Kwa taarifa tu ndugu mleta mada unatakiwa utambue kwamba Wajaluo ni wapinzani na hawakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na serikali mpaka mwaka 2018 baada ya Raila kujiapisha na mkoa wote wa Nyanza kugomea uchaguzi wa marudio 2017.
Hawakuruhusu vifyaa vya uchaguzi kuingia mkoani humo. Sasa hayo unayosema kuhusu ukosefu wa nyumba za nyasi kwa wajaluo ni suala la historia.
Nyumba za nyasi zikikuwepo sana tu sema kwasababu wajaluo ni watu wa misimamo mikali na hawajui kubembeleza waliamua liwalo na liwe toka enzi za Kenyatta alipomzingua aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais Jaramogi Oginga Odinga, baba yake Raila Amollo Odinga na Oburu Odinga. Wanasema (Jaluo oksechi) mjaluo habembelezi au Jaluo Jeuri.
Sasa kutokana tifu ilokuwepo kati ka Kenyatta na Oginga Odinga, mkoa wote wa Nyanza ulitengwa kimaendeleo sana. Wao kwa jeuri wakasema hamna shida, wakaamua kuwekeza kwenye elimu. Walisomesha watoto kama hawana akili nzuri ndo maana wajaluo wana jeuri sana, kuna kipindi bungeni wakati bado kulikuwa na uhasama kati ya Raila na Uhuru, walikuwa wanasema chama cha jubilee kina mtaji wa watu wengi ila ODM kina mtaji wa akili wakimaanisha wasomi.
Sasa baada ya watu kupata elimu, ikabidi ajira zipatikane, wajaluo wakaamua kuondoa Nyumba za nyasi. Wakaja na kitu kinaitwa semi-permanent, ukuta tope ila paa limepigwa bati. Siku hizi wanazipiga na plasta usipoangalia vizuri unaweza kudhani ni nyumba ya matofali kumbe semi-permanent.
Pili, ile barabara uliyoitumia kutoka Sirare mpaka sehemu inaitwa Kakrao kabla ya kuingia kwenye ukanda wa mashamba ya miwa Uriri, Awendo (kuna kiwanda cha sukari hapa kinaitwa South Nyanza Sugar Company -Sony) mpaka Rongo ilijengwa na serikali ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya makubaliano katika jumuiya ya Afrika madhara mimi. Kampuni iliyoinjenga inaitwa Kojifa, hii barabara inatokea Tarime na inapitiliza mpaka Kakrao kama nilivyokwisha kusema.
Kipande kinachotoka Kakrao mpaka Kisii kimejengwa juzi tu hata hakina miaka mitano. Hii ni kama matokeo ya serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa mwaka 2008 baada ya varangati la 2007. Raila akiwa waziri mkuu alihakikisha anajenga miundombinu Nyanza ndo maana ukiwa Kisumu, barabara ni kama za Dar, Raila ni engineer na alikuwa waziri wa ujenzi na barabara kipindi cha nyuma hivyo alihusika katika kupanga miundombinu ya barabara.
Pia sehemu ya maendeleo hayo uliyoyaona ni matokeo ya katiba mpya ambayo iliwapa serikali ya majimbo (County governments) kila county inajipangia na kutekeleza miradi yake ya maendeleo na mfumo ule umehakikisha kwamba kila mwaka bajeti ya serikali lazima itenge siyo chini ya asilimia 15 kwenda kwenye county, hii ni tofauti na makusanyo ya ndani ya county zenyewe hivyo hela inashuka mpaka chini.
Kuhusu wanawake, nakuachia.