Nitawashangaa sana AU wakikubali mapinduzi Zimbabwe!

Nitawashangaa sana AU wakikubali mapinduzi Zimbabwe!

Ziko njia za kidemokrasia za kumpumzisha
Bw eeh, acha kuzungusha maneno.
Ni mara ngapi katiba ya Zimbabwe imekojolewa, hasa linapokuja suala la uchaguzi?
Kuiba kura na kung'ang'ania madaraka, ndiyo demokrasia?
Wanajeshi waliomsweka Mugabe ndani, wametangazia umma kuwa wao hawana nia ya kuchukua madaraka, bali wana restore katiba na demokrasia.
Inamaana hapo utaitishwa uchaguzi wa kidemokrasia nk nk, kuliko hali ilivyokuwa imefikia kutaka kumpatia mdaraka mke wake wanayelala naye kitanda kimoja.
 
Aisee ni kweli, mwenendo wa Emerson na wazungu ulikuwa ni wakutiliwa shaka hivi karibuni ndio maana mugabe alimuonya na bado hakusikia...
(wazungu wapo nyuma ya Emerson)

Kuliko udikteta afadhali Mugabe aondolewe madarakani. Jeshi la Zimbabwe limefanya jambo jema. Ya Zimbabwe ni salamu kwa madikteta waliopo Afrika.
 
Ushangae nini wamwondoe haraka we unaona katika Zimbabwe nini yeye tu mwenye uwrzo a kuiongoza Zimbabwe? antaka afie madarakani shame to him and u. Tamaa za kipumbavu yani sisi waafrika tuna tamaaa mno za madaraka ubinafsi wa ajabu mno hata ubinafsi waliokua nao wazungu sio kama sisi tungekua na Akili kama mzungu hakika tusingetoa ujuzi wowote kwa wengine Mugabe anatakiwa aondoke kimya kimya ni aibu miaka karibu mia
 
Kwenda sokoni na kapu la fedha kununua mboga unataka muujiza gani mwingine?
Mimi huwa nawashangaa watu kila kitu kumsingizia mzungu, Mugabe kauwa uchumi wa Zimbabwe wazungu alishawafukuza kagawa ardhi sasa ana kisingizio gani cha kuuwa uchumi? halafu wanakuja watu hapa kumtetea huyu mzee. hapa juzi ilisemekana dola imepanda tu ikiwa kama kiama kimetokea huyo Zimbabwe mpaka pesa yao wameitupa halafu unakuja kumtetea huyu mzee. pesa ya Zimbabwe wanafungia chapati bado unakuja kumtetea.
 
Wewe si uende ukawaonye Wachina kama una weza. AU ya siku hizi sio ya kipindi cha Nyerere ndugu yangu. Ukifanya upuuzi wako usitegemee utasaidiwa chochote toka ndani ya umoja huo. Kumbuka mambo yote yanayotokea ndani ya nchi zetu siku hizi yana anikwa wazi wazi na hakuna siri. Maisha magumu ya Zimbabwe ya kubeba gunia la noti kwenda kununua paketi ya chumi kila mtu anayaona. Tanzania vile vile, Usifikiri yote yanayofanywa hadharani na Rais wetu hayaonekani huko AU unakowashwa washwa na kukutaja taja. Dunia ya leo sio ya Saddam wala Gaddafi. Huko Lebanoni rais anatolewa mkuku, Saudi mfalme anawa funga mpaka watoto wake. Chungeni sana nyakati mnazopewa na mzitumie vizuri na si kwa mabavu. Nguvu na ubabe vimepitwa na wakati. Wakati ukifika hakuna cha msaada toka AU wala UN, UNAKUFA NA MZIGO WAKO BEGANI.
 
Kilichotokea Zimbabwe ni mtifuano ndani ya chama tawala,wapinzani hata hawahusiki,na hamna hata pressure kutoka nje,wananchi walikuwa wameshamchoka,na inaonekana chama chake pia ilimchoka
Umeongea hali halisi na si ushabiki.
 
Mimi nawashangaa Wazimbabwe kwa nini imewachukua muda mrefu hivi kumng'oa huyo kibabu!!

Ilifika wakati watu walianza kushindia majani na nyama za panya!!

Huyo kibabu alipaswa kuwa keshaondolewa muda mrefu sana.
Nchi wanapeana na mkewe inamaana Wazimbabwe wote hamnazo?
 
Itabidi tupeleke vikosi vyetu huko. Sisi ni wapenda amani,Mugabe pia ni ndugu etu amekuja mara nyingi kwenye sherehe zetu za uhuru na kuapishwa marais wetu.
 
Hizi habari si nzuri sana hapa nyumbani. Kuna watu matumbo yanawaka moo wakiona rafik yako kafungiwa sehem
 
Kwani Al Sisi Wa Misri haiingii kwenye vikao vya AU!?
 
Africans ndo tulivyo, mnakumbuka Mugabe aliwang'oa wazungu kwa sababu gani? Ile ardhi aliwapa kina nani? Ndugu zake? Leo mnashabikia eti Dikteta anang'olewa
 
Wazungu huwa wanaplan mambo yao hata miaka 100 mbele....walipandikiza taratibu vibaraka wao weusi kuvuruga Uchumi wa Zimbabwe...na leo point ndo hiyo...ila Mugabe alikuwa na lengo zuri tu kwa watu wake
 
Hata jeshi la Zimbabwe huenda halijui kama top Officers wapo wa CIA, NSA e.t.c ila ni weusi kabisaaa
 
Back
Top Bottom