoa haikua na baraka za wazazi wako wala ndugu zako,hukutaka kusikia neno la mtu na ukaamua kuolewa tu,sasa yamekufika,mbele moto,nyuma moto,huwezi hata kwenda kushtaki kwenu coz ndoa uliitaka wewe mwenyewe kwa nguvu,
Ushauri,
Mchunguze huyo mwanamke kama kaolewa,kama kaolewa tafuta namba ya mumewe,ukisha ondoka hapo kwako,watumie hizo screen shot,Mume wako,Mwanamke wake na mume wa huyo mwanamke,
KOSA ulilolifanya ni ulivumilia kwa muda mrefu ukiamini kua Mumeo angebadilika,msaliti hua habadiliki,kosa lingine ulimuonyesha kua unamuhitajia sana na huwezi kuishi bila yeye,ndio maana akakushusha thamani yako,
WATOTO wako usiwaache,chukua watoto wako uende nao popote utakapo enda,
Huyo Mwanaume hata akija kukuomba radhi,usimpe nafasi kabisa,yani usirudiane nae tena,utakuja kufa kwa magonjwa ya stress au akuletee magonjwa ya zinaa,
Huu ni ushauri tu but the rest it's up to you,
Good luck.
Yeap mama basi ujue shida ni malezi ameathiriwa alikosa upendo ni kitu muhimu sana angalia tabia za wanaume wengi wenye hayo mambo na angalia historia yao walilelewaje.Hapo kwe Msamaha kiukweli Mungu aingilie Kati... SIJAWAHI kumsamehe kwa matukio hayo mawili niliyotaja kule juu.. na ndio mana Huwa yanarudi kichwani na kunikosesha Amani.
Ni kweli ulichosema hujakosea historia inaonesha alilelewa na ndugu sana KULIKO wazazi.
Ndio maana nilitamani mzani kutokwa kwa mwanaume mwenzangu pia.Pakini kwa hali ya sasa mengi husababishwa na hii 50 kutamaniwa.Wanaume tuache kujinyanyua mabega na kujihesabia haki dhidi ya wanawake!
Kwamba mwanaume kaumbiwa tamaa kuchepuka ni sawa ila kwa mwanamke ni uhaini.
Tustuke that's no longer working na tuadjust kuendana na mabadiliko haya ya kijamii yaliyotokea.
Hapana na Wala sitaki kufanya hivyo .nitapambana mwenyewe staki kutia WATU kwe preshaKaa utafakari mustikabari wa watoto wako na Familia yako
Kama moyo unakushauri kuacha Watoto pekee yao muulize Mungu kama ulichokitafakari ni sahihi ?
Mama/baba yako mzazi ulishawahi kumshirikisha suala lako ?
Mama lete kazi.mezani..fursa hiyoKwa muda mrefu nimekuwa nikimuhisi mwanamke mmoja kuwa na mahusiano na MUME wangu kutokana na charting zao ..na ubize WA simu WA MUME wangu..
Wiki iliyopita nikapata nafasi nzuri ya kukagua simu ya Mr hivyo ..nimethibitisha pasi na shaka kuwa wako katika mahusiano kutokana na majina ya kimapenzi wanayoitana,na MAWASILIANO ya mara kwa mara( karibu kila siku wanawasiliana asubuh,mchana Hadi usiku).
Nilichofanya niliscreenshot MESEJI zoote nikajitumia na sikuacha ushahidi wowote kama nilishika simu yake..MAISHA yanaendelea kama kawaida ...
Wote ni waajiriwa..Tuna miaka 10 ya ndoa(tulikubaliana kufunga ndoa ya serikali sisi wenyewe bila kushirikisha wazazi hivyo hata mashahidi hawakuwa ndugu zetu Wala rafiki zetu japo MAHARI ALITOA na taratibu zingine zilifuatwa. Hivyo tukaanza kuishi pamoja ili tukijipata tufunge ndoa ya kanisani) , ..but Hadi leo hatujafanikiwa kuwa na ndoa ya kanisani.
Tuna watoto 4( mmoja WA mama mwingine mkubwa kwa watoto wangu jhakuwahi kunieleza kabla ..niligundua baada ya kuanza kuishi pamoja... lakini MAISHA yaliendelea)
Sikuwa na tabia ya kumchunguza Mume wangu apo mwanzo Kilichonifanya nianze kumchunguza ni mabadiliko ya muda mrefu yaliyopo ndani( miaka kama 4 sasa )dharau ,MAPUUZA, kutokujali mambo..Kuna KIPINDI aliwahi kunipiga,kunifungia mlango nje Tena nikiwa na mtoto mdogo WA miezi(nilimuacha ndani) sikuwahi kusikia neno la Msamaha kutoka kwake aliona sawa tu...bado nilivumilia MAISHA yakaendelea ...ukikosea jambo anakua mkali kupita maelezo Tena kwa maneno makali ya kukera.Mwanzoni nilikua naumia sana na kulia.. badaye nilivyoona ni ujinga kumlilia mtu ambaye haoni thamani ya chozi lako na Wala hawezi kubadilika,na mimi nikaanza kupunguza upendo taratibu kwake nikahamishia mapenzi kwa watoto wangu,kazi na kuanzisha biashara zangu,...
Tendo la ndoa SIJAWAHI kumnyima japo sometimes mood inakata kabisa nikianza kufikiria matukio na kauli zake.. tunaweza kukaa hata wiki hatujagusana ...
Sasa kilichonifanya nije hapa...
Ni hiki.. kwa muda wote huo nilikua natafuta nafasi na chanzo kikuu Cha mabadiliko hayo...Nimeshakipata kama nilivyoeleza huko juu MAHUSIANO na mwanamke mwingine..na ushahidi ninao..
Sitaki kumuuliza WAla kuongea naye chochote juu ya hilo..
Nataka niondoke nikaanzishe MAISHA yangu nimuache na watoto ( kuhusu kuondoka na watoto hapa usinishauri))
....lakini kabla ya kuondoka, nataka AJUE KAMA NIMEJUA USALITI WAKE na nataka ATESEKE KISAIKOLOJIA alipie MAUMIVU yote niliyoyaishi kwa miaka yote hiyo..
Je NITUMIE MBINU GANI?.. Ikiwezekana nipe MBINU ya kumtesa na huyo mwanamke(iwe MENTALLY). Tena ikiwezekana kuwafanya wote wawili kila mmoja kwa wakati wake anipe hela Ndefu afu nijikatae ZANGU lengo ni kuwakomoa tu...wasinisahau..
SIMTAKI TENA!!
Libayaaaa!Dahh inasikitisha
View attachment 3680369
😁 Dah mkuu punguza hasiraWanawake kama ulipenda mtu tambua Kuna vitu vilikuvutia
Tena ukaona na kasoro zake na bado ukajipa moyo utazimudu kulingana muda
Sasa tuseme basi wewe hukuolewa na muasherati ila uasherati umeanza Baada ya kuwa na wewe.. Huoni ni tatizo.?
Wanawake wapumbavu siku zote uharibu nyumba zao kwa mikono yao wenye huku wanatafuta mchawi nani
Kuna mpuuzi mmoja naye kila kukicha mume wangu ni mlevi
Watu tukamuuliza kabla hamjaoana alikuwa mla kilaji jibu HAPANA
Sasa iweje kabadilika anajibu mimi sijui.!? 🤭
Wanawake mnawapa sana stress waume zenu kwa upungufu wenu wa akili na mazoea ya kiswahili huku mnajisahau na kujikuta mnajua
Na bado mtaachika sana mpaka tabia ya ufenism ipotee
Na ukianza tolarate hata kofi kesho anakupiga ngumi ya jicho keshokutwa unakatwa shingo. Vipigo hapana kwakweli. Tena nimependa ujasiri wa dada wa kumuachia watoto nae apambane nao tu, hizi huruma za kusema watoto wataishije sijui watateseka nikiondoka zisisababishe tuwe abused.Mimi nilijiapiza sitatolerate vipigo hata kama ni kofi,sivumilii. Nimekulia sehemu ambayo wanawake wanapigwa na waume zao hadi wanakufa, kwangu mimi mwanaume anaempiga mwanamke namchukulia kama muuaji tu na muuaji havumiliwi anakimbiwa.
. .. 'Hawakuwa na imani ya namna hii'... Imani ya kufanyaje?Huu sio ushauri, naandika tu nachokiwaza:
1) Kwanini binadamu anafikiri ana hati miliki ya binadamu mwengine? ? ? Like how? ? Who are you? ?
2) Utasema ni kwasababu alisema / alitoa kiapo kuwa utakuwa mali yake.
Watu husema mengi ambayo hawayamaanishi.
Wengine wanasindikiza maneno yao na matarumbeta na sherehe za bei ghali, lakini hawamaanishi walichokisema. Understand this.
Njia pekee ya kujua kuwa mtu kamaanisha alichokisema ni matendo yake, anayaishi maneno yake.
Kama mtu alisema nyeupe lakini anaishi nyeusi, wewe kukaa kung'ang'ana kumkumbusha kuwa alisema nyeupe, ni tatizo lako seriously. Rudia point namba 1.
3) Tungekuwa na imani juu ya MUNGU kama tulivyo na imani juu ya hawa wafanya mauzauza, maisha yangekuwa bora sana.
Unakuta mtu haamini MUNGU akisema ataleta Ufalme wake duniani, lakini kabaki kushikilia maneno ya kikaragosi kimoja kilichompiga fix kwa nderemo na vifijo, kabaki kuishi kwa sonona akishikilia imani kuwa siku moja kikaragosi hicho kitatimiza ahadi zake na maisha yatabadilika na kuwa mapya! ! !
Hata Abrahamu aliyekuwa tayari kumtoa Isaka hakuwa na imani ya namna hii!
Hata Noah aliyejenga safina wakati hakuwahi kuona mvua maisha yake yote hakuwa na imani ya namna hii!
Hata wanafunzi wa Yesu waliokubali kuuawa kumshuhudia Yesu hawakuwa na imani ya namna hii!
Wewe ndio una tatozo la kisaikolojia sio tatizo ni tatozo unawaza sana maokoto, leo katika pitapita nikakuta wanawake wenzio wanaongea wanasema kwambaJe NITUMIE MBINU GANI?.. Ikiwezekana nipe MBINU ya kumtesa na huyo mwanamke(iwe MENTALLY). Tena ikiwezekana kuwafanya wote wawili kila mmoja kwa wakati wake anipe hela Ndefu afu nijikatae ZANGU lengo ni kuwakomoa tu...wasinisahau..
SIMTAKI TENA!!
Samehe saba mara sabini, Fanya kazi kwa bidii, Simamia watoto wako wapate elimu bora, Walee katika maadili mazuri ya Kitanzania.Hapana na Wala sitaki kufanya hivyo .nitapambana mwenyewe staki kutia WATU kwe presha