Nivunje vipi haya mahusiano?

Nivunje vipi haya mahusiano?

Pole Sana
Tulia Hali Yako Ndiyo Hiyo Kwa Kipindi Ulichosema
Muhimu Mweleze Ukweli Ingawa Changamoto Hapo Usije Kuchukua Maamuzi Mabaya
Inaweza Kukuketea Shida

Lakini Umeonyesha Kukata Tamaa
Akijitokeza Mtu Yoyote Mchumba Anaondoka, Simama Eneo Lako Ongea Naye Na Akishindwa Kukuvumilia Mwache Aende. Ingawa Kanuni Sasa Hivi Hakuna
Tuelekeza Nguvu Sana Kwenye Pesa
Kuongea nae nimeshaongea nae na alinihaidi kunivumilia lakini kiuhalisia kabisa naona tayari kuna vitu vimeanza kuonekana na vinanitia simanzi sana na simlaum kwa kweli sio rahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jifunze kuwa Mwanaume kamili.....huu muda ambao unapitia changamoto za kifedha ndo muda mzuri wa kujua kuwa umepata mwanamke wa aina gani ndo wakati wa kupima mapenzi yake kwako kama atakuvumilia na kutokuonesha dalili za usaliti nakushauri huyo mweke ndani.

Unachotakiwa sasa hivi ni kumweleza mpenzi wako kuwa unachangamoto za kifedha hivyo kama atakuelewa na kukuvumilia mpk hapo hali yako itakapokuwa nzuri huyo ni mke.

Kingine na kushauri acha tabia za kugawa gawa pesa ovyo ukiamini ndo mwanamke atakupenda. Unaweza kumpa na yeye akawa anampelekea msela wake ambaye hana kitu lkn ndo hivyo demu kadata kwake, kwako nikukuchuna tu!

Kipindi unachopitia sasa kifedha kinakusaidia kujua type ya mwanamke uliyenaye

Sent using Jamii Forums mobile app
Sahihi mkuu ila kutokana na maisha ya muhusika na ukizingatia ni msichana ana mahitaji ya msingi kuna namna ana suffer sana mpaka najihic hasira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mbona hutaki mwenzako amuandae mke wake...!??
Hapana mkuu sijafikia hatua ya kutotaka aandae mke...hapa kijiweni tu mkuu.

Kila mmoja anatoa experince yake.

Maisha ya siku hizi magumu saana kuandaa mke. Kutana na mke aliyekwisha andaliwa huko walau amejitosheleza jikokote naye tu umalizie maisha yaliyobaki.
 
Mkuu usiwaze sana tena moyo wako wa kupenda kutoa toa sio mzuri unamuendekeza kwani lazima umpe hela kila mwisho wa mwezi,yeye ndo anafanya kazi? Kwani umemuoa,wewe ni mpenzi tu
Cha msingi mpe hela siku ukiwa nae falagha zaidi ya hapo uache kuchezea hela hovyo kwa kuwapa mabinti
 
Sasa kwanini ujisumbue...mweleze ukweli ya yaliyotokea uone kama atakaa avumilie au atakukimbia. Hata ukioa unafikiri utakuwa stable siku zote? Kuna siku utaishiwa.

Hapo umepewa nafasi ya kumpima...kama ameonyesha changes akiwa mke (kumbuka mke ana nguvu mkononi) hizo changes zitaonekana zaid ya zilivyo.

Kikubwa hakudai....useme ni deni utalipa...mwambie huna pesa kwasasa.
Nilimwambia mkuu,tangu wakati tatizo limetokea ila mpaka leo tupo pamoja ananiheshim lakin kuna vitu vimepungua sana kati yetu ndo maana japo hajanitamkia lakini naona ni bora ningepata namna ya kuyamaliza tu niwe na amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimwambia mkuu,tangu wakati tatizo limetokea ila mpaka leo tupo pamoja ananiheshim lakin kuna vitu vimepungua sana kati yetu ndo maana japo hajanitamkia lakini naona ni bora ningepata namna ya kuyamaliza tu niwe na amani

Sent using Jamii Forums mobile app
Aah hapo mute tu vimiezi viwili bila mawasiliano.
 
Mpiganie Kama anaonyesha wazi upendo kwako. Lakin jaribu kumweka wazi juu ya kipato chako kuathirika pamoja mjadili Nini la kufanya ili kuokoa jahazi.

Pesa Ni maua tu Leo ipo kesho hakuna, inabidi maisha yaendelee



Sent using Jamii Forums mobile app
Kumpigania ni pamoja na kumpunguzia ukali wa maisha hata kwa mahitaji madogo madogo haya ya 30k mwa mwezi ila siwez tena kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ndo wakati wa kupima huo upendo sasa
Habari wakuu

Mwaka huu niliazimia kuwa na mahusiano rasmi ambayo kama Mola akibariki tufike kwenye kujenga familia maana mwakani nnafikisha miaka30


Kweli mwaka jana mwezi november nilifanikiwa kuanza mahusiano na binti mmoja wa mtaa wa pili ambae kiukweli nafsi yangu ilimkubali sana tangu siku ya kwanza namuona hadi leo hii tulipo.

Lakini changamoto ni kuwa siku chache baada ya kuanza mahusiano yetu dadangu wa damu alipata shida kubwa ya kifedha ambayo kama nisingeingilia kati kuokoa jahazi maisha yake yangeingia doa sana kama mjuavo mambo ya mikopo yalivo,kwa hiyo nikalazimika kumkopea bank kiasi ambacho itanilazimu nikae mwaka mzima ndo nirudi kwenye mstari.

Sasa dhumuni kuu la kuandika uzi huu ni kwamba kiasi cha fedha kinachobaki baada ya makato ni kidogo sana kiasi kwamba nashindwa hata kumhudumia mpenzi wangu huyu ambae hana ajira na kwao anaishi na mamake tu nae ni maisha ya chini tu hawezi mtimizia binti mahitaji yake.


So mpaka sasa anaonesha kunivumilia sana ingawa naona kabisa kuna namna mapenzi yetu yamefubaa na hata yeye ile moyo wa kujitoa sana kwangu dizaini umepungua na simlaum kwa hilo


Kwa hiyo wakuu binafsi inaniuma sana na sina amani kabisa kuendelea na haya mahusiano maana me nna asili ya kujali sana na najihisi vibaya kwamba hata 50k ya kubaki kumsaidia mpenz wangu kwa mwezi inashindikana.


Mwisho naombeni ushauri njia gani bora ya kumuacha huyu dada bila kumuumiza?


Samahani kwa uzi mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua haya ni maoni yako ila sio kesi tukiyajadili.


Umpiganie mtu kwasababu anaonyesha dalili za kukupenda tu?

Binafsi nampongeza mtoa mada...kumpigani dada yake ni jambo la kuigwa kuliko kuendelea kumpigania huyu mdada mwingine wanayeunganishwa na kaupendo tu ka sex ya kitandani.
Hata kasex kenyewe sikapati tena mkuu ndo maana naona ni bora kuliko kusononeka heri nihairishe hii safari mpaka mambo yataporejea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkiachana wakati huu wa tabu then hamkuwahi kupendana.

Umekata tamaa...unahisi huyu dem ni mzigo.

Nakuonya tu. Ukimwacha itachukua muda mfupi sana kumkumbuka.

Keep holding into love.
Mkuu tunaongea vizuri ila huwez amini hata hom kuja imekua ngumu sio kama awali na najua hii hali imetokana na anaona me ndo nafaidika sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usiwaze sana tena moyo wako wa kupenda kutoa toa sio mzuri unamuendekeza kwani lazima umpe hela kila mwisho wa mwezi,yeye ndo anafanya kazi? Kwani umemuoa,wewe ni mpenzi tu
Cha msingi mpe hela siku ukiwa nae falagha zaidi ya hapo uache kuchezea hela hovyo kwa kuwapa mabinti
Haha yani kaka hata faragha yenyewe tangu march hajataka kukanyaga hom na tuko nae mtaa wa pili tu,ndo maana nahisi kuliko kuendelea hivi na huzuni ni bora nitafute njia ya kuyamaliza tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kasex kenyewe sikapati tena mkuu ndo maana naona ni bora kuliko kusononeka heri nihairishe hii safari mpaka mambo yataporejea

Sent using Jamii Forums mobile app
Practically, wanawake wanahitaji kuhudumiwa na mwanaume. Hili twende mbele turudi litabaki kuwa ukweli.

Ila,

Kuna kalakini, ukishajua hivyo jitafutie walau ambaye anaweza kukuvumilia kipindi umepungukiwa.

Au , tafuta ambaye walau amejitosheleza wewe kazi yako kujazia tu.

Sasa mkuu hata sex hupati wewe unafaidika na nini sasa? Siku hizi ni mchezo wa shinda ni shinde.
 
Wanawake karibu wote mabomu tu.... wanakupenda ukiwa na cha kuwapa.

Ukitaka kuoa tafuta kabomu kenye walau na kazi.

Wanawake msinishambulie ametype babu yangu mzaa kaka.
😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom