Nitakuchukia for the rest of my life

Nitakuchukia for the rest of my life

raia_mwema

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
479
Reaction score
314
Niliingia katika mahusiano na wewe mwanamke kipindi kile na graduate, nikakupenda kwa moyo wangu wote, pamoja na kuishi katika mikoa tofauti nikawa mwaminifu kwako sikuwahi kuchepuka hata kidogo, nilijitahidi kwa moyo wangu wote kwa kadiri kulingana na uwezo wangu kudumisha pendo langu, wakati mwingine niliwadanganya wazazi naenda kwenye interview (MUNGU anisamehe) wanaponipatia nauli na fedha ya kujikimu basi nakuja kukutembelea.

Hii ilibaki kuwa siri yangu baada ya miaka mitatu changamoto ya ajira ikaendelea, pasipo kujali upendo wangu kwako ukanipiga chini baada ya kupata wa kukuoa, miezi nane mbeleni ukafunga ndoa. Haukujali ahadi nyingi na nadhiri tulizoziweka mbele za MUNGU na pia mbele za wazazi.

Niliumia saaana siwezi kusahau, Dunia nzima ilinielemea, maisha yakawa machungu kama chloroquine... Lakn siku zikasogea. Ni mwaka wa nne huu Moyo umekufa ganzi, sijawahi kabisa kuwa na hisia za mapenzi teena, Huwa namwomba MUNGU anipe moyo wa kusamehe na kusahau ili moyo uwe na amani niweze kusonga mbele nashindwa kabisaa kusamehe na kusahau...

Nakuchukua sana na kamwe sitakusamehe we mwanamke kwa ulilonitendea
 
4711ca449c1f78a60a81cabe11dfc12c.jpg
 
Huyo mwanamke alikupa nini!??
Ana nini cha ziada paka akukoseshe Raha?¿

Unamuomba Mungu yupi huyo ambae wewe unataka akusamehe while wewe hutaki kusamehe wengine???

Ili Mungu akuinue lazima usamehe... (B. Bukukuu)

Kubali Ishatokea Na hauwezkurudisha muda nyuma, Move on.

Be gentlemen
 
Ukisema kamwe hautamsamehe tayari unajifunga mwenyewe

Msamehe ili upate amani na uweze kuendelea na mengine.

Utakapomwachilia utajikuta hisia zinafunguka kwa Mwanamke wa maisha yako...
Mungu pekee anaiwezeshe kusamehe na kusahau Valentina
 
Acha akili ndogo ww. Msamehe kwa ajili yako. Huwezi jua huko mbeleni angegeuka kuwa mateso kwako.
Duniani tunapita tu na usipomsamehe unajitesa mwenyew. Unakuja leta thread huku sa hizi mwenzako anakojozwa
 
Acha akili ndogo ww. Msamehe kwa ajili yako. Huwezi jua huko mbeleni angegeuka kuwa mateso kwako.
Duniani tunapita tu na usipomsamehe unajitesa mwenyew. Unakuja leta thread huku sa hizi mwenzako anakojozwa
umetumia maneno makalin aseeeeeeeeeee
 
Tafuta kwanza ajira acha ujinga, sasa ungeenda kulisha nini mtoto wa watu? Pata pesa uone kama hajaanza kukutafuta tena!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom