Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 7,290
- 11,805
Kwenye maisha ya mwanadamu hapa duniani, pesa sio kila kitu… lakini ukweli usiosemwa mara nyingi ni kwamba pesa inatatua karibu asilimia 99% ya changamoto tunazokutana nazo. Ukikosa pesa kwenye dunia ya sasa, ni kama umejitenga na mfumo mzima wa maisha. Unakuwa kama unaishi pembeni ya dunia halisi.
Fikiria hili…
Ukiwa na pesa, una uwezo wa kupata huduma bora za afya, kula vizuri, kuishi sehemu salama, na hata kupata heshima fulani kwenye jamii. Lakini ukikosa pesa, hata mahitaji ya msingi yanakuwa vita. Unaanza kuona dunia kama inakuonea, kumbe mfumo wake ndio uko hivyo.
Wakati mwingine maisha yanakupiga sana…
Unaweza ukajituma kwa nguvu zote - unaamka mapema, unapambana mchana kutwa, una ndoto kubwa - lakini matokeo hayaonekani. Unachoka, unakata tamaa, unaanza kujiuliza kama kweli kuna mwanga mbele. Watu wanakuja wanakupa moyo, wanakuambia “subiri muda wako,” lakini ukweli ni kwamba bills hazisubiri muda wako ufike.
Na hapo ndipo wengi hukosea…
Wanaanza kuzoea hali. Wanajituliza na kusema “haya ndiyo maisha.” Lakini ndugu yangu, kuna vitu hupaswi kabisa kuvikubali kama sehemu ya maisha yako - na kimojawapo ni umasikini. Umasikini sio destiny, ni hali inayopaswa kupingwa kwa nguvu zote.
Ukikosa pesa, madhara yake hayaishii kwenye tumbo tu - yanaenda mbali zaidi…
Unaweza kupoteza marafiki. Wale uliokuwa nao karibu wanaanza kupotea taratibu. Sio wote ni wabaya, lakini ukweli ni kwamba wengi wanavutiwa na mazingira ya mafanikio. Ukianza kushuka, wanajitenga kimya kimya.
Hata ndugu nao hubadilika…
Wale waliokuwa wanakuona kama msaada wao, ghafla wanakuona mzigo. Simu zako hazipokelewi kwa haraka kama zamani. Mialiko inapungua. Unaanza kujiona kama huna thamani tena kwenye ukoo au familia.
Heshima inapungua…
Jamii nyingi zinaheshimu matokeo, sio juhudi. Unaweza kuwa mtu mwema, mwenye moyo safi, lakini kama huna pesa, sauti yako haisikiki sana. Watu wanakuchukulia kawaida, wengine wanakuona kama hauna mwelekeo.
Na kibaya zaidi…
Ukikosa pesa kwa muda mrefu, hata confidence yako inaanza kupotea. Unaogopa kujaribu vitu vipya, unaanza kujiona mdogo, unaanza kuamini labda wewe sio wa kufanikiwa. Hapo ndipo hatari kubwa ilipo - unapopoteza imani na wewe mwenyewe.
Lakini pamoja na yote hayo…
Mapambano ya pesa hayapaswi kukufanya upoteze utu wako. Usikubali pesa ikufanye uwe mtu wa kuumiza wengine, kudhulumu, au kupoteza maadili yako. Maana pesa bila utu, ni hatari kwa jamii na hata kwako mwenyewe.
Pambana…
Pambana kwa akili, sio nguvu tu. Tafuta maarifa, jifunze skills, badili mbinu kama mambo hayaendi. Dunia ya leo haitaji nguvu pekee, inahitaji ujanja na uelewa wa mifumo ya pesa.
Tambua hili…
Hakuna mtu atakayekuja kukuokoa. Maisha yako yapo mikononi mwako. Na kama kuna kitu hupaswi kuvumilia katika maisha haya - basi ni kukaa bila hela.
Ntavumilia yote… lakini sio kukaa bila hela.