Nisikilizeni CHADEMA: Tatizo ni UKAWA, Hili ndilo chaguo langu la rais wa 5

Ni kweli kuwaachia CUF au NCCR lakini unadhani ni yupi atasimama watu wakavutika labda kama mnataka wabunge nao tupoteze fikirini mara mbili jamani Lipumba au Mbatia? Sijui!!
 
Chadema wanachekesha,hivi hawajui Lipumba anaivuruga Ukawa makusudi.?
Lipumba ameshahongwa pesa nyingi sana na JK aivuruge Ukawa. Lipumba sio mjinga ,anajua wazi kabisa hawezi kushinda uchaguzi, Anachofanya ni kuivuruga tu Ukawa
 
Hayo ni Mawazo Mazuri sana!; Ambayo ni Nccr na Nld tu, Wanaweza Kuyaafiki!; Cuf hawawezi kuyaafiki! Hivyo basi wapelekee hii Ajenda kwa walio Tayari, kwa ajili ya utekelezaji! Muda si rafiki tena kwa kusubiri!

Kamwe Lipumba hawezi kukubali kumwachia Slaa agombee Urais, Ameshakula hela za ccm.., subiri hiyo tarehe 25 watapiga tu dana dana ili kuwakatisha tamaa Ukawa,, Hakuna maamuzi yoyote watakayofanya. Teh trh teh,, Huu mvurugano umepangwa kiustadi sana na ccm.. Chadema wameingia kwenye mtego
 
Chadema wanachekesha,hivi hawajui Lipumba anaivuruga Ukawa makusudi.?
Lipumba ameshahongwa pesa nyingi sana na JK aivuruge Ukawa. Lipumba sio mjinga ,anajua wazