Nitateua Makatibu Wakuu wa Wizara Wanajeshi waliokula Kiapo cha Kifo nikishika hatamu

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Sep 10, 2022
1,282
2,508
Wakuu

KIFO ndio fumbo pekee ambalo wanadamu tunaogopa. Watu hawaogopi tena kifungo cha Maisha jela wala faini zinazolipika.

ILI kuongeza tija kiutendaji na kuepuka ubadhirifu, wizi na UFISADI katika wizara mbalimbali nchini,ipo haja ya kuteua kada ambayo itakula kiapo cha KIFO!kabla ya kukabidhiwa kusimamia fedha za miradi ya Jamhuri.

Na kada yenye nidhamu hiyo ni wanajeshi pekee ambao wanauwezo wa kula kiapo hicho,nadhani sheria kali kama hii itaondoa kelele za ubadhirifu zinazoripotiwa na VYOMBO mbali mbali nchini!

Hili litatokea iwapo nikipewa FURSA ya kushika hatamu hapo Baadae kwa maslahi ya jamuhuri yetu!

Mungu IBARIKI nchi yetu Tanzania niipendayo Sana!
 
Another Rubbish...

As if dunia nzima hakuna mifano ya nchi zinazo ongozwa vizuri za kujifunza?

Sweden wanateua wanajeshi?Norway wanateua wanajeshi....mawazo ya kizamani sana haya very expired mind
ILI tufike huko unakozungumzia lazima tuanzie Hapa!!

Kuna gharama za kulipa kabla ya huo ustaarabu haujatufikia!!

Mi naona kuna umuhimu wa hati hiyo kusainiwa ILI kutia nidhamu kwenye fedha za umma!!

Hii ni jamuhuri sio ukoo wala genge la WATU FULANI!!
 
Wakuu

KIFO ndio fumbo pekee ambalo wanadamu tunaogopa. Watu hawaogopi tena kifungo cha Maisha jela wala faini zinazolipika.

ILI kuongeza tija kiutendaji na kuepuka ubadhirifu, wizi na UFISADI katika wizara mbalimbali nchini,ipo haja ya kuteua kada ambayo itakula kiapo cha KIFO!kabla ya kukabidhiwa kusimamia fedha za miradi ya Jamhuri.

Na kada yenye nidhamu hiyo ni wanajeshi pekee ambao wanauwezo wa kula kiapo hicho,nadhani sheria kali kama hii itaondoa kelele za ubadhirifu zinazoripotiwa na VYOMBO mbali mbali nchini!

Hili litatokea iwapo nikipewa FURSA ya kushika hatamu hapo Baadae kwa maslahi ya jamuhuri yetu!

Mungu IBARIKI nchi yetu Tanzania niipendayo Sana!
We umechemka,nenda bohari ya dawa(MSD) uliza madudu alivyofanya Meja General Mhidze mpaka SSH akamuondoa Kwa aibu.Acha,hao Jamaa wabaki na kazi zao za Medani
 
We umechemka,nenda bohari ya dawa(MSD) uliza madudu alivyofanya Meja General Mhidze mpaka SSH akamuondoa Kwa aibu.Acha,hao Jamaa wabaki na kazi zao za Medani
Alikula kiapo cha KIFO iwapo akihusika na HAYO!!?

Si angelikuwa KWA Baba mwenyezi huko akiimba mapambio!!?

Kiapo cha KIFO mkuu!akiapa hawezi risk life KWA wizi akiiba anakula ya kichwa!!
 
Na kada yenye nidhamu hiyo ni wanajeshi pekee ambao wanauwezo wa kula kiapo hicho,nadhani sheria kali kama hii itaondoa kelele za ubadhirifu zinazoripotiwa na VYOMBO mbali mbali nchini!
Purely "Wrong footing". Pitia upya makablasha yako, na kama hayatoshi hayo makablasha azima kwa Ndugu Paskali Mayalla anayo humu jamvini.

Jikite kujua tulianzaje kufika katika Hali iliyokufanya ufikirie na kuandika maneno hayo hapo juu niliyonukuu. Baada ya hapo rejea Tena mpango kazi wako.
 
Hakuna nchi inaongozwa na wanajeshi ikafanikiwa. Hivi ulishawahi kaa na wanajeshi hao wenye vyeo vikubwa ukaona akili zao zilivyo?

Hata hivyo unaota
Sijasema kuongozwa kijeshi nimesema makatibu wakuu wa wizara!wawe wajeda waliokula kiapo cha KIFO KWA jamuhuri kuzuia ubadhirifu kwenye wizara ZAO!
 
Kusaini kuuawa hakumaanishi kuogopa kuuawa.

Kuna uwezekano yule ambaye hajasaini kawa muoga zaidi ya aliyesaini.

Nasema Kuna uwezekano sijasema nimedhibitisha, tafadhali.
Akiuawa itakua fundisho KWA wengine ILI fedha za jamuhuri zi heshimiwe!

Watumishi wanafanya fedha za jamuhuri kama fedha za ukoo wao!!
 
Back
Top Bottom