Nitumie njia gani kupanga bei za bidhaa zangu?

Akili kali united

New Member
May 12, 2024
3
0
Hello....

Habari za muda huu.

Je, huyu ni wewe?

Unajiuliza ni njia gani utumie kupanga bei ya kuuzia bidhaa zako? Kwenye upangaji wa bei kuna factor nyingi za kuziangalia mfano.

1. Washindani wako katika soko.
2. Kipato cha wateja wako.
3. Mazingira ya soko.

Ila leo nitazungumza kupanga bei kwa kutumia njia ya QUEEN OF SHEBA kwenye kupanga bei ya kuuza huwa tunatumia kanuni ya %.

Hii kanuni izingatie saaaaaaana. Sasa hapa unatakiwa kujua unataka % ngapi ya faida.

Mfano unataka 30% ya faida na bei ya manunuzi ni 5,000. Swali linakuja je niuze bei gani ili niweze kupata faida ya 30%?

Kumbuka tuna manunuzi 5,000, faida tunayotaka ni 30%. Je, bei ya kuuzia ni ipi?

Kanuni:
Chukua 100 toa asilimia unayotaka. Chukua 100 gawanya kwa jibu ulopata. Zidisha bei ya manunuzi kwa jibu la mwisho kabisa. Hiyo ndo itakuwa bei ya kuuzia.

Twende kwenye mfano wetu wa juu.

1. Manunuzi 5,000
2. Faida 30%

Turudi kwenye kanuni.

1. 100-30= 70
2. 100÷70= 1.42
3. 1.42×5,000
4. 7,100 hii ndo bei ya kuuzia.

So hapo ukiuza 7,100 unapata faida 30% ambayo faida ni sawa na 2,100 hapo. Sijui umenipata?

Imedhaminiwa Na Akili Kali United

Payless 0654208515
Kijana mpole +255785408249
Cusho creatives +255 😁
 
Ni swali unataka majibu au ni shule unataka utufundishe?
Ila mkuu tumekupata vilivyo ubarikiwe.. ila hiyo namba imekaa kimtego?
 
tsh 2100 aiwezi kuwa faida labda uwe machinga.

Kama ni duka kuna mshahara
Bill ya umeme
Tozo za halmashauri
Kodi ya pango kama unakodisha.

Halafu hesabu zako hazina VAT ndio maana baadae mnaanza kulalamika TRA inawaonea.

Ujatoa VAT ya kununulia na kuweka yako baada ya kupanga ndio maana uwa mnalalamika ukiweka VAT bei inakuwa kubwa kumbe tatizo hesabu zenu tu.

Halafu faida ya 30% ya 5000 ni tsh 1500 sio 2100
 
Back
Top Bottom