Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini ikiwa Taifa Stars itafuzu AFCON mwakani 2024

Symbiotic

Member
Oct 25, 2022
24
37
Jana tumeshuhudia Stars ikishinda tena kwa mbinde goli 1 kwa sufuri dhidi ya Niger, huku Algeria akiifunga Uganda 2-1. Msimamo hadi sasa ukionesha Algeria akiongoza kundi na akiwa tayari kashafuzu fainali hizo hapo mwakani.

Mbio zimebaki kwa Tanzania anaeshika nafasi ya 2 kwa kuwa na points 7 na hasi ya goli 1 huku nafasi ya 3 akishika Uganda akiwa na points 4 na hasi ya goli 3.

Kiuhalisi Stars na Uganda wote bado wako na nafasi kutegemeana na matokeo ya mechi zao za mwisho.

Huku Stars yy akitafuta sare tu dhidi ya Algeria bila kujali matokeo ya Waganda kule dhidi ya Niger au Stars akifungwa na Algeria basi aombe asifungwe goli nyingi wakat huo akimuombea Uganda matokeo ya sare.

Ugumu unakuja pale ambapo kiuhalisia ni ngumu Stars kupata matokeo away tena kwa Algeria hapa binafsi sina matuamini hata kidogo hata sara tu ni ngumu sana kwa aina ya mpira tunaocheza ukilinganisha na kiwango cha Waarabu.

Kwangu naona hii game Stars akipoteza na hesabu zitaharibika zadi pale tutakapochezea kichapo cha goli nyingi kuanzia labda 3 nk, au hata mbili tu halafu wakati huo Uganda akamfunga Niger.

Nitakuwa wa mwisho kuamini ikiwa Stars itafuzu kwakuwa ninaamini tutafungwa na Waarabu na si chini ya goli moja pekee na wakati huo nawapa Waganda nafasi ya kumfunga Niger.

Wenzetu Waganda anagalau hatua kama hizi huwa wanajua nini wanachokitaka na ni wazuri na wana uwezo wa kupata matokeo away kwa timu aina ya Niger wanajua nin wanakipambania, ila bado nahic sisi huwa tunacheza tu ila hatushindani.

Nawaona waganda wakiungana na Algeria. hatuna uwezo wa kuwafunga Algeria na kutoa nao sare kwao, hiyo nafasi ni finyu na ndogo kuliko ngamia kupenya kwa tundu la sindano, wale jamaa walishatupiga hadi goli 7 kule kwao. Waganda uwezo wa kumfunga Niger wanao.

Ndio utaifa ni muhimu lkakini huwezi kwepa uhalisia. Hata Ukinambia nibeti nitaondoa mahaba na utaifa pembeni, mkeka nitawapa Algeria na Uganda kushinda.
 
Nafasi ya Taifa stars kupitia ni kubwa sana, ushindi wetu na Niger ulikuwa ni bahati ila wana uwezo mkubwa kutushinda, sitegemei Uganda wakamfunga zaidi ya goli mbili sanasana itakuwa Uganda kufungwa, kutoa draw au Uganda kupata ushindi wa goli chache
 
Kumbe unajua mpira.

Wajinga ni wale wanaoishi kwa matumaini wakati facts za kisoka (ambazo baadhi umezitaja hapo juu) zinawadai..

Kila la kheri stars..ila apambane na hali yake vilivyo.

Sare au kufungwa magoli machache. Its easy, as pie.

FUNZO KUU KWETU: Tujifunze mpira, elimu haina mwisho. INAWEZEKANA.

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Nafasi ya Taifa stars kupitia ni kubwa sana, ushindi wetu na Niger ulikuwa ni bahati ila Wana uwezo mkubwa kutushinda, sitegemei Uganda wakamfunga zaidi ya goli mbili sanasana itakuwa Uganda kufungwa, kutoa draw au Uganda kupata ushindi wa goli chache
Assume Uganda anapata ushindi wa goli moja maana yake anakuwa na points 7 tunalingana na tofaut ya goli inabaki goli moja. Sasa je sisi tutapigwa ngapi na mwarabu kule kwao? Au unadhani mwarabu ana masihara atatuacha salama? Maana Uganda akishinda hata moja tu cc tukakandwa hata 2 tu tuko nje. hapo upo!
 
Jana tumeshuhudia Stars ikishinda tena kwa mbinde goli 1 kwa sufuri dhidi ya Niger, huku Algeria akiifunga Uganda 2-1 . Msimamo hadi sasa ukionesha Algeria akiongoza kundi na akiwa tayari kashafuzu fainali hizo hapo mwakani.
Mbio zimebaki kwa Tanzania anaeshika nafasi ya 2 kwa kuwa na points 7 na hasi ya goli 1 huku nafasi ya 3 akishika Uganda akiwa na points 4 na hasi ya goli 3.

Kiuhalisi Stars na Uganda wote bado wako na nafasi kutegemeana na matokeo ya mechi zao za mwisho.

Huku Stars yy akitafuta sare tu dhidi ya Algeria bila kujali matokeo ya Waganda kule dhidi ya Niger.
Au Stars akifungwa na Algeria basi aombe asifungwe goli nyingi wakat huo akimuombea Uganda matokeo ya Sare.
Ugumu unakuja pale ambapo kiuhalisia ni ngumu Stars kupata matokeo away tena kwa Algeria hapa binafsi sina matuamini hata kidogo hata sara tu ni ngumu sana kwa aina ya mpira tunaocheza ukilinganisha na kiwango cha waarabu. Kwangu naona hii game Stars akipoteza na hesabu zitaharibika zadi pale tutakapochezea kichapo cha goli nyingi kuanzia labda 3 n.k au hata 2 tu alafu wakati huo Uganda akamfunga Niger.

Ntakuwa wa mwisho kuamini ikiwa Stars itafuzu kwakuwa ninaamini Tutafungwa na waarabu na c chini ya goli moja pekee na wakati huo nawapa Waganda nafasi ya kumfunga Niger.
Wenzetu Waganda anagalau hatua kama izi huwa wanajua nin wanachokitaka na ni wazur na wana uwezo wa kupata matokeo away kwa timu aina ya Niger wanajua nin wanakipambania, ila cc bado nahic cc huwa tunacheza tu ila hatushindani.

Nawaona waganda wakiungana na Algeria. hatuna uwezo wa kuwafunga Algeria na kutoa nao sare kwao, iyo nafasi ni finyu na ndogo kuliko ngamia kupenya kwa tundu la sindano, wale jamaa walishatupiga hadi goli 7 kule kwao.
waganda uwezo wa kunfunga Niger wanao.

Ndio U-Taifa ni muhimu lkn huwez kwepa uhalisia. Hata Ukinambia ni bet ntaondoa mahaba na U-Taifa pembeni mkeka ntawapa Algeria na Uganda kushinda.
Algeria watachezesha wachezaji wa kikosi Cha pili ambao wanasaka namba kwa udi na uvumba kuingia first eleven ogopa sana hao watu wa kupewa nafas ya kuonyesha uwezo wao huwa wanakiwasha hatar Bora hata wale first eleven maana wangekuwa wanaogopa kuumizwa.
 
Algeria watachezesha wachezaji wa kikosi Cha pili ambao wanasaka namba kwa udi na uvumba kuingia first eleven ogopa sana hao watu wa kupewa nafas ya kuonyesha uwezo wao huwa wanakiwasha hatar Bora hata wale first eleven maana wangekuwa wanaogopa kuumizwa.
Algeria atatunza kikosi kwa sababu ipi

Kwa sababu vikosi huwa vinatunzwa kwa sababu maalum

Wenzetu wanapenda kutengeneza rekodi watupige 5 watengeneze rekodi zao
 
Algeria atatunza kikosi kwa sababu ipi

Kwa sababu vikosi huwa vinatunzwa kwa sababu maalum

Wenzetu wanapenda kutengeneza rekodi watupige 5 watengeneze rekodi zao
Jana tu hawajapuuza na walikuwa away lkn wakamkanda Uganda pale pale. sasa na ukizingatia Uganda walivyokuwa wanautaka ule mchezo lkn wapi sasa cc je na ictoshe tuko kwao. alafu hatuna historianzur kule kwao hadi 7 huwa tunapigwa
 
Back
Top Bottom