Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,075
kwanini umesema aende chuo cha kiislam na sio cha kikristo??? una chuki na uislam wewe.
Nimeelekeza hivyo kwa sababu najua waislamu waliosoma vizuri Qur An, wengi wao ni waalimu katika vyuo vikuu, wanajua kuwa Ukristo na Uislam ni mitizamo ya Mungu yule yule kwa mila na desturi mbili tofauti. Lakini kimsingi imani ni katika Mungu yuleyule. Kumuelekeza kwenda kwenye Chuo cha Kikristo ni kuwa Crusador, na mimi si crusador. Yale atayoyapata kutoka kwa Muislam Msomi ndo hayo hayo atayoyapata kutoka kwa Msomi Mkristo, na hawa wawili hawagombani hata siku moja.
Karibu migogoro yote ya kidini kiini chake ni Upumbavu na Ujinga katika mambo ya Imani kwa Mola. Elimu inamweka mtu huru akaacha kutizama mambo kwa macho ya Uislamu ama Ukristo; badala yake atasiliza hoja kwa mtizamo wa maslahi makuu wa jamii kwa kuwa kwenye eneo la dini hapataonekana kuwa na tatizo. Na hili linakuwa kweli kwa wafuasi wa imani zote.