Nitakavyomkumbuka JK

Ulitaka atumie fedha za nani? hivi ulikwenda NSSF kudai mafao yako ukaambiwa hakuna.

Acha kufikiri kwa kutumia kiuno. sheria ya mafao imeshasainiwa lakini huonekani kuwa unafahamu chochote. Deni la taifa limekua kwa zaidi ya mara tatu katika kipindi cha miaka mitano tu. Naomba uniambie fedha hizo zimepelekwa wapi? Kwanini pia hawataki ukaguzi ufanyike ktk matumizi ya deni la taifa? Unafikiri kimagamba magamba ndio maana huwa hupendi kuumiza kichwa.
 
Rais aliyejenga chuo kikuu kikubwa Afrika Mashariki na ya Kati, Hii ni college of education pekee, chuo kizima hakiingii kwenye picha moja:

udom-012-college-of-education-hostels23.jpg
Zomba mkapa aliondoka ameacha plan na misingi mikubwa ya kuanzishwa kwa UDOM na hata jengo la chimwaga alilitoa mkapa kama njia mojawapo ya ku stimulate ujenzi wa chuo hicho kwahiyo pongezi kubwa zinaenda CCM na serikali ya wakati wa mkapa...ndio waliofanya foundation ...ila na serikali na CCM hii wanatakiwa wapongezwe kdg kwa kusimamia kimekamilika kwa anagalau wanafunzi wanasoma....na ilibidi wasimamie maana wangekosa la kuongea
 
rais anayehudhuria mazishi mengi mno kuliko raisi yoyote duniani, lakini misiba ya maana inoyoigusa taifa hakuudhuria wala kutoa neno mfano msiba wa mwangosi
 
Kumbe katumia pesa za walalahoi wanazochanga ili ziwafae wakistaafu halafu mnataka asifiwe. Kwanini asisifiwe yule aliyeweka mikakati ili mifuko ya jamii ikasimama kama JK alivyoikuta? Si mnataka tuwe fare basi ni vema tuwasifie walioanzisha mifuko hiyo naye akakuta pesa ipo akaamuru ijenge UDOM. Then hii itakuwa ni multiplier's effect lakini kumpa sifa mtu hatutendei haki nafsi zetu. Kuwaona marais waliomtangulia hawakufanya kitu kwa sababu hawakujenga UDOM ni kujidanganya. Give a credit where it's due. Tusilazimishe hata yale ambayo hayapo. JK atasifiwa kwa mazuri na ninaomba yaandikwe vizuri but not at belittling his predessors ambao hata yeye uwaheshimu na tumeshushudia akijivunia mahali amabapo Mzee Mwinyi alimfikisha. Amejivunia Mkapa kumpa nafasi. That's how people who moderate analyse issues
 
Elimu
elimu_image.jpg

elimu_image.jpg



Serikali kwa kushirikiana na Taasisi, Wakala na Mamlaka za Elimu, Wadau wa Maendeleo, Asasi Zisizo za Kiserikali na Wananchi katika ngazi zote imeendelea kujenga shule, Vyuo na Vyuo Vikuu katika maeneo mbalimbali. Ujenzi huu umewezesha kuongezeka kwa nafasi za masomo.
1. Kuongezeka kwa fursa ya utoaji wa elimu ya awali kwa kuhakikisha kuwa kila shule ya msingi ina darasa la Elimu ya Awali

  • Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 kwa mwaka 2005 hadi 896, 146 mwaka 2010.(wav 445,867, was 450,279)
2. Kuongezeka kwa ubora wa Elimu

  • Uandikishaji wa Wanafunzi katika shule za msingi umeongezeka kutoka wanafunzi 7,541,208 mwaka 2005 na kufikia 8,441,553 mwaka 2010
  • Uwiano wa mwanafunzi katika darasa umeboreshwa kutoka 1:80 mwaka 2005 na kufikia 1:54 mwaka 2010
  • Uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi umeimarika kutoka 1:7 mwaka 2005 na kufikia 1:3 mwaka 2009.
  • Idadi ya walimu wa shule za Msingi imeongezeka kutoka 151,882 mwaka 2006 hadi 157,185 mwaka 2010.
  • Idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka 14,700 mwaka 2006 na kufikia 15,727 mwaka 2009.
  • Kuongezeka kwa uandikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum(walemavu) kutoka wanafunzi 18,982 mwaka 2005 hadiwanafunzi 27,422 mwaka 2009.
3. Idadi ya wanafunzi wanaoendelea na na elimu ya sekondari imeongezeka

  • Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka wanafunzi 493,636 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 999,070 mwaka 2009.
  • Kuongezeka kwa wanafunzi wanaogharamiwa na serikali kutoka katika familia zenye kipato duni na yatima , kutoka wanafunzi 16,345 na kufikia wanafunzi 58,843 mwaka 2009
4. Mafanikio ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari(MMES)

  • yamefanikisha kujengwa na kuongezeka kwa Shule za sekondari za serikali na zilizojengwa kwa nguvu za wananchi kutoka shule 1,745 ( 1,202 za serikali na shule 543 zisizo za serikali) mwaka 2005 hadi shule 4,102 ( 3,283 za Serikali na zisizo za Serikali ni 819) mwaka 2010.
  • Uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Sekondari umeongezeka kutoka wanafunzi 524,325 mwaka 2005 hadi wanafunzi 1,466,402 mwaka 2010.
  • Nyumba 4,087 za walimu zimejengwa kuanzia mwaka 2005 hadi 2009 kupitia MMES.
  • Serikali ya awamu ya nne imefanikiwa kujenga Shule za kata 3,131 katika kata 2,575 mwaka 2005-2010.
  • Vitabu nakala 35,6000 vya masomo ya hisabati na sayansi vimesambazwa katika shule 81 za sekondari katika halmashauri 31 ili kuongeza uelewa wa masomo hayo kwa wanafunzi.
  • Vitabu 266,032 vya Sayansi na vitabu 203,824 vya hisabati kutoka USAID vilisambazwa katika shule za sekondari 1,259
5. Kuongezeka na upanuzi wa Mafunzo ya walimu katika shule za msingi na sekondari ambapo vyuo 16 vimefanyiwa ukarabati

  • Vyuo vya ualimu vimeongezeka kutoka vyuo 32 mwaka 2005 na kufikia 34 mwaka 2009.
  • Idadi ya wanafunzi katika vyuo vya ualimu imeongezeka kutoka 14,00(2005) hadi kufikia wanafunzi 21,846 mwaka 2010.
  • Walimu waliohitimu stashahada wameongezeka kutoka 3,148 mwaka 2005 na kufikia 5,476 mwaka 2009.
  • Walimu waliohitimu Shahada wameongezeka kutoka walimu 2,843 mwaka 2005 na kufikia walimu 5,331 mwaka 2009.
  • Jumla ya wahitimu wote ni 5,985 mwaka 2005 walimu 10,807 mwaka 2009
  • Jumla ya walimu kwa sasa ni 19,000
6. Mafanikio ya elimu ya Juu ni pamoja na

  • kuongezeka kwa udahili katika vyuo vikuu ambapo udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka wanafunzi 40,993 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 111,078 mwaka 2010.
  • Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo vikuu 31, 2010.
  • Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kuna wanafunzi 17,282.
  • Kumekuwepo na Ongezeko la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka wanafunzi 42,729( sh. 62.5) mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 58,841 ( Sh. 140 bilioni) mwaka 2009.
  • Programu za vyuo vikuu zimepanuka na kuboreshwa ambapo vyuo vikuu vya Sokoine, Mzumbe na Dodoma vinatoa shahada ya Elimu.
7. Kuongezeka kwa upanuzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi

  • kuongezeka kwa nafasi za mafunzo kutoka wanafunzi 78,586 mwaka 2005, hadi kufikia wanafunzi 125,359 mwaka 2009.
  • Ujenzi wa vyuo 10 vya ufundi umekamilika katika mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro,Mtwara, Pwani, Dar es salaam, Manyara na Kagera(karagwe).
8. Kuongeza fursa ya upatikanaji wa Elimu ya Watu wazima

  • Walimu 940 na Maafisa Elimu watu Wazima487 wa Halmashauri zote nchini wamepatiwa mafunzo kuhusu uanzishwajio wan a uendeshaji wa vituo na vikundi vya MUKEJA
  • Moduli 2,280 za MUKEJA zilichapwa na kusambazwa
  • Wanafunzi 7,290 wa Mpango Elimu ya Msingi kwa Walioikosa( MEMKWA) walimaliza Elimu ya Msingi na kati yao wanafunzi 2,363 walichaguliwa kuendelea na Elimu ya Sekondari
pamoja_elimu.jpg
 
hiki cha kata, chuo kikuu cha kisiasa

kuongezeka kwa udahili katika vyuo vikuu ambapo udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka wanafunzi 40,993 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 111,078 mwaka 2010.


2012 Wangapi?
 
Nitamkumbuka kama mtu binafsi muungwana na mstaarabu,lakini mtawala dhaifu kabisa kupata tokea toka uhuru wa Tanganyika!
 
Ni raisi ambaye ametawala huku akiandamwa na misukosuko mingi kwa kukosa strategies to impliment.
 
Rais aliyepanda mbegu za udini na ukabila. mcheka hovyo, anaanguka anugka

1. Raisi mwanzilishi wa KUCHAKACHUA!
2. Raisi wa kujieleza iliaonewe uruma!
3. Raisi aliyekimywa wakati wa matatizo/ hasiye na jibu jibu juu ya mambo ya msingi/ hasiye na maamuzi magumu na
ya busara!
 
Rais aliye imarisha demokrasia ya kujieleza! hadi wengine mkapata nafasi ya kuweka utumbo humu JF! Fungukeni!
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom