Niuzie Sumu....

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,948
...Mwanamke mmoja aliingia duka la dawa na kuomba auziwe sumu.

Mwenye duka akamuuliza: " Ya nini hiyo sumu unayoitaka?"

Mwanamke: "Nataka kumuua mume wangu".

Muuza duka: "Mungu wangu! Nikuuzie sumu ili ukamuue mumeo wako? Kwanza ni dhambi, na ikigundulika nitanyang'anywa leseni yangu ya biashara halafu mimi na wewe wote tutaozea jela. Mimi siwezi kufanya hivyo hata siku moja!"

Mwanamke akatoa picha toka kwenye pochi yake, akatoa picha ya mume wake akiwa uchi na mke wa muuza duka na kumuonyesha muuza duka.

Muuza duka baada ya kuiona picha: "Ah! Kumbe umeandikiwa na daktari! Basi utapata hiyo sumu, tena ile kali kabisa. Si ungeniambia hilo tangu mwanzo?"
 
Hahahahaha,alaf wakaendeleza libenekee,muuza sumu na mnunua sumu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom