Nitapata wapi hati ya tabia Njema Police clearance Report

Nitapata wapi hati ya tabia Njema Police clearance Report

Habari jf
Naomba kuuliza Nina shida na police clearance certificate! Je nitapata wapi kwa gharama ipi na inachukua muda gani??

Makao makuu ya police ndio pale Central au msaada jamani
Wizara ya Mambo ya Ndani, Makao Makuu, Jeshi la Polisi Tanzania.

Jaribu kuomba bila rushwa. Ni haki yako.
 
Nenda mambo ya ndani na 2,590 kwenye simu, lipia kisha fanya fp, toka nje mpe jamaa 10... Baada ya mda unaondoka nayo vinginevyo seven days
 
Ubalozini,au baadhi ya Nchi wakitaka kukupa vibali vya kudumu vya kuishi au kufungishwa ndoa huko ughaibuni,Kufungua kampuni nje huko ni mambo mengi ili wakujue wanadili na mtu salama ipo toka kitambo hii wanatoa wizara mambo ya ndani...kitambo jamaa aliomba Stellenbosch Unviversty wakamwambia aende na hiyo kitu..
Shukran sana mkuu, nimekupata
 
Ukiitaka haraka, hasa kwa wilaya/mikoa iliyo mbali na Dar, unalipa kiasi kitakachomwezesha askari kwenda physically Dar kwenye kanzidata na kurudi. Hapo utaipata faster. Ila sijui kama hii ya kutuma mtu Dar ni utaratibu rasmi au wa msaada tu.

Ukingojea utaratibu wa kawaida iko likely kuchukua wiki kadhaa, maana zinangojeana, huko Dar hakuna wa kuzisukuma ziende faster na kumbuka Dar zipo toka kote Tz.
Dodoma,wizara ya mambo ya ndani,hawatoi?
 
Nenda Central police iliyo karibu nawe utapata utaratibu mzima hasa ofisi ya OCD.
Ukiwa na kabahasha ndo kabisaaa.... kila la kheri mkuu.
Kabasha ni kwa ajili tu ya kurahisisha mchakato.. Mengine yote yamesimamia ukucha
 
Kabasha ni kwa ajili tu ya kurahisisha mchakato.. Mengine yote yamesimamia ukucha
Bila bahasha lazima ujute... unaweza kuwa na mapungufu 6 katika maombi lakini akahakikisha kila siku anakurudisha na moja hadi urudi siku sita.... awaukize wanaosota RITA...

Unaweza ukaenda leo ukaambiwa kalete hiki ukirudi kesho unaambiwa bad9 kile.
 
Kama upo dar es salaam fika Wizara ya mambo ya ndani Posta Ghana Street ukiwa umevaa nadhifu,kuanzia kichwani, usivae viatu vya wazi mfano wa ndala usivae pensi, usivae nguo inayobana,usivae singlend,fika siku ya kazi,usivae nguo iliyochanwa chanwa.

Nb
Usisahau kubeba passport size hata 3, kitambulisho chako

Mengine utafahamishwa utakapofika
 
Habari jf
Naomba kuuliza Nina shida na police clearance certificate! Je nitapata wapi kwa gharama ipi na inachukua muda gani??

Makao makuu ya police ndio pale Central au msaada jamani
Nenda wizara ya mambo ya ndani hapo Ghana street na picha passport size 2 kopi ya kadi ya kitambulisho cha taifa,kura au leseni na pia kwenye simu usikose elfu3 malipo ni kama elfu 2.

Uvaaji ni nadhifu unatakiwa uvae, usivae suruali ya jeans,kaptula au gauni fupi, sketi.
Muda wa kuipata clearence certificate ni baada ya wiki mbili.


Vijana muishi kwa uaminifu kuepuka kuwekwa kwenye rekodi mbaya za mambo ya ndani.
 
Daah mnahamasisha rushwa kwa kitu ambacho wao ni kazi yao kufanya na wewe haki yako kupata...
Sio rushwa ni kusaidiana majukumu tu,
Imagine wewe unaitaka kwa ajili ya viza na mhudumu anakwambia utaipata baada ya wiki na wewe safari ni after four days, sasa minyana na hiyo senti uone matokeao
 
Sio rushwa ni kusaidiana majukumu tu,
Imagine wewe unaitaka kwa ajili ya viza na mhudumu anakwambia utaipata baada ya wiki na wewe safari ni after four days, sasa minyana na hiyo senti uone matokeao
Ni rushwa mkuu unaweza kupata haki yako bila kutoa rushwa ukizoea...
 
Ni rushwa mkuu unaweza kupata haki yako bila kutoa rushwa ukizoea...
Subutuuuu!!!! Labda kama
Utapata basi sio kwa wakati muafaka
Serikali ya mtaa tu ni mpaka utoe chochote vinginevyo utapewa barua ya utambulisho watakapotaka wao sio kwa muda wewe ulienda
 
Inalipiwa buku jero au buku 2 tu!

Kwa Dar nenda Mambo ya Ndani pale karibu na Exim Bank na ONAMO hotel...

Hiyo buku jero au buku 2 iwe kwa simu ukipewa Control number unalipia.

Hapo Mambo ya ndani hicho kitengo kiko kule nyuma ya Ofisi kwenye yale Magofu magofu.
Yes you're right,ni buku mbili nakumbuka waliniambia iwe kwenye simu na nikalipa kwa control number

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
We jifanye punguani kwakujifanya hujui nini maana ya kibaasha wakati we ni mtanzania halisi na miaka yote CCM inaongoza huo ukiwa utaratibu walioujenga miaka kwa miaka.
Actually We should get a rid of this monster!
Swadakta
 
Back
Top Bottom