Nitarudi tena Marangu

Nitarudi tena Marangu

Kuna ile waterfalls pale Marangu mtoni inaitwa Kinuka mwori,Du! ni balaa...

uliiioba eeeeh ni noma asee pale nlitimba siku moja nkaenjoy sana, yule dada wa pale juu kisanamu chake daaah kinukamori si mchezo
 
Last edited by a moderator:
Ambony tsa mpfiri meeku
.. Tirima Kidongk'o ndipo uende tena meeku... Utachokwa...
 
Habarini za saa hizi.Kuna jambo ambalo nimeona nishee na wanajamii kuhusu Marangu.Mimi mzaliwa wa Dar es salaam ingawa kwa kabila ni msukuma.Tangu nimezaliwa nilikuwa sijawahi kwenda mikoa ya kaskazini.Kuna mshkaji wangu mmoja tulikuwa tunasoma nae pale Mlimani ni Mchaga toka Marangu.Kijiji anachotoka kinaitwa Rauya yaani kama Jina langu.Mara kwa mara alikuwa akiniambia kuna kijiji kinaitwa Rauya na mara nyingi alikuwa akinitania kwa kuniita Mangi.Nilikuwa nachukia sana coz nilikuwa sifagilii sana kabila la wachaga.Ila siku zilivyoendelea kusonga nilimzoea na tukawa marafiki wakubwa haswa.

Sasa juzi kati mzimu wa sikuku za xmass na mwaka mpya alinialika niende Marangu nikakione hicho kijiji cha Rauya.Nilikubali bila hiyana.Mama yanguu.Nilipofika sikuamini kama ni kijijini.Kulaleki wachaga ni Nyoko.Hiyo mijumba iliyofunikwa katikati ya migomba ilinifanya nitoe macho kama mjusi aliyebanwa na lango kuu la magereza.Yaani ni masinagogi ya kifahari haswa.Mijumba ya thamani kubwa imezungukwa na migomba.Mi nilijua naenda kijijini nitakuta nyumba za mbavu za mbwa kumbe ni kinyume chake.Wazazi wake walinipokea kwa moyo mkunjufu na wa upendo.Nilikuwa nimepanga kukaa siku tatu lakini nikajikuta nakaa wiki na ushee.Mazingira ya kijani kibichi yalinivutia sana.Mito mikubwa yenye maporomoko ndo usiseme.Alinipeleka mahali panaitwa Marangu mtoni.Hapo kuna kila huduma zinazopatikana mjini.Pub na restaurant za maana kama vile niko samakisamaki Dar.

Kwa mara ya kwanza nilikunywa mbege(Nilikuwa naidharaugi sana)Ila nilipoionja nilijua ni kwanini wachaga wanaisifiaga sana.Mbuzi na ng'ombe zilikuwa zinachinjwa kama vile hakuna kesho.Watoto warembo wakichaga ndani ya magari ya kifahari ndo usiseme.Usafiri wa kila aina hadi tax za maana.Basi jamaa akanipeleka kwa mshikaji mmoja wa mwenge Dar na yeye ni mchaga wa Marangu ingawa ni kijiji kingine.Huwa anafanya kazi za kuchomelea.Nilipofika kwake kidogo nilie baada ya kushangaa sana.Huo mjumba alioujenga ni balaa.Kidogo niseme niko msasani Dar.Mimi nilikuwa namdharau anavyoangaika na mavyuma kumbe jamaa ana jumba la mamilioni huko kiliji.Du!Naweza nikaeleza mengi ila kwa kifupi hawa watu wako juu.Na nitarudi tena Marangu Rauya.
weka picha,acha maneno mingi.
 
Kumbe jf inawachaga wengi ila ni wakimya du kweli hawa jamaa ni noma
 
Tatizo wanajenga hayo majumba halafu hawakai ni mpaka siku ya xmas sasa ya kazi gani hayo..na umri wa juu wa mtanzania ni miaka 55 tuu...wanawajengea mapanya na mabuibui tuu..mie sifagilii hiko kitu banaa..maisha ni kule unakoishi sio !!sio Dar umepanga chumba unachomelea vyuma, huko marangu una sinagogi na hauishi what the f.u*&^&...
 
Hizi thread za kuwasifia hawa watu kuanzia mwishoni na mwanzoni mwa mwaka huu zimekuwa nyingi sana hapa.Anyway hongereni wachaga.
 
every good come from north, see the northern part of the world you will realize, and the issue sio kujenga nyumba na wewe kukaa hapo kumuka kwamba una wazazi wako hapo na pale ni kwenu, ndio maana baadhi ya watu hawapendo kwenda kwao kabisa
 
Hizi thread za kuwasifia hawa watu kuanzia mwishoni na mwanzoni mwa mwaka huu zimekuwa nyingi sana hapa.Anyway hongereni wachaga.
Ahsante sana, lakini usisahau za kutuponda ni zaidi ya mara kumi ya za kutusifia..... Maisha ndivyo yalivyo.
 
Huo ndio ukweli wa mambo. Uchagani ni mahali pa kwenda kutalii. Sijui kama ulibahatika kuzitembelea zile hoteli zetu kadhaa. Ila mfukoni baba uwe umejaa! Karibu tena uje na ndugu zako wengine kwani nyumba za kulala wageni (guest) zipo za kutosha.
 
ukiwa huko huwez jua kama uko kwenye moja ya vijiji vya Tanzania.
 
Sisi tunatafuta hela kwa maendeleo,nyie wengine endeleeni kupiga kelele.
 
machame ipo njia panda ya Arusha na lazime uende hadi moshi mjini na pale utaanza safari ya marangu utapita njia panda ya dar then unaenda kama HOLILI then kuna njia ya kwenda hadi marangu mtoni

Inabidi tukuelewe hivyo hivyo tu. Kutokea Moshi ukielekea Arusha au Dar hizo ndio njia kuu (barabara kuu). Ukifika pale machine tools kuna tawi la barabara ndogo kuelekea Machame, pale pataitwa njia panda ya Machame. Hivyo hivyo kwa njia panda ya Himo kuelekea Marangu. Pale siyo njia panda ya Dar ila ni njia panda ya Himo kwa sababu hilo ni tawi dogo linaloelekea Himo lililojiunga kwenye barabara kuu inayoelekea Dar. Mfano pale Mombo kuna njia panda ya Lushoto, pale Chalinze kuna njia panda ya Kuelekea mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha nk.
 
Hahahaha! Mentor naomba unipe taarifa eti nitumie jina gani kwa Asprin badala ya 'kaka'! Au niseme "msacha' tehe...!

Sijafurahia ulivyoniita "kaka". Unaweza niita jina zuri zaidi ujue.....

CC: Mentor, kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom