Nitamwamini na kumuunga mkono Rais Samia atakapotatua suala la fao la kujitoa

Hata kuidai kila baada ya mwezi si ya kwako? Watunga sheria wenyewe wakimaliza tu miaka mitano wanachukua fao lao mbona hawaachi? Mtu analipwa mil 12 na mikopo hadi milioni 800 halafu yeye kajitungia sheria achukue fao lake kila mkataba wake ukiisha ila wavuja jasho wanaolipwa hela ya kula tu wamewatungia sheria wasichukue mafao yao mpaka wafikishe miaka 55.
Huyu jamaa ni bogaz kbs.
 
Habari!

Sasa ni awamu ya 6 kwa mujibu wa Rais mwenyewe na serikali yake. Rais Samia Suluhu nitakuunga mkono kama utaondoa dhuluma hii kwa vijana.

Kumnyima kijana asichukue fedha yake kwenye mfuko wa kijamii mara baada ya ajira yake kukoma ni dhulma isiyovumilika.

Hebu vuta picha kijana aliyeajiriwa kwenye mradi na mradi ukaisha baada ya miaka 4 anaambiwa asubiri umri wa kustaafu ndipo apewe chake.

Je, thamani ya fedha husika leo italingana na miaka ijayo?

Sometimes wengine hupewa nusususu. Mara 30%, mara % ngapi itamsaidiaje kuondokana na umaskini?

Vijana wanaogopa kuacha kazi kwa sheria hizi za kinyonyaji.

Kama hii ni njia bora ya kuboresha maisha ya Watanzania kwanini wabunge ambao wengi ni over 40 wasichukue marupurupu yao ya kustaafu watakapotimiza miaka 60?

Kama hili Ni gumu, kwanini msipitishe sheria itakayoruhusu wabunge walioshindwa kuingia bunge linalofuta tu ndio wachukue fedha zao?

Kama Rais hatasolve hili nitamwona hana upendo na uzalendo kwa vijana zaidi ya maigizo tu yakumjenga na kumuimarisha kisiasa.
Naunga mkono hoja
 
Ina maana kila baada ya ajira ya mkataba, utadai mafao yako? Leo miaka minne kampuni A... Then kampuni B miaka 6 n.k

Basi itakuwa ni mwendo wa kudai mafao kila baada ya mkataba kuisha!

Labda ungemwomba SSH aanzishe unemployment benefit ili wakati unatafuta ajira nyingine uwe na kadhaa za kukutosheleza kwa mwezi..
Kuna tatizo mtu akidai stahiki zake, aijailishi nitadai mara ngapi hiyo hela ni yake anatakiwa kupewa ni yake.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mama ukimaliza huko tunakuomba utupie jicho NSSF, kuna vijana walimaliza mikataba yao huko na wakarudi mitaani. Ukienda kudai mafao yako angalao upambane mtaani unapewa mafao yako 33% then hiyo nyingine hawakupi. Ni utaisotea mpaka ukate tamaa. Hiyo 33% kwanza kuipata ni mtihani. Tunakuomba mama!!
 
Back
Top Bottom