Nivunje vipi haya mahusiano?

Nivunje vipi haya mahusiano?

Aah hapo mute tu vimiezi viwili bila mawasiliano.
Mwezi uliopita nilijaribu hiyo njia,nikaanza kupata malalamiko toka kwa rafiki zake ambao kaniunganisha nao kuwa namtesa rafiki yao nimemchunia kwa kuwa nimeshapata nilichotaka nikasema fine ngoja nimtafute upya

Lakini cha ajabu tulipoanza mawasiliano tena hadi leo hata kuja hom imekua kama tuko mikoani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Practically, wanawake wanahitaji kuhudumiwa na mwanaume. Hili twende mbele turudi litabaki kuwa ukweli.

Ila,

Kuna kalakini, ukishajua hivyo jitafutie walau ambaye anaweza kukuvumilia kipindi umepungukiwa.

Au , tafuta ambaye walau amejitosheleza wewe kazi yako kujazia tu.

Sasa mkuu hata sex hupati wewe unafaidika na nini sasa? Siku hizi ni mchezo wa shinda ni shinde.
Ni hatar yamebaki mapenzi ya kwenye keyboard tu yenyewe anajitaidi sana kiukweli,heshima za kiwango cha sgr ila hajawahi jiuliza huyu mtu mahitaji yake ya kihisia anayamaliza vipi?

Au ndo ile usipokua na hela hisia unatoa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua haya ni maoni yako ila sio kesi tukiyajadili.

Umpiganie mtu kwasababu anaonyesha dalili za kukupenda tu?

Binafsi nampongeza mtoa mada...kumpigani dada yake ni jambo la kuigwa kuliko kuendelea kumpigania huyu mdada mwingine wanayeunganishwa na kaupendo tu ka sex ya kitandani.
Ni sahihi kabisa kumsaidia ndungu yake na hili naunga mkono kabisa.

Shida Ni kwamba kumwacha umpendae kwa Sababu tu umeyumba kwa kipato.kama anakupenda Haina sababu kuvunja mahusiano lakini Kama yupo kwa kuchuma pesa sawa weka kulee.....

Pesa haiwezi kuwepo Kila siku kwa ajiri yake tu, ikiwepo sawa.kama Ni wife material atavumilia Kama sio atasepa tu Wala haihitaji kuumiza kichwa namna ya kumwacha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwezi uliopita nilijaribu hiyo njia,nikaanza kupata malalamiko toka kwa rafiki zake ambao kaniunganisha nao kuwa namtesa rafiki yao nimemchunia kwa kuwa nimeshapata nilichotaka nikasema fine ngoja nimtafute upya

Lakini cha ajabu tulipoanza mawasiliano tena hadi leo hata kuja hom imekua kama tuko mikoani

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee baba unaiabisha kambi rasmi. Hao wapambe tu.

Hao wapambe tu...wanataka wakutoe kwenye reli uendeelee kutoa pesa. Hebu nin'gate sikio ulikuwa unampa shingapi?
 
"dhumuni kuu la kuandika uzi huu ni kwamba kiasi cha fedha kinachobaki baada ya makato ni kidogo sana kiasi kwamba nashindwa hata kumhudumia mpenzi wangu"

Hili dhumuni lako tafutia suluhisho[emoji121]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa sasa kiukweli sina namna maana kaajira ndo haka nakategemea japo nikiri ni uzembe wa kifikra kutopanua kipato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hatar yamebaki mapenzi ya kwenye keyboard tu yenyewe anajitaidi sana kiukweli,heshima za kiwango cha sgr ila hajawahi jiuliza huyu mtu mahitaji yake ya kihisia anayamaliza vipi?

Au ndo ile usipokua na hela hisia unatoa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani atakukubali usipokuwa na cha kumpa? Hata marafiki wa kiume siku hizi usipokuwa na cha kuchangia kwenye vijiwe vyetu vya kahawa tunakutenga.
 
Habari wakuu

Mwaka huu niliazimia kuwa na mahusiano rasmi ambayo kama Mola akibariki tufike kwenye kujenga familia maana mwakani nnafikisha miaka30

Kweli mwaka jana mwezi november nilifanikiwa kuanza mahusiano na binti mmoja wa mtaa wa pili ambae kiukweli nafsi yangu ilimkubali sana tangu siku ya kwanza namuona hadi leo hii tulipo.

Lakini changamoto ni kuwa siku chache baada ya kuanza mahusiano yetu dadangu wa damu alipata shida kubwa ya kifedha ambayo kama nisingeingilia kati kuokoa jahazi maisha yake yangeingia doa sana kama mjuavo mambo ya mikopo yalivo,kwa hiyo nikalazimika kumkopea bank kiasi ambacho itanilazimu nikae mwaka mzima ndo nirudi kwenye mstari.

Sasa dhumuni kuu la kuandika uzi huu ni kwamba kiasi cha fedha kinachobaki baada ya makato ni kidogo sana kiasi kwamba nashindwa hata kumhudumia mpenzi wangu huyu ambae hana ajira na kwao anaishi na mamake tu nae ni maisha ya chini tu hawezi mtimizia binti mahitaji yake.

So mpaka sasa anaonesha kunivumilia sana ingawa naona kabisa kuna namna mapenzi yetu yamefubaa na hata yeye ile moyo wa kujitoa sana kwangu dizaini umepungua na simlaum kwa hilo

Kwa hiyo wakuu binafsi inaniuma sana na sina amani kabisa kuendelea na haya mahusiano maana me nna asili ya kujali sana na najihisi vibaya kwamba hata 50k ya kubaki kumsaidia mpenz wangu kwa mwezi inashindikana.

Mwisho naombeni ushauri njia gani bora ya kumuacha huyu dada bila kumuumiza?

Samahani kwa uzi mrefu.
Kwani mazee kabla hujakutana na huyo manzi na kuanza kumhudumia alikuwa anaishi vipi na hiyo familia yake duni?

Nje ya mada:
JUZI NILIKUWA NA MAJADILIANO NA BABE ANGU AKANAMBIA UNAJUA NINI AVRIEL, TAFSIRI YA MWANAUME AKIKUAMBIA ANAKUPENDA MAANA YAKE YUKO TAYARI WEWE ULIEPENDWA UMGEUZE YEYE AWE TEGEMEZI KWA KILA KITU.
sikumuelewa kiaina, sasa mleta mada amenielewesha kwa vitendo.

Wewe uwakute watu wana maisha yao, hawakukutegemea wewe mpaka unawakuta, sasa kinachokufanya ujione ndio kila kitu kwao ni nini ilhali hata hujamuoa binti wa watu?
Halafu hapo mbona ni issue ya kumuelewesha tu huyo binti kuwa uko na wakati gani kiuchumi ili akuelewe, mapenzi sio pesa na usitumie pesa kuimarisha penzi, siku zikiisha utapata tabu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haha yani kaka hata faragha yenyewe tangu march hajataka kukanyaga hom na tuko nae mtaa wa pili tu,ndo maana nahisi kuliko kuendelea hivi na huzuni ni bora nitafute njia ya kuyamaliza tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah pole Mkuu ndo maana mi kipindi natafuta mke sikutaka ambae ananitegemea nimtoe kimaisha maana ningemwangusha tu because hata wazazi wangu sijawafanyia la maana nije nimfanyie la maana mpenzi wangu na mama ake ni ngumu sana...nilitafuta ambae anataka mpenzi wa upendo sio wa kumtoa kimaisha
 
Ni sahihi kabisa kumsaidia ndungu yake na hili naunga mkono kabisa.

Shida Ni kwamba kumwacha umpendae kwa Sababu tu umeyumba kwa kipato.kama anakupenda Haina sababu kuvunja mahusiano lakini Kama yupo kwa kuchuma pesa sawa weka kulee.....

Pesa haiwezi kuwepo Kila siku kwa ajiri yake tu, ikiwepo sawa.kama Ni wife material atavumilia Kama sio atasepa tu Wala haihitaji kuumiza kichwa namna ya kumwacha

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mtoa mada mke huyu hapa....jaribu bahati yako.
 
Ni sahihi kabisa kumsaidia ndungu yake na hili naunga mkono kabisa.

Shida Ni kwamba kumwacha umpendae kwa Sababu tu umeyumba kwa kipato.kama anakupenda Haina sababu kuvunja mahusiano lakini Kama yupo kwa kuchuma pesa sawa weka kulee.....

Pesa haiwezi kuwepo Kila siku kwa ajiri yake tu, ikiwepo sawa.kama Ni wife material atavumilia Kama sio atasepa tu Wala haihitaji kuumiza kichwa namna ya kumwacha

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani kunipenda ananipenda ile kwa keyboard hiyo nikiri wazi na naheshim pia ila mambo mengine yamekata kabisa since march so ndo maana nataka njia bora ya kuachana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake karibu wote mabomu tu.... wanakupenda ukiwa na cha kuwapa.

Ukitaka kuoa tafuta kabomu kenye walau na kazi. Hata kakikulipukia hakakudhuru saana.

Wanawake msinishambulie ametype babu yangu mzaa kaka.
Tutake radhi, mmo humu tunawalea na watoto wenu na mahari tumewalipia na harusi show tukasikamia na hamna vibarua tunawavumilia mpaka siku mkipata ilhali tunajua mtaota mapembe
Tuna upendo wa dhati sana sisi wanawake ninyi ndio mnatuvurugaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa asee maana mapenzi bila ya kuyapalilia kwa vipesa hayaendi hata kama girl anakukubali vipi

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uzushi au kwakuwa hatuwataji?
Mpo humu mnavimba wakati hata ndinga mnaemdesha kwa hisani zetu wanawake.
Ni vile mmekariri na tukisema mnadai tunawasimanga wakati jukumu ni lenu mnajishaua tu hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tutake radhi, mmo humu tunawalea na watoto wenu na mahari tumewalipia na harusi show tukasikamia na hamna vibarua tunawavumilia mpaka siku mkipata ilhali tunajua mtaota mapembe
Tuna upendo wa dhati sana sisi wanawake ninyi ndio mnatuvurugaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio mimi niliyeandika mkuu.

Kuna mwanaume mwezetu unamlea kiasi hicho na yupo humu...ana bahati mbaya maana umekwisha mtangaza.
 
Daaah pole Mkuu ndo maana mi kipindi natafuta mke sikutaka ambae ananitegemea nimtoe kimaisha maana ningemwangusha tu because hata wazazi wangu sijawafanyia la maana nije nimfanyie la maana mpenzi wangu na mama ake ni ngumu sana...nilitafuta ambae anataka mpenzi wa upendo sio wa kumtoa kimaisha
Dadangu alinishauri hili wakati flani sema ndo ivo hisia za mapenzi huangukia popote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada usimwache mpenzi wako. Hajabadilika bali ni wewe unajishtukia.
Ila wanaume sijui kwanini mkikosa hela mnakosa confidence kwa wapenzi wenu.

Wakwangu alikuwa akikosa hela utasikia kila saa " Hannah nisamehe ila mambo yakikaa sawa nitalipiza kipindi chote". Nyumbani hakai kwenye sofa akaegemea, na hapo anakaa tako moja. Kitandani mkienda kulala anaanza kukaa kwenye kona ya kitanda mwisho kabisa anatafakari.
Nashukuru Mungu niliweza kumbadilisha, sasa hivi akiwa hana hela haombi msamaha tena anaanza tuu kuniita Boss. Na mimi nakuwa nampa zile hela ninazokuwa nimezitunza akinipa. Maisha yanasonga.
 
Kwani huyo mwanamke kabla ya november mwaka jama mlipokutana alikua anaishi vipi? Kiasi kwamba wewe kuyumba kiuchumi hadi penzi lenu lifubae??

Shukuru Mungu umeoneshwa true colour ya huyo binti kabla ya kufunga ndoa. Maana imagine mna watoto wawili then ukapoteza kazi yako je mapenzi yangefubaa au ungekukimbia kisa huna pesa ...
Mwisho kabisa.. tafuta mwanamke ambaye hata ukiwa huna pesa atakusaidia upambane upate pesa zaidi sio kukuacha kisa huna hela
 
Mwenye kazi ujiandae kumuweza sasa atakusumbua si anayo pesa.

Ila huyu unayemwacha raha yake unajiendeshea.
Hofu zenu na inferiority complex tu mnajijazia.

Natamani mnngetoa ushuhuda wa namna tunavowawezesha majumbani. Hamna shukrani ninyi.

Halafu mnatuogopa sana wanawake tinaojitegemea na kuwazidi kiaina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uzushi au kwakuwa hatuwataji?
Mpo humu mnavimba wakati hata ndinga mnaemdesha kwa hisani zetu wanawake.
Ni vile mmekariri na tukisema mnadai tunawasimanga wakati jukumu ni lenu mnajishaua tu hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Natambua upendo wa pekee mlionao wanawake hasa mkiwa nacho,lakini hiyo haibadili maana kuwa wanaume ndo tulipaswa kusimama katika hiyo nafasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada usimwache mpenzi wako. Hajabadilika bali ni wewe unajishtukia.
Ila wanaume sijui kwanini mkikosa hela mnakosa confidence kwa wapenzi wenu.

Wakwangu alikuwa akikosa hela utasikia kila saa " Hannah nisamehe ila mambo yakikaa sawa nitalipiza kipindi chote". Nyumbani hakai kwenye sofa akaegemea, na hapo anakaa tako moja. Kitandani mkienda kulala anaanza kukaa kwenye kona ya kitanda mwisho kabisa anatafakari.
Nashukuru Mungu niliweza kumbadilisha, sasa hivi akiwa hana hela haombi msamaha tena anaanza tuu kuniita Boss. Na mimi nakuwa nampa zile hela ninazokuwa nimezitunza akinipa. Maisha yanasonga.
😂😂😂😂eti anakaa tako moja..

Sema sisi wanaume tukikosa pesa ni sawa na kuwa uchi aiseeh..yaani hadi mzuka wa kuongea ongea au kutembea tembea unakata kabisa..
 
Back
Top Bottom