Nitakabidhi nchi kwa CCM: JK

Hivi Chadema mnawaza kushika hii nchi.Kweli maajabu yapo Chadema ganja sio kitu kizuri kabisa tena Kama chakula huli vizuri

Chadema wana matamanio ya nafsi kuchukua nchi jambo ambalo hawata weza na nina imani dr Magufuli ata shinda zaidi ya asilimia 70
 
Huyo ndiye JK,anavijua vita vya ndani zaidi dhidi ya wananchi wake mwenyewe kuliko wale wanaotuibia rasilimali na kumega ardhi yetu mipakani.
 
Hapo zamani za kale mnamo mwaka 1995 niliamini kua huyu mtanzania ana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko nchini.

Nililaani sana kitendo cha mwalimu kuliengua jina lake katika kinyang'anyiro cha kuelekea kushika hatamu.

Ni takribani miaka 18 imepita ndipo nimeanza kujua maana ya mwalimu kwa ule mwaka 1995.

Sasa nimeamini hapa duniani tuna chui waliojivika ngozi ya kondoo, pia, majuto ni mjukuu.

Kila ulichosema ni kwajili yangu pia
 
Kauli hii imetolewa na JK mjini Kigoma wakati wa sherehe za miaka 36 ya CCM....

"Nitahakikisha nina kabidhi nchi kwa mgombea wa CCM na si vinginevyo"!

KAMA RAIS WA NCHI, SALAAM HIZI MAANA YAKE NINI?!!
amesahau kwamba yeye anapanga Mungu anapangua
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Zilikuwa sherehe za CCM tulitaka Mwenyekiti wa chama aseme CCM haitashinda?

mara kadhaa nimesikia CHADEMA wanasema mwaka 2015 ni wao!!! CCM wajiandaye kuondoka IKULU.
 
RAIS J.M.KIKWETE kabidhi Nchi kwa kiongozi atakaye shinda kwa kura halali zitakazo kuwa zimetangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi. Vinginevyo ni ubatili mtupu!
 
Tunaposema Rais ajaye ni Dk SLAA tuna maana kwamba CCM itaondoka mwaka 2015. Hii haina tofauti na kauli ya Mwenyekiti wa CCM aliyosema Kigoma.
 
Sishangai kwa kauli za jk kwani mara nyingi huwa ccm wanaropoka pasipo kufikiria madhara ya kauli zao. Huwezi kutamka maneno kama hayo katika nchi ya kidemokrasia na kama si ya kidemokrasia ni bora watangaze wazi kwamba hakuna kuwa na vyama vingi kuliko kupoteza resource kuingia kwenye uchaguzi. Kama uchaguzi wa viongozi ni wa wananchi, akili timamu haiwezi kutamka maneno kama hayo ya jk kwasababu lazima utapata kigugumizi. Napingana na mmoja hapo juu anayesema upinzani haujawa tayari kushika nchi. Huyu naona kama ana fikra mgando. Kama dhana ingekuwa hivyo, mpaka sasa tungekuwa bado chini ya ukoloni kwa sababu 1961 wazungu wangesema watanganyika hawana uwezo wa kuongoza nchi. Lazima tuanzie mahali na mahali penyewe ndiyo hapa na ni sasa. Kuna viongozi wengi sana ambao hawako katika huo mfumo unaouita "viongozi" wa nchi ambao ni bora zaidi ya hao waliopo lakini hawapewi nafasi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hapo amesema kweli kabisa, upinzani bado sana Tanzania. CCM itatawala milele.

Kwa maneno hayo nadhani uelewa wako utakuwa mdogo sana hakuna katika historial ya dunia dola ambayo ilishawahi kutawala milele hata kama ilikuwa na ndoto hiyo lakuna haijawahi kutokea ni mungu tu ndiye atakaye tawala milele hata yeye anapata ushindani mkubwa kutoka kwa ibilisi katika dunia ya leo waliomwasi mungu ni wengi hata wazungu waliotuletea dini tunaambiwa wao leo hii hawaendi tena makanisani sasa utasemaje CCM itatawala milele hicho ni kitu ambacho hakiwezekani kamwe is just a matter of time siku moja CCM haitakuwepo tena madarakani dalili za maandamano na watu kupambana na vyombo vya usalama ni dalili tosha kuwa watu wamechoka na wanahitaji mabadiliko hata wewe huwezi kula ugali maisha yako yote siku moja utatamani kuonja kitu cha tofauti na ndivyo itakavyokuwa kwa CCM siku moja watu watatamani kuongozwa na mtu ambaye hatoki ndani ya CCM. Hata ndani ya CCM leo kunamgawanyiko kunawatu wameshachoshwa na mambo jinsi yanavyoenda hawatamani tena kuna hali iliyopo sasa hivi wanataka mabadiliko na amini amini na kwambambia baada ya kuandikwa tu kwa katiba mpya CCM will be no longer itakuwa imekufa hakuna jinsi ambavyo haitaangamia ikidumu sana basi ni miaka 10 au 20 ijayo lakini si zaidi ya hapo.
 
