Niulize, Nipongeze, Nikosoe, Nishauri

Niulize, Nipongeze, Nikosoe, Nishauri

Why?
Una tatizo la kiafya au shida nini.
Gyna
Nilipata saratani ya shingo ya kizazi, kutokana na umaskini na hali ngumu ya nyumbani kwetu sikuwa na uwezo wa kupata mionzi ya kukausha na hali hiyo ilipelekea saratani kula mpaka mji wa mimba nadhani.
Na katika mapambano ya kuokoa maisha yangu ikabidi nitolewe kizazi.
Sidhani sababu kuu ilikuwa nini mpaka kupata saratani
 
Leo Nusratt Mohammed nimepata nafasi kuliko siku zote tangu nimejiunga humu JF (Jamii Africa).

Hivyo basi kutokana na jambo hili natoa nafasi kwa member yeyote aliyepo MMU:-
Kuniuliza Swali,
Kunikosoa kwa lolote,
Kunishauri Chochote,
Kunipongeza kwa lolote.

ILA:
Maswali yasiyo na tija na yasiyo na mrengo wa MMU sitayajibu,

Maswali yatakayodhalilisha jukwaa sitayajibu,

Maswali ya kipumbavu na ya kipuuzi sitayajibu,

Maswali yaliyo nje ya uwezo wangu pia sitayajibu.

Kuna wale walio kwenye ignore list yangu, hao nao sitaweza kujibu maswali yao (wanajijua)

Nipongezeni, nishaurini, nikosoeni ili niweze kujirekebisha maana kuna watu humu wana hasira sana na mimi wakati sijawakosea lolote.


Najua kama nchi tunapitia kipindi kigumu sana nyakati hizi, ila tunaomba tuvumiliane tu wapendwa.

Mimi nawapenda sana wanajukwaa wa JF (JA)
Allah aendelee kutusimamia katika mapambano ya utafutaji wa riziki zetu.

Jioni njema.

View attachment 3315319
nina maswali madogo mawili tu kwa sasa kwa faida ya wadau.,

ni lini hasa ulianza rasmi kuvaa vigodoro, na je una mpango wa kuacha hivi karibuni?🐒
 
Nilipata saratani ya shingo ya kizazi, kutokana na umaskini na hali ngumu ya nyumbani kwetu sikuwa na uwezo wa kupata mionzi ya kukausha na hali hiyo ilipelekea saratani kula mpaka mji wa mimba nadhani.
Na katika mapambano ya kuokoa maisha yangu ikabidi nitolewe kizazi.
Sidhani sababu kuu ilikuwa nini mpaka kupata saratani
Sijui uwezo wako kifedha ila kuna njia ya kupata mtoto.
surrogacy
 
Unaona umuhimu wowote wa mwanaume kwenye maisha yako ?

Unaamini ukiwa mama wa nyumbani ndo kuwa mke Bora kwa mumeo ?

Unawaambia nn wadogo zako wanaoamini dating na wababa wametoboa kimaisha ?
Ndio, kwa upande wangu ninaona umuhimu wa mwanaume.
Japo nilidhalilika ila nimeshasahau.

Hapana, kuwa mama wa nyumbani hakukufanyi kuwa mke bora kwa mumeo.
Kuwa mama bora ni zaidi ya kuwa mama wa nyumbani.
Mke bora ni yule anayemtii na kumuheshimu mume kwa madhaifu na mapungufu yake.
Wapo wamama wa nyumbani wengi sana na hawana ubora wowote katika ndoa zao.

Unajua katika hali ya sasa ya kiuchumi, kila mtu anapenda kuishi maisha mazuri.
Naona suala la kudate na wababa si jambo baya au zuri ni vile tu kama utatimiziwa malengo yako na kuwa na heshima kwa mubaba wako 🙂
 
Back
Top Bottom