Nitakubeba Juu Juu

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,412
Kuna demu 1 nilikuwa naye chuo, juzi nimekutana naye akaniambia kuwa tarehe 7 mwezi huu ni Birthday yake. Akaniomba nimnunulie zawadi, nikamuuliza zawadi gani utataka? Akaniambia zawadi yoyote. Nikamuuliza tena je kama nitakununulia simu ya Blackberry, akaniambia kama nitamnunulia BB atanibeba juu juu.

Mpaka sasa hivi sijui huku kubebwa kukoje?? Atanibeba kwa kuninyanyua kama mtoto? Au kuna maana nyingine, Maana nimeogopa kumuuliza asije niona mshamba, Wana Jf naomba mnijuze..
 

Mpe BB ya mchina, hiyo original unayo taka kumpa niuzie mm kisha nikupe ya mchina.
Huwezi ukampa demu BB original bana
 
Nunua hiyo simu halafu ndio utajua utabebwaje?
 
Siku ya tukio usisahau kubeba dume mkuu,lolote laweza kutokea!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…