- "Ni mafanikio gani ambayo una fahari nayo zaidi na kwa nini?"
- "Ni ushauri gani bora uliowahi kupokea?"
- "Ni nani ambaye amekuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa katika maisha yako?"
- "Ni kitu kipi kuhusu wewe kinachowashangaza watu?"
- "Kama ungeweza kutatua tatizo moja katika ulimwengu, lingekuwa lipi?"
- "Ni kitu kipi unachotamani ungeweza kuwa bora zaidi nacho?"
- "Unashughulikiaje msongo wa mawazo au shinikizo?"
Vizuri sana.
Naomba nikujibu kama ifuatavyo.
1. Mafanikio yangu ambayo ninayafurahia mpaka sasa ni kuachana na biashara ya kuuza mwili na kuamua kufungua ofisi yangu ndogo ya kutengeneza batiki hapa Ubungo.
Kwa sababu sikuweza kuamini kama ipo siku nitashika pesa yangu ya halali
2. Ushauri bora ulitoka kwa marehemu bibi yangu aliyekuwa ananilea tangu mchanga, aliniambia siku moja "
kutokupata kwako mtoto usichukulie kama umepoteza kila kitu duniani maana wapo waliofanikiwa na hawana watoto"
3. Marehemu bibi yangu, alinilea tangu nazaliwa maana sikuwahi kumjua mama yangu mpaka hapa nilipo.
Alilea familia kubwa kuliko uwezo na kipato chake lakini alitupambania mpaka sisi kukua na kwenda kufanya maisha mengine nje ya kijiji.
Nilijifunza vingi kupitia kwake.
4. Kikubwa ambacho watu wanashangaa kuhusu mimi ni kuacha kazi ya kujiuza ambayo nilikuwa naweza kuingiza hadi Tsh laki 5 kwa siku (
mbali ya kazi na kuiba pia kupo) na kuamua kufungua banda dogo la kutengenezea batiki.
Wanashangaa kwa maana kazi ya batiki si lelemama na haina faida kama ile niliyokuwa nafanya awali.
Lakini nimeweza na ninaendelea na maisha mpaka sasa.
5. Kutibu na kuponesha kabisa ugonjwa wa saratani.
6. Mtoto tu, natamani sana nipate mtoto sana.
Lakini haiwezekani tena.
7. Kwa sasa nimeshaizoea hii hali ya kutopata mtoto tofauti na awali.
Nimeikubali hii hali na ninaishi nayo sasa.