Nitajuaje kama fridge guard imeharibika?

Nitajuaje kama fridge guard imeharibika?

Mynd177

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2022
Posts
3,167
Reaction score
5,655
Habari wakuu?
Poleni na majukumu na mihangaiko ya siku ya leo..
Niende kwenye mada.
Hapa maskani kuna fridge guard lakini muda mwingi inazima na kuonyesha taa nyekundu inaweza kuwaka na kuzima hata mara 10 kwa siku.

Mimi nilihisi labda ni power surges zinazoweza kuanzia TANESCO sasa nimemuuliza jamaa mmoja wa Tanesco akasema huenda fridge guard ndio mbovu.
Najua kuna wajuvi wa mambo hapa tafadhal naombeni kueleweshwa juu Ya hili.
Natanguliza shukran.
NB- Kuna muda inafanya kaz fresh.
 
Back
Top Bottom