Tunatumia vigezo gani kuunda majimbo?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Kwa takwimu nilizonazo ni kuwa Tanzania ina majimbo 264 ambapo ni Wabunge 264 bila kujumuisha Wabunge wa Viti Maalumu na Wabunge wa kuteuliwa na Rais.

Katika majimbo hayo, jimbo lenye watu wengi ni Jimbo la Ukonga lililoko Dar, ambalo kwa mujibu wa Sensa ya 2022 lina watu 921,857 na jimbo lenye watu wachache ni Jimbo la Donge lililopo Kaskazini Unguja ambalo lina watu 19,173. Yaani jimbo la Ukonga linawatu mara 48 zaidi ya watu wa Donge.

Tukichukua majimbo ya Tanzania Bara pekee, jimbo lenye watu wachache ni Madaba ambalo lina watu 65,215. Jimbo la Madaba liko Ruvuma. Hata hivyo, Ukonga lina watu mara 14 zaidi ya watu wa Madaba.

Swali ni je, tunatumia vigezo gani kuunda majimbo? Je, ni idadi ya watu au ukubwa wa kijiografia? Kuna tija gani ya kuwa na jimbo ambalo idadi ya watu wake ni sawa na watu wa kata kwenye jimbo fulani. Mfano Kata ya Wazo iliyoko Dar in watu 153,013 ambao ni wengi kuliko idadi ya watu wa majimbo 91 nchini.

Je, hatuoni huu uni upotevu wa rasimali kwa kuzingatia kuwa, kila Mbunge huwa na gharama kadhaa ikiwemo mshahara na marupurupu kibao?

Nadhani tuwe na sheria ya kutuongoza kuwa Jimbo linatakiwa kuwa na watu wangapi badala ya kujiundia tu jimbo. Hivi karibuni kuna mtu mmoja alitamani Jimbo la Mbeya ligawanye ili kuwagawia Sugu na Tulia, yeye hakufikira gharama kwa nchi amefikiria jimbo ni zawadi kwa mtu, sad.

Hoja zangu ni hizo tu, mimi naenda zangu kulima pilipili, karibuni shamba.
 
Kwa takwimu nilizonazo ni kuwa Tanzania ina majimbo 264 ambapo ni wabunge 264 bila kujumuisha wabunge wa viti maalumu na wabunge wa kuteuliwa na rais

Katika majimbo hayo, jimbo lenye watu wengi ni jimbo la Ukonga lililoko Dar ambalo kwa mujibu wa sensa ya 2022 lina watu 921,857 na jimbo lenye watu wachache ni jimbo la Donge lililopo Kaskazini Unguja ambalo lina watu 19,173. Yaani jimbo la Ukonga linawatu mara 48 zaidi ya watu wa Donge.

Tukichukua majimbo ya Tanzania Bara pekee, jimbo lenye watu wachache ni Madaba ambalo lina watu 65,215. Jimbo la Madaba liko Ruvuma. Hata hivyo, Ukonga lina watu mara 14 zaidi ya watu wa Madaba.

Swali ni Je, tunatumia vigezo gani kuunda majimbo. Je ni idadi ya watu au Ukubwa wa kijiografia. Kuna tija gani ya kuwa na jimbo ambalo idadi ya watu wake ni sawa na watu wa kata kwenye jimbo fulani. Mfano Kata ya Wazo iliyoko Dar in watu 153,013 ambao ni wengi kuliko idadi ya watu wa majimbo 91 nchini.

Je hatuoni huu uni upotevu wa rasimali kwa kuzingatia kuwa, kila mbunge huwa na gharama kadhaa ikiwemo mshahara na marupurupu kibao?

Nadhani tuwe na sheria ya kutuongoza kuwa Jimbo linatakiwa kuwa na watu wangapi badala ya kujiundia tu jimbo. Hivi karibuni kuna mtu mmoja alitamani Jimbo la Mbeya ligawanye ili kuwagawia Sugu na Tulia, yeye hakufikira gharama kwa nchi amefikiria jimbo ni zawadi kwa mtu, sad.

Huja zangu ni hizo tu, mimi naenda zangu kulima pilipili, karibuni shamba.
Idadi ya watu ndio inatakiwa iwe kigezo cha kuanzisha au kupunguza majimbo ya uchaguzi na viti vya wabunge
 
Back
Top Bottom