Bila shaka amesema hivyo kwa sababu anajua udhaifu wa watanzania walio wengi ambao wananunulika kirahisi kwa khanga na pilau ili kuipa kura CCM. Bado kuna kazi kubwa sana ya kubadilisha fikra na mtazamo wa watanzania, hasa vijijini, ili watambue kwamba umaskini wao unatokana na utawala dhalimu wa CCM, na si vinginevyo.
 
Sioni kasoro ya kauli ya Mwenyekiti wa CCM kipindi hiki cha siasa za ushindani ambapo kila chama kiko vitani huwezi kuwaambia askari/wafuasi kwamba adui atatushinda. Ni lugha ya kisiasa ........mwamba ngoma huvutia kwake.

Tabu iko wapi? Hakusema hata wakishinda chadema mwaka 2015 tutatumia dola kurudi madarakani.

Kauli mbalimbali zinazotolewa na Chadema, zinaonyesha kwamba na wao wanatabiri kwamba mwisho wa CCM ni mwaka 2015.
 
Hapo zamani za kale mnamo mwaka 1995 niliamini kua huyu mtanzania ana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko nchini.

Nililaani sana kitendo cha mwalimu kuliengua jina lake katika kinyang'anyiro cha kuelekea kushika hatamu.

Ni takribani miaka 18 imepita ndipo nimeanza kujua maana ya mwalimu kwa ule mwaka 1995.

Sasa nimeamini hapa duniani tuna chui waliojivika ngozi ya kondoo, pia, majuto ni mjukuu.

Mkuu nadhani uelewe kuwa kuna mabadiliko chanya na hasi hii ni tafsiri ya moja kwa moja toka kwenye maneno ya kiingereza positive and negative change. Mabadiliko yapo tena sana tu! lkn je ni chanya au hasi?????
 
The Hegue inanukia hapa , na hii ni moja ya kauli za ushahidi mahakamani huko pindi kikiwaka , Chadema kusanyeni video za ushahidi huu muhimu.
 
Nakumbuka siku aliyopitishwa na chama chake pale Dodoma mwaka 2005 kuwa mgombea nilikuwa kwenye nyumba moja ya rafiki yangu pale Makongo walifanya kazi naye foreign ,aliangua kilio huku akisindikizwa na mkewe akilia alisema na mnukuu,nchi yetu itaharibika sana hii miaka kumi tutajuta na kujuta
alisema Kikwete ni mvivu wa kufikiri na ni mroho sana na mwizi akanisimulia historia ya Kikwete kushiriki na baadhi ya wafanya biashara ya kuuza mafuta Ruanda baada ya Ruanda kupewa zuio la biashara na umoja wa mataifa
Alisema ni mfitini ana visasi na inda
karibu miaka saba baadaye nayashuhudia yule bwana alifariki mwaka jana angekuwa hai ningemshuhudia kwamba uliyosema ni kweli KIkwete ameingiza nchi kwenye dimbwi la damu tunayaona sasa
Ni kweli yeye atakabidhi nchi kwa CCM 2015 lakini sisi wananchi hatutakabidhi nchi kwa CCM kwani CCM ni janga la kitaifa na kama yeye na CCM wanadhani wapo juu ya wananchi basi ni hapo wakati utakapofika
Legacy aliyoiacha ni uchonganishi na upotevu wa mapatano ya kitaifa ametufikisha mahala tunaulizana nani kachinja nyama,swali ambalo tunajiuliza kwa mara ya kwanza
 
Na sisi tunahakikisha tunaindoa CCM madarakani na yeye na genge lake lazima waende jela.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom