Nitakavyomkumbuka JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitakavyomkumbuka JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Sep 17, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,873
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  1. Rais aliyeingia madarakani kwa ahadi lukuki na kuwapa matumaini makubwa Watanzania kuwa na maisha bora!
  2. Rais aliyeingia Ikulu kwa bwembwe kubwa na wafuasi wengi!
  3. Rais aliyeunda baraza kubwa la mawaziri kuliko wote waliomtangulia!
  4. Rais aliyeteuwa viongozi vijana wengi na hasa wanawake kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi!
  5. Rais aliyeanzisha mikoa na wilaya nyingi nchini bila kuzingatia uwezo wa kiuchumi na kiutawala wa serikali yake!
  6. Rais aliyeteuwa majaji wengi bila kuandaa mazingira mazuri ya utendaji wao na uwezo wa kifedha wa serikali yake kuwahudumia!
  7. Rais aliyeteuwa viongozi wengi wake kwa waume, wazee kwa vijana kwa kuzingatia ushwahiba badala ya uwezo na uzoefu wa kazi au taaluma husika!
  8. Rais aliyefanya safari nyingi za nje kuliko wote waliomtangulia na hata kuvunja rekodi kwa viongozi wa bara la Afrika!
  9. Rais aliyedidimiza uchumi kwa kiasi kikubwa kwa kukosa mipango sahihi!
  10. Rais aliyeshindwa kukemea maovu na waovu katika serikali yake kwa kuogopa lawama!

  ATHARI KWA TAIFA:

  1. Ukubwa wa serikali umekuwa mzigo mkubwa kulingana na uwezo wa kiuchumi wa Taifa.
  2. Serikali imeshindwa kupata fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo na hivyo kusababisha miradi mingi kusuasua.
  3. Mfumuko wa bei umekuwa mkubwa na hivyo kuathiri wananchi wengi wenye kipato cha kati na chini.
  4. Wananchi wengi wamekata tamaa ya kuwa na maisha bora kama walivyoahidiwa.
  5. Taifa limekosa dira ya maendeleo kwa kutokuwa na hakika ya fedha.
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Rais aliyejenga chuo kikuu kikubwa Afrika Mashariki na ya Kati, Hii ni college of education pekee, chuo kizima hakiingii kwenye picha moja:

  [​IMG]
   
 3. N

  Nduguyangu Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ni rais aliyejenga shule za sekondari nyingi hadi katika miji ya Waisilamu kuliko maraisi wote waliyomtangulia.
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  hahaha! zomba nimekukubali, wewe sio mchezo aiseee.... Dah! Hicho chuo kwa kweli kizuri kwa macho, ndio kiko wapi na kitaegemea mambo yepi? Hapo raisi wangu anastahili pongezi kwa moyo mweupe kabisa!

  Asalam aleykum'
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Nasikia majengo yake yameanza kuwa na nyufa.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  ESTABLISHMENT:
  The University of Dodoma was formaly established in March 2007 following the signing of the charter by the president of United republic of Tanzania. The first academic programmes commenced in september 2007.

  The University has been designed on a campus college mode each of which will be semi autonomous. In its structure, six colleges are envisaged when the university if fully established by 2012/13. There are:  • College of Education
  • College fo Hummanities and Social Sciences
  • College of Informatics and Virtual Education
  • College of Natural Sciences and Mathematics
  • College of Health and Allied Sciences
  • College of Earth Sciences


  UDOM initially started with four schools, namely Education, Hummanities, Social Sciences and informatics. Currently three colleges and two schools are Operational. These are College of Education, Hummanities and Social Sciences, and College of Informatics and Virtual Education. In addition there are four chools on transition to Campus College. These are School of Natural Sciences and mathematics, on transition to College of Natural Sciences and Mathematics; School of Medicine and Nursing on transition to College of Health and Allied Sciences; and School of Mines and Petroleum to College of Earth Sciences.


  Source: The University of Dodoma
   
 7. kiplagati26

  kiplagati26 JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Rais mvumilivu kuliko wote duniani bali anamatatizo ya kibinadamu.
   
 8. awp

  awp JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  rais wa kutabasamu na kupiga picha
   
 9. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  NSSF wameisha lipwa pesa ya hicho chuo? aisee sikumbuki kumsikia Jk akikemea rushwa, wakati hili ni tatizo kubwa sana nchi mwetu...
   
 10. m

  mopaomokonzi JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You have got a point
   
 11. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa kutumia fedha za NSSF na PPF ambazo ni michango ya walalahoi wa nchi hii. Ameshindwa kurejesha fedha hizo kutokana na serikali yake kutokukusanya kodi. Matokeo yake amekimbilia kupeleka muswada bungeni kutaka wafanyakazi wote wanachama wa NSSF na PPF kufutiwa mafao ya kujitoa na kuweka masharti kuwa mafao kwasasa ni mpaka mfanyakazi (mwanacha) atakapostaafu. Aibu kubwa sana.
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni Rais pekee katika historia ya nchi yetu ambae msafara wake una AMBULANCE... mtu ambae hajui akiona msafara wake anaweza dhani wanasafirisha mgonjwa au maiti..
   
 13. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nitamkumbuka kama rais wetu aliyefanya mambo makubwa kuliko wote waliomtangulia
  1.Chuo kikuu dom hakuna mfano wake africa
  2.kupandisha mishahara ya wafanyakazi
  3.Sekondari kata zote nchini hakuna tena wasichana kuchukuliwa uhousgirl wote shule
  4.Zahanati kila kijiji hadi 2015 vijiji vyote vina zahanati
  6.uhuru wa vyombo vya habari
  7.Hajafanya biashara yeyote full time yuko kuhudumia wananchi
  8kapambana na mafisadi kwa uthubutu wa kipekee ambao wenzie uliwashinda(CAG,PCCB nk nk)
  9.Kaboresha jeshi la polisi maslahi yao na vitendea kazi(magari VX kwa rpc,hardtop za kumwaga,deffender,majengo ya kisasa askari wanamudu maisha sasa hadi wameeza kununua magari)
  10.Barabara kajenga nyiiingiii hadi 2015 zitakuwa zimekamilika
  11---- ni mengi mengi mazuri tatizo ushabiki wa siasa za kizamani zisizokuwa na tija yeyote ndo mnaandika msiyoyajua hamna hata shukurani nyie wala moyo wa kusifia mazuri mnasikitisha sana kumbukeni mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ulitaka atumie fedha za nani? hivi ulikwenda NSSF kudai mafao yako ukaambiwa hakuna.
   
 15. l

  luckman JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  chuo kimejengwa na nssf, ppf, nhif kwa pesa yetu sisi na si KJ ka mnavyodhani!
   
 16. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,873
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  Huwa ananuna akitaka kusambaratisha migomo ya wafanyakazi!
   
 17. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,216
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Raisi aliyevunja rekodi kwa kupiga picha na wasanii na warembo
   
 18. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Zomba ungepewa nusu ya resources alizopewa/alizozikuta Kikwete, je na wewe ungefanya kama yeye, au?
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Watu aina ya Zomba wanaamini maendeleo ni vitu na sio watu.

  Kuna tofuati gani na majengo ya zahanati yasiyo na dawa, vifaa wala wataalam? Au kuna tofauti gani na mejengo (dhaifu) ya vyumba vya madarasa yasiyo na walimu, nyenzo na vifaa vya kufundishia?

  Najua uko kazini, lakini bila shaka kazi yako ni suluba na dhalili sana.
   
 20. W

  Wimana JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Nilikugongea like ulipomkubali JK kwa kujenga UDOM lakini kwa hili naona ni zile jazba za watu wanaokwepa kujibu hoja na kuzusha vurugu.
   
Loading...