Nitarudi tena nchini Kenya

Ugumu wangu

JF-Expert Member
May 6, 2021
1,613
2,000
2343160_IMG_20200309_155937_694.jpeg

Vile nakufanyia vurugu ili urudi kuleta storyπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
1,255
2,000
Tuendelee

Basi nilichukua lodge jioni hiyo kwa ajili ya kupumzika,wakati huo hapo Migori kulikuwa na hali ya hewa ya kawaida sana na hakukuwa na baridi japo mazingira yalionyesha ni mji wa baridi,nadhani ilikuwa kipindi cha joto.

Niliendelea kukaa nje ya ile lodge huku nikitazama mazingira ya Migori namna yalovyovutia,kiukweli pale Migori ndipo sasa nilianza kuwaona wanawake wazuri kiasili wenye type ya lupita Nyong'o,ile county ya Migori imejazwa na wenyeji ambao ni waluo(JALUO),jamani labda tu niwaambie ya kwamba,kama hujabahatika kufika Kenya hebu nenda tu ukatembee halafu utaleta hapa majibu kwa maana mimi mwenzenu nilibaki nawashangaa wale wanawake wa kiluo pale Migori,siyo kwamba Tanzania hatuna wanawake wazuri,la hasha!,nadiriki kusema ya kwamba Tanzania tunao wanawake wazuri ila kiukweli naona kama wenzetu wamebarikiwa kuwa na wanawake wazuri.

Kwanza,ni wanawake warefu kwenda juu,pili wamejaaliwa nyama za kutosha,tatu ni wazuri wa asili ambao wana rangi moja tu ambayo ni nyeusi(black),nilipoenda huko ndipo nikafahamu ya kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee afrika mashariki ambayo wanawake wake(si wote bali wengi) wana rangi mbili.
Wenzetu wao rangi yao ni moja tu!,sikubahatika kumuona mwanamke mweupe hapo Migori na kama walikuwepo basi ni weupe wa kuzaliwa nao!!,Siyo kama huku kwetu mwanamke anazaliwa mweusi lakini akienda you-dsm au you-dom anarudi amekuwa mweupe.

Sasa kuna kitu kilinishangaza sana ambacho nilijaribu kuwauliza wenyeji ili kupata majibu.Nilipofika hapo Migori karibia kila mwanamke niliyekuwa nikimuona alikuwa amevaa mini sketi(ki/vi-mini),sasa kumbe wenyeji wao walishazoea ile hali na wanaona ni kawaida tu!,mimi niliyetoka nchi ambayo kila mwanaume akipishana na mwanamke mwenye shepu matata lazima ageuze shingo,kiukweli nilipata taabu!,pia hata jamaa yangu aliniambia biashara ya nguo za kike hasa mini sketi kule zinalipa sana na soko ni kubwa,hivyo kama unasoma uzi huu na una mtaji wa kutosha hebu fanya biashara ya nguo za kike na peleka huko,kuhusu wenyeji mimi nitakupatia namba za wenyeji kadhaa ambazo ninazo na utajenga urafiki ili uone wapi pa kuanzia.

Asubuhi palipokucha niliamka nikaingia kwenye mgahawa mmoja ulikuwa jirani na hapo lodge nilipolala kwenda kupata chai ya strungi!,ile nimeingia ndani nikakutana na jamaa wamevaa magwanda ya kijeshi kama wote huku wakinitazama,sasa kumbe wale jamaa walikuwa ni askari na hao askari wa kikenya ndivyo wanavyovaa,ile lodge kumbe ilikuwa jirani na kituo cha polisi kikuu cha hapo migori na huo mgahawa ndiyo huwa sehemu yao ya kupata vifungua vinywa!,basi sikuwa na wasiwasi kwasababu niliingia Kenya kihalali,bahati nzuri hakuna aliyenighasi!.

Nilipomaliza kunywa strungi nililipa nikaondoka zangu kuelekea stage(stendi ya bus),sasa wenzetu vituo vya magari wanaita "stage" na siyo "stendi" kama tulivyozoea huku kwetu.Pia kule hakuna ma-bus makubwa kama huku kwetu,kule wanatumia Hiace ambazo wanaziita "shuttle" au "matatuu".
Basi nililipa nauli kutoka hapo Migori kuelekea Kisumu ambapo ni Ksh 600,kutoka hapo Migori mpaka Kisumu ni takribani masaa 3,hizo shuttle zikiisha jaza hapo stage(stendi)zinaondoka na kwenye gari hakuna mtu anayeitwa Konda(kondakta),huu utaratibu niliupenda sana,natamani tujitahidi na huku kwetu ungekuwepo.

Wakati nikiwa kwenye gari jamani uongo dhambi,mimi nilikuwa nikiwashangaa wanawake tu wanavyopita wakiwa ndani ya vi-mini huku wakitepesha nyama zilizoshikilia makalio yenye haja(Lazima nirudi Kenya).
Ndugu zangu watanzania,nilichojifunza hapo Migori ni kwamba,wakenya wanapiga kazi na wala siyo mchezo,hawana muda wa kupiga stori na mtu,nilikuwa nikiangalia sehemu ambazo bodaboda wanapaki lazima utakuta kuna vibanda vizuri ambavyo vimejengwa kwa ajili ya kuwasitiri kwenye mvua na jua,siyo kama Tanzania bodaboda wanaishi kama majambazi kutwa kufukuzana na polisi barabarani.

Safari ya kuelekea Kisumu ilianza sasa,nashukuru Mungu nilikaa siti ya mbele ya ile Shuttle,hivyo nilikuwa naangalia mandhari nzuri ya ile miji niliyopita,Kuanzia pale migori kuelekea Kisumu sikuona kitu kinachoitwa "Nyumba ya nyasi",narudia tena kuanzia pale Migori mpaka Kisumu sikuona nyumba ya nyasi,nyumba za tope zipo nyingi sana lakini huwezi kukuta zimeezekwa kwa nyasi,nyumba zote hata kama niza tope zilikuwa zimeezekwa kwa nyasi!,nilimuuliza dereva wa ile shuttle akaniambia kwamba " Huku kwetu kuezeka nyumba kwa nyasi ni ishara ya laana,hivyo hakuna mluo anataka laana kwenye boma yake".

Hayo ndiyo maneno aliyoniambia dereva wa ile shuttle,pia aliendelea kuniambia kwamba,bei ya bati Kenya ni nafuu sana ambayo kila mwananchi anaweza kuimudu na ndiyo maana huwezi kuona nyumba ya nyasi,ndugu zangu kwa ambao wamefika huko wanaweza wakaweka hapa shuhuda hizi ninazo zisema.

Kuhusu barabara kiukweli ndipo nilifahamu viongozi wetu wanatutania watanzania,ile barabara ya kutokea Migori kwenda Kisumu ilikuwa ni pana sana kiasi kwamba ukii-compare na barabara ya morogoro Road inayoanzia kibaha,basi inaingia mara moja na nusu kwa ukubwa.Ule mji wa Migori kiuhalisia unaizidi miji mingi tu hapa Tanzania kwa uzuri.
Tulitembea kwa umbali mrefu huku nikiendelea kushangaa mandhari nzuri za ile nchi,nilichobaini pia kule mtandao wa simu wenye nguvu ni Safaricom,mitandao ipo mingi lakini huwezi kuona ikiwa imetapakaa kama huku kwetu,Safaricom niliambiwa kule ndiyo kila kitu na wananchi wanaupenda sana kwasababu una huduma za uhakika,siyo kama huku kwetu ma-mitandao ni mengi lakini kila siku wananchi wanalalamika kuhusu huduma mbovu na serikali ikiwa inakodoa macho tu isijue cha kufanya!
Pia nilikuta mavazi yenye nembo ya "WCB WASAFI" yanavaliwa kama njugu,bado sijajua hawa watu wa wasafi kama wanalifahamu hili jambo ama la!,yaani vijana karibia wote niliyokutana nao basi lazima utakuta kavaa shati au sweta lenye nembo ya "WCB WASAFI",mimi kuhusu mavazi pia nahitaji nirudi huko kuanzisha hiyo biashara na wala sijachelewa maana jamaa aliniambia nguo huko zinalipa sana hasa za kike!,ndugu zangu mnaofanya kazi ya kuuzia dada zetu nguo nzuri hapo Mwenge hebu ingieni kule mkajionee na mtanipa mrejesho,msiendelee kulalamika biashara imekuwa ngumu wakati wenzetu wanauhaba wa mavazi mazuri!!,kuhusu mtu wa kuwapokea nitawapatieni mawasiliano!.

Pia wakati tukiwa njiani tunaelekea kisumu sikuona ma-bar kabisa,siyo kwamba wao hawanywi pombe,la hasha!,wanakunywa sana ila jamaa aliniambia kwa kule ma-bar yanapaswa yawe ndani siyo nje!!,nikawa najiuliza hebu anzia pale kibaha maili moja kama unaelekea mjini Daslam umejionea ma-bar mangapi barabarani,yawezekana hata yakawa zaidi ya 10000,sasa hiyo kitu huwezi kuikuta kule!.

Kilichonishangaza zaidi ni kutokuona kabisa mabango ya "dawa za kuongeza nguvu za kiume",narudia tena huwezi kuona!!,Jamaa aliniambia ukiona hilo bango mahali,basi tambua kuna mjanja katokea bongo kapeleka utapeli huko,lakini wao hawana huo muda wa kubandika mabango ya dawa za kuongeza nguvu za kiume kwasababu ni mashababi ki-kweli kweli(kuna kisa nilikishuhudia Kisumu usiku nitakieleza vizuri,hapo ndipo nikagundua jamaa kweli ni mashababi kwasababu yule mwanamke asingeokolewa na meneja wa ile lodge jamaa alikuwa anamuua kwa mkuyenge)

Nitarudi baadae kidogo

Kwa taarifa tu ndugu mleta mada unatakiwa utambue kwamba Wajaluo ni wapinzani na hawakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na serikali mpaka mwaka 2018 baada ya Raila kujiapisha na mkoa wote wa Nyanza kugomea uchaguzi wa marudio 2017.

Hawakuruhusu vifyaa vya uchaguzi kuingia mkoani humo. Sasa hayo unayosema kuhusu ukosefu wa nyumba za nyasi kwa wajaluo ni suala la historia.

Nyumba za nyasi zikikuwepo sana tu sema kwasababu wajaluo ni watu wa misimamo mikali na hawajui kubembeleza waliamua liwalo na liwe toka enzi za Kenyatta alipomzingua aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais Jaramogi Oginga Odinga, baba yake Raila Amollo Odinga na Oburu Odinga. Wanasema (Jaluo oksechi) mjaluo habembelezi au Jaluo Jeuri.

Sasa kutokana tifu ilokuwepo kati ka Kenyatta na Oginga Odinga, mkoa wote wa Nyanza ulitengwa kimaendeleo sana. Wao kwa jeuri wakasema hamna shida, wakaamua kuwekeza kwenye elimu. Walisomesha watoto kama hawana akili nzuri ndo maana wajaluo wana jeuri sana, kuna kipindi bungeni wakati bado kulikuwa na uhasama kati ya Raila na Uhuru, walikuwa wanasema chama cha jubilee kina mtaji wa watu wengi ila ODM kina mtaji wa akili wakimaanisha wasomi.

Sasa baada ya watu kupata elimu, ikabidi ajira zipatikane, wajaluo wakaamua kuondoa Nyumba za nyasi. Wakaja na kitu kinaitwa semi-permanent, ukuta tope ila paa limepigwa bati. Siku hizi wanazipiga na plasta usipoangalia vizuri unaweza kudhani ni nyumba ya matofali kumbe semi-permanent.

Pili, ile barabara uliyoitumia kutoka Sirare mpaka sehemu inaitwa Kakrao kabla ya kuingia kwenye ukanda wa mashamba ya miwa Uriri, Awendo (kuna kiwanda cha sukari hapa kinaitwa South Nyanza Sugar Company -Sony) mpaka Rongo ilijengwa na serikali ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya makubaliano katika jumuiya ya Afrika madhara mimi. Kampuni iliyoinjenga inaitwa Kojifa, hii barabara inatokea Tarime na inapitiliza mpaka Kakrao kama nilivyokwisha kusema.

Kipande kinachotoka Kakrao mpaka Kisii kimejengwa juzi tu hata hakina miaka mitano. Hii ni kama matokeo ya serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa mwaka 2008 baada ya varangati la 2007. Raila akiwa waziri mkuu alihakikisha anajenga miundombinu Nyanza ndo maana ukiwa Kisumu, barabara ni kama za Dar, Raila ni engineer na alikuwa waziri wa ujenzi na barabara kipindi cha nyuma hivyo alihusika katika kupanga miundombinu ya barabara.

Pia sehemu ya maendeleo hayo uliyoyaona ni matokeo ya katiba mpya ambayo iliwapa serikali ya majimbo (County governments) kila county inajipangia na kutekeleza miradi yake ya maendeleo na mfumo ule umehakikisha kwamba kila mwaka bajeti ya serikali lazima itenge siyo chini ya asilimia 15 kwenda kwenye county, hii ni tofauti na makusanyo ya ndani ya county zenyewe hivyo hela inashuka mpaka chini.

Kuhusu wanawake, nakuachia.
 
Baada ya watu kupata elimu, ikabidi ajira zipatikane, wajaluo wakaamua kuondoa Nyumba za nyasi. Wakaja na kitu kinaitwa semi-permanent, ukuta tope ila paa limepigwa bati. Siku hizi wanazipiga na plasta usipoangalia vizuri unaweza kudhani ni nyumba ya matofali kumbe semi-permanent.

Pili, ile barabara uliyoitumia kutoka Sirare mpaka sehemu inaitwa Kakrao kabla ya kuingia kwenye ukanda wa mashamba ya miwa Uriri, Awendo (kuna kiwanda cha sukari hapa kinaitwa South Nyanza Sugar Company -Sony) mpaka Rongo ilijengwa na serikali ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya makubaliano katika jumuiya ya Afrika mashariki. Kampuni iliyoinjenga inaitwa Kojifa, hii barabara inatokea Tarime na inapitiliza mpaka Kakrao kama nilivyokwisha kusema.

Kipande kinachotoka Kakrao mpaka Kisii kimejengwa juzi tu hata hakina miaka mitano. Hii ni kama matokeo ya serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa mwaka 2008 baada ya varangati la 2007. Raila akiwa waziri mkuu alihakikisha anajenga miundombinu Nyanza ndo maana ukiwa Kisumu, barabara ni kama za Dar, Raila ni engineer na alikuwa waziri wa ujenzi na barabara kipindi cha nyuma hivyo alihusika katika kupanga miundombinu ya barabara.

Pia sehemu ya maendeleo hayo uliyoyaona ni matokeo ya katiba mpya ambayo iliwapa serikali ya majimbo (County governments) kila county inajipangia na kutekeleza miradi yake ya maendeleo na mfumo ule umehakikisha kwamba kila mwaka bajeti ya serikali lazima itenge siyo chini ya asilimia 15 kwenda kwenye county, hii ni tofauti na makusanyo ya ndani ya county zenyewe hivyo hela inashuka mpaka chini.

Kuhusu wanawake, nakuachia.
 
Said S Yande

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
766
1,000
Kwa taarifa tu ndugu mleta mada unatakiwa utambue kwamba Wajaluo ni wapinzani na hawakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na serikali mpaka mwaka 2018 baada ya Raila kujiapisha na mkoa wote wa Nyanza kugomea uchaguzi wa marudio 2017.

Hawakuruhusu vifyaa vya uchaguzi kuingia mkoani humo. Sasa hayo unayosema kuhusu ukosefu wa nyumba za nyasi kwa wajaluo ni suala la historia.

Nyumba za nyasi zikikuwepo sana tu sema kwasababu wajaluo ni watu wa misimamo mikali na hawajui kubembeleza waliamua liwalo na liwe toka enzi za Kenyatta alipomzingua aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais Jaramogi Oginga Odinga, baba yake Raila Amollo Odinga na Oburu Odinga. Wanasema (Jaluo oksechi) mjaluo habembelezi au Jaluo Jeuri.

Sasa kutokana tifu ilokuwepo kati ka Kenyatta na Oginga Odinga, mkoa wote wa Nyanza ulitengwa kimaendeleo sana. Wao kwa jeuri wakasema hamna shida, wakaamua kuwekeza kwenye elimu. Walisomesha watoto kama hawana akili nzuri ndo maana wajaluo wana jeuri sana, kuna kipindi bungeni wakati bado kulikuwa na uhasama kati ya Raila na Uhuru, walikuwa wanasema chama cha jubilee kina mtaji wa watu wengi ila ODM kina mtaji wa akili wakimaanisha wasomi.

Sasa baada ya watu kupata elimu, ikabidi ajira zipatikane, wajaluo wakaamua kuondoa Nyumba za nyasi. Wakaja na kitu kinaitwa semi-permanent, ukuta tope ila paa limepigwa bati. Siku hizi wanazipiga na plasta usipoangalia vizuri unaweza kudhani ni nyumba ya matofali kumbe semi-permanent.

Pili, ile barabara uliyoitumia kutoka Sirare mpaka sehemu inaitwa Kakrao kabla ya kuingia kwenye ukanda wa mashamba ya miwa Uriri, Awendo (kuna kiwanda cha sukari hapa kinaitwa South Nyanza Sugar Company -Sony) mpaka Rongo ilijengwa na serikali ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya makubaliano katika jumuiya ya Afrika madhara mimi. Kampuni iliyoinjenga inaitwa Kojifa, hii barabara inatokea Tarime na inapitiliza mpaka Kakrao kama nilivyokwisha kusema.

Kipande kinachotoka Kakrao mpaka Kisii kimejengwa juzi tu hata hakina miaka mitano. Hii ni kama matokeo ya serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa mwaka 2008 baada ya varangati la 2007. Raila akiwa waziri mkuu alihakikisha anajenga miundombinu Nyanza ndo maana ukiwa Kisumu, barabara ni kama za Dar, Raila ni engineer na alikuwa waziri wa ujenzi na barabara kipindi cha nyuma hivyo alihusika katika kupanga miundombinu ya barabara.

Pia sehemu ya maendeleo hayo uliyoyaona ni matokeo ya katiba mpya ambayo iliwapa serikali ya majimbo (County governments) kila county inajipangia na kutekeleza miradi yake ya maendeleo na mfumo ule umehakikisha kwamba kila mwaka bajeti ya serikali lazima itenge siyo chini ya asilimia 15 kwenda kwenye county, hii ni tofauti na makusanyo ya ndani ya county zenyewe hivyo hela inashuka mpaka chini.

Kuhusu wanawake, nakuachia.
Kuhusu wanawake kadanganya.
 
UMUGHAKA

Member
Sep 1, 2021
24
75

Ahsante sana mkuu DALA kwa ufafanuzi mzuri,hakika nimefurahi kujazia nyama maana huko ni pazuri mpaka nilitekewa!,Kuhusu wanawake kule mkuu ni habari nyingine,wenzetu wanafaidi sana
 
Aug 10, 2021
96
150
Mleta mada hii njoo umalizie
Ila adi apo uko sahihi ,,kwanza umesahau jambo moja kubwa Sana
"Tofauti ya TANZANIA na KENYA inaanzia ofisi za uhamiaji " sirari (Kenya) ofisi zao ziko vizuri sana,,yaan mimi mara ya kwanza naingia Kenya machozi yalinilenga
niliumia Sana,,wezentu wako juu,,county ya Isbania nimekaa miaka 2 nikiwa nasoma VETA Isbania (welding),,wanawake ni kweli wapo Kama ulivoeleza,,wanapenda kusuka nywele ndefu zenye rangi rangi wengi ni wasomi somi kidogo,,
 
Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
13,622

Kwahiyo mkuu hiyo county ya Migori hakuna mkoa wa bongo unafika uzuri wake tukiacha haya majiji?

Itabidi nijipange nianze kuzurura kidogo.
 
clinician

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
276
500
Wakuu naomba mnieleweshe,kutoka hapo tarime Tz kama unataka kwenda Kenya Nairobi bus una book wapi? Una book hapo hapo Tarime au unaingia Kenya kwanza? Na nauli kutoka mpakani mpaka Nairobi ni how much? Hiyo safari inatumia masaa mangapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom