Nitumie njia gani ili YouTube iweze kuninufaisha zaidi?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,483
40,500
Wakuu habari,

Kuna kampuni ndogo nategemea kuianzisha hivi karibuni, ambayo baadhi ya kazi zake zitakuwa zikionyweshwa huko 'youtube'; mpango mzima wa kuandaa maudhui utakuwa ni huku Tanzania, ila watengenezaji watakuwa ni huko bara la Asia.

Nikimaanisha ili nipate kazi kamili, lazima niwalipe ao watu wa nje; bahati nzuri nipo nao kwenye mazunguzo ya kulifanikisha hilo.

Changamoto niliyoiona katika kufanya utafiti kwenye majukwa ya huko nje, wanasema nchi ambazo 'you tubers' wananufaika vizuri ni USA, UK, Canada; na mimi lengo langu nataka ninufakie vizuri, kwa sababu hawa watu wa nje nitakuwa nawalipa kwa fedha za kigeni.

Swali, nitumie njia gani ili 'youtube' iweze kuninufaisha zaidi? Je, mafao yanatokana na nchi hiyo chaneli ilipo au, kama sio, kwa nini waseme USA, Canada, na UK ndio inalipa zaidi?

Malengo yangu ni kupata faida kubwa.

Karibu kwa maoni.
 
Karibu kwa maoni.​
Tumia lugha ya Kiingereza uwavute audience wa nje ya nchi, ndo kuna hela, wazungu wanaclick ads. Pesa ziko kwenye ads.

Wabongo hawaclick ads, wanaskip,hela unalipwa kidogo. Waulize wote wanaotumia lugha ya kiswahili YouTube.
 
youtube inapata hela kupitia yale matangazo yanayooneshwa kwenye video, sasa hiyo hela wanagawana na mwenye video husika, ambaye ni wewe....

watangazaji ambao sasa wananunua matangazo yaoneshwe kwenye hizo video, wanalipa zaidi matangazo yao yaoneshwe kwa watu kutoka nchi zilizoendelea, hii ni kwasababu wana kipato kikubwa zaidi, hivyo uwezekano mkubwa zaidi wa kununua kinachotangazwa(buyer intent)

video yenye 1M views iliyoangaliwa sana na wazungu itaingiza pesa zaidi kuliko video yenye 1M views iliyoangaliwa na wabongo

we jiulize, ushawahi kununua kitu kwa kuona tangazo la youtube?

youtube ya tz haina matangazo kivile, washa vpn utumie youtube za wazungu uone....

karibu kwa maswali
 
Lenga india.
Ndio nchi yenye watu wengi duniani wanaoingia online kwa siku maana internet bei iko chini.

Fungua channel, kwa siku mbili mfululizo kabla hujaupload video yoyote angalia video kama mia za kihindi youtube. Itakusaidia kupata recommendations za traffics za india
Lugha itakuwa ni ya ki-ingereza; na itaonekana kila sehemu; nilitaka nijue, Je sehemu ya kusajilia hiyo chaneli (nchi) ni muhimu katika kupata faida? ili kama ni kuifungua niangalie ni wapi ifunguliwe/isajiliwe.​
 
youtube inapata hela kupitia yale matangazo yanayooneshwa kwenye video, sasa hiyo hela wanagawana na mwenye video husika, ambaye ni wewe....

watangazaji ambao sasa wananunua matangazo yaoneshwe kwenye hizo video, wanalipa zaidi matangazo yao yaoneshwe kwa watu kutoka nchi zilizoendelea, hii ni kwasababu wana kipato kikubwa zaidi, hivyo uwezekano mkubwa zaidi wa kununua kinachotangazwa(buyer intent)

video yenye 1M views iliyoangaliwa sana na wazungu itaingiza pesa zaidi kuliko video yenye 1M views iliyoangaliwa na wabongo

we jiulize, ushawahi kununua kitu kwa kuona tangazo la youtube?

youtube ya tz haina matangazo kivile, washa vpn utumie youtube za wazungu uone....

karibu kwa maswali
Hili nimemwambia tayari. Atumie lugha ya Kiingereza.
 
Tumia lugha ya Kiingereza uwavute audience wa nje ya nchi, ndo kuna hela, wazungu wanaclick ads. Pesa ziko kwenye ads.

Wabongo hawaclick ads, wanaskip,hela unalipwa kidogo. Waulize wote wanaotumia lugha ya kiswahili YouTube.
Kama hajui kiingereza, anaweza kutumia text to sound converter. Zipo Ai na website nyingi tu. Unagugo maneno, ynataweka kwenye apps za kubadili kuua copyright, unachagua sauti ya dada wa kihindi au kichina anayasoma ukipenda unaweka na autocaption ukiwa mvumilivu lazima utoboe.
 
Back
Top Bottom