Nitakabidhi nchi kwa CCM: JK

Nitakabidhi nchi kwa CCM: JK

Sijui kama ataweza kuisafisha CCM kwa mafuta gani kwani chama hicho hivi sasa ni cha watafuta maslahi tu. Chama kimekua soko la wanunuzi na wauza kura. Bahati mbaya watu wameliona hilo na hawataki.
 
Ni Maneno tu hata kwenye Kanga Moja yapo CDM tuko Imara.
 
Fikra mgando za kibabe. Asingekuwa na kichwa cha nazi, kauli kama hizo angewaachia akina Nape na Nchemba!!
 
Aibu itakuwa juu yake kwani watanganyika hawadanganyiki tena.
 
Na wawe tayari kuaanda mahali a kutuzikia maana watatuua wengi hatutakubali na wawe tayri kwenda the heague
.
.
Sogea tupite bwanaaaa..!! Ah nani aende huko the-Hague Court -Uholanzi, kufanyanini, ukiua KWANINI wewe UACHWE..!! ??. Mambo ya Kisavimbi sasa Basi, Mtu mmoja kusababisha mauaji ya halaiki halafu Baadae kwenda mpozapoza huko mafenini hii kitu haipo tena..
 
Sasa nyie mlifikiri ataisema CDM?..mbona hii ishu ndogo sana,kama Tz ni ya ukoo wa ccm,kama yy tu ndo mpiga kura may be
 
Kauli hii imetolewa na JK mjini Kigoma wakati wa sherehe za miaka 36 ya CCM....

"Nitahakikisha nina kabidhi nchi kwa mgombea wa CCM na si vinginevyo"!

KAMA RAIS WA NCHI, SALAAM HIZI MAANA YAKE NINI?!!
Kwa mawazo yangu nadhani kauli hii si ya kutilia maanani sana....ikizingatiwa sehemu aliyoitolea ni kwenye sherehe za ccm....mbele ya wanaccm......na yeye ni mwenyekiti wa ccm na ni mwana ccm pia......ulitegemea aseme ataikabidhi nchi kwa chausta au udp????...... Profesa akiwaambia wanaCUF kwamba 2015 lazima wachukue nchi ni kosa?....... au Dk akiwaambia wana CDM kuwa 2015 iwe isiwe lazima washike dola ni kosa?? ....wakati mwingine tuangalie kauli hizi kwa kutilia maanani wakati, sehemu na tukio lenyewe.....
 
nae ajiandae kukabidhiwa the Hague
tena atakabidhiwa kama Loura ghabgo.
kwa rais mwenye kujua dhana ya demokrasia ya kweli sio kauli ya kuongea
aige kauli ya Obama kwa watu wa Kenya.
CCM haina hati miliki na nchi, tumeshachoka kuibiwa na kudanganywa
kilichobaki ni kudai haki kwa lazima au kwa amani
watatupeleka huko tusikotaka.
 
Kasema ukweli kutoka moyoni mwake kazi kwenu kujipanga. Yeye na wenzake wanajipanga kuhakikisha CCM inakabidhiwa nchi 2015... na keshawaambia sasa sijui tufanye nini isiwe hivyo...

Chakufanya hapa mzee Mwanakijiji ni kujiandaa tu kisaikologia maana ........ Mtawala anayejaribu kutawala kwa mabavu anawafundisha wapinzani wake kumpinga kwa mabavu hayohayo. Ndo kusema Kikwete ameshatangaza kuwa 2015 anatumia nguvu ili pia kuwaandaa watanzania kila walipo kujiandaa kuipinga ccm kwa nguvu.
 
Kama kauli JK ameishatoa nyingi sana, hizi ni baadhi tu,,,,

''Wanafunzi wanapata mimba kwa ajili ya kiherehere chao''

''Nitaleta maisha bora kwa kila mtanzania''

''Tatizo la maji Daresalaam litakuwa historia''

''Ukitaka KULA lazime ULIWE kidogo''

Na nyingine nyingi, but all in all ukifuata kauli za FASTJET unaweza kuumiza kichwa chako maana huwa anaongea huku hajui anamaanisha nini.


Na kwa sasa ana msemo wake mmoja wa '"AKILI YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YA KWAKO"

HUYU JAMAA ANA MATATIZO YA AKILI NAHISI..
 
Hivi bwana swai una ndoto za chadema kushinda urais?? Kuwa mkweli huwezi kutegemea ukoo mmoja usambae nchi nzima na kupewa nchi. Kighoma wameshasema hawachezi tena midundiko ya wapinzani wanataka uongozi si kupewa viroba orijino kurushia watu mawe
Ndugu acha kuutumia vibaya Ubongo wako unajidhalilisha.
 
Kila ulichosema ni kwajili yangu pia

Nakumbuka pia tuliwahi kuambiwa na mwalimu mara baada ya vita vya kagera mwaka 1979 kua uchumi uliyumba na ilibidi tujifunge mikanda ili kuuimarisha, kweli watanzania tulijifunga si mikanda tu bali pia mikangaja.
Sikumbuki kama uchumi uliimarika ama la.

Zikapita awamu mbili hatimaye ikaja awamu ya kijana wetu mpendwa. Nikajua sasa nchi itawagawia wananchi wake maziwa na asali, zabibu na matufaha, minofu na maini.
Lakini kwa mshangao zaidi wananchi tumekabwa kabali hata kuhema hatuhemi, tunatweta kwa kufungishwa mikangaja tena kwa lazima kwa miaka takriban 7 sasa huku matunda ya nchi yakitumbuliwa na kijana wetu mpendwa akishirikiana na maswahiba zake wanaojiita watoto wa washika jembe hali ya kua hata mpini hawaujui.

Kilichobaki ni wananchi kujikomboa kifikra kisha kuchukua maamuzi magumu baadaye.
 
Hiyo kauli japo haipendezi na inazua wasiwasi, lakini ukizingatia mahali alipoisemea katika kujitapa kwamba CCM imefanya mengi ktk miaka 36 ya kuzaliwa kwake inaweza kuonekana ya kawaida tu
 
Kauli hii imetolewa na JK mjini Kigoma wakati wa sherehe za miaka 36 ya CCM....

"Nitahakikisha nina kabidhi nchi kwa mgombea wa CCM na si vinginevyo"!

KAMA RAIS WA NCHI, SALAAM HIZI MAANA YAKE NINI?!!

Kule USA Mr. OBAMA ameanzisha phrase mpya ukiachia ile ya ""YES WE CAN"" sasa kaja na ""COMMON SENSE"".
Common sense nadhani inamhusu sana huyu fastjet
 
ukiona hivyo ujue kashanusa maji ya pua na safari hii kauzu shimbo hayupo kutishia watu na mabomu
 
Kauli hii imetolewa na JK mjini Kigoma wakati wa sherehe za miaka 36 ya CCM....

"Nitahakikisha nina kabidhi nchi kwa mgombea wa CCM na si vinginevyo"!

KAMA RAIS WA NCHI, SALAAM HIZI MAANA YAKE NINI?!!

Si mpaka akabidhi!!?? hiyo ni dhana ya "Wape watu kile wanachotaka"; je mbele ya hadhara ya wana CCM ulitarajia Mwenyekiti wa CCM aseme tofauti hivyo?! itakuwa ajabu ya 10 duniani au labda awe amerukwa na akili.

Do not read too much in that statement; ni moja ya manjonjo ya ushereheshaji tu. ukweli unabaki pale pale.
 
Back
Top Bottom