Mshawa
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 787
- 325
Samahanini sana akina Mangi sikujua kama inakuwaga siri.Ila ndo hivyo tena nimesha mwaga mchele kwenye kuku wengi.
Samahani bila sale na ndoo ya mbegee!!? Wewe namna gani aisee makosa yanatozwa eti.
Samahanini sana akina Mangi sikujua kama inakuwaga siri.Ila ndo hivyo tena nimesha mwaga mchele kwenye kuku wengi.
Bora iseme wewe chasaka wakiongea wengine humu hawakawii kusema mwamba ngoma karibu sana marangu hakukupeleka kinuka mori mkuu.
nakuambia angeenda kinuka mori huyu angeandika kitabu cha historia..au angeenda kwenye mihoteli ya kitalii kama Kilimanjaro Mountain Resort au angempeleka maeneo ya kinapa ajionee mihoteli asingerud huyu...lol
kama hujui kitu nyamaza mkuu maana ulichoandika kinakufunga mwenyewe .ina maaana kama alikuwa rauya ya marangu alikwenda marangu mtoni kuona maporomoko ya kinukamori weweKuna Rauya mbili: Rauya ya Marangu na Rauya ya Mamba. Wewe ulikuwa Rauya ipi na yenye maporomoko ya maji kama siyo muongo kama yule waziri wa TANESCO?
shem subiri wakija huko watakusifia
wewe unatokea kijiji kipi??Mkuu hiyo ni sembeti nyingine au? mimi ninafahamu sembeti ya kupitia mahali wanaita barabara ya kilema au kwa Anaseli. Marangu mtoni ukielekea kushoto unaenda kilema, si ndio?
Habarini za saa hizi.Kuna jambo ambalo nimeona nishee na wanajamii kuhusu Marangu.Mimi mzaliwa wa Dar es salaam ingawa kwa kabila ni msukuma.Tangu nimezaliwa nilikuwa sijawahi kwenda mikoa ya kaskazini.Kuna mshkaji wangu mmoja tulikuwa tunasoma nae pale Mlimani ni Mchaga toka Marangu.Kijiji anachotoka kinaitwa Rauya yaani kama Jina langu.Mara kwa mara alikuwa akiniambia kuna kijiji kinaitwa Rauya na mara nyingi alikuwa akinitania kwa kuniita Mangi.Nilikuwa nachukia sana coz nilikuwa sifagilii sana kabila la wachaga.Ila siku zilivyoendelea kusonga nilimzoea na tukawa marafiki wakubwa haswa.
Sasa juzi kati mzimu wa sikuku za xmass na mwaka mpya alinialika niende Marangu nikakione hicho kijiji cha Rauya.Nilikubali bila hiyana.Mama yanguu.Nilipofika sikuamini kama ni kijijini.Kulaleki wachaga ni Nyoko.Hiyo mijumba iliyofunikwa katikati ya migomba ilinifanya nitoe macho kama mjusi aliyebanwa na lango kuu la magereza.Yaani ni masinagogi ya kifahari haswa.Mijumba ya thamani kubwa imezungukwa na migomba.Mi nilijua naenda kijijini nitakuta nyumba za mbavu za mbwa kumbe ni kinyume chake.Wazazi wake walinipokea kwa moyo mkunjufu na wa upendo.Nilikuwa nimepanga kukaa siku tatu lakini nikajikuta nakaa wiki na ushee.Mazingira ya kijani kibichi yalinivutia sana.Mito mikubwa yenye maporomoko ndo usiseme.Alinipeleka mahali panaitwa Marangu mtoni.Hapo kuna kila huduma zinazopatikana mjini.Pub na restaurant za maana kama vile niko samakisamaki Dar.
Kwa mara ya kwanza nilikunywa mbege(Nilikuwa naidharaugi sana)Ila nilipoionja nilijua ni kwanini wachaga wanaisifiaga sana.Mbuzi na ng'ombe zilikuwa zinachinjwa kama vile hakuna kesho.Watoto warembo wakichaga ndani ya magari ya kifahari ndo usiseme.Usafiri wa kila aina hadi tax za maana.Basi jamaa akanipeleka kwa mshikaji mmoja wa mwenge Dar na yeye ni mchaga wa Marangu ingawa ni kijiji kingine.Huwa anafanya kazi za kuchomelea.Nilipofika kwake kidogo nilie baada ya kushangaa sana.Huo mjumba alioujenga ni balaa.Kidogo niseme niko msasani Dar.Mimi nilikuwa namdharau anavyoangaika na mavyuma kumbe jamaa ana jumba la mamilioni huko kiliji.Du!Naweza nikaeleza mengi ila kwa kifupi hawa watu wako juu.Na nitarudi tena Marangu Rauya.
Tatizo wanajenga hayo majumba halafu hawakai ni mpaka siku ya xmas sasa ya kazi gani hayo..na umri wa juu wa mtanzania ni miaka 55 tuu...wanawajengea mapanya na mabuibui tuu..mie sifagilii hiko kitu banaa..maisha ni kule unakoishi sio !!sio Dar umepanga chumba unachomelea vyuma, huko marangu una sinagogi na hauishi what the f.u*&^&...
Kisusio, Next time ukifika maeneo ya Marangu Hotel nitafute nikuonjeshe Kiburu, Kitawa, Machalari, Shiro, Ng'ande, Mtori, Ndafu na Ngararimo.
sijuim kwann sion kitufe cha like
BTW karibu tena unywe kiburu, kitalolo, kisusio, kitawa, ng'ande., ngararimo, mtori, machalari, vibere, vikwa, viiye, nyany' et al
cc Arushaone, Asprin Smile, Lily Flower et al
Sisi Wachaga Hutunaga Maneno Mengi Sisi Ni Kazi Tu. Mapenz Tumewaachia Watu Wa pwani
Kwa maelezo yako wewe ni Mmarangu, naona umetak upazungumzie kijijini kwenu.
Sishangai sana kwa kuwa Wamarangu na misifa hawajambo.
Siku ingine uwaulize wakuoneshe pia kwa yule mzee aliyekuwa akiwalawiti mabinti zake kule Marangu
Hapo hata mimi palinichanganya kidogo.Mi nilijua ni karibukaribu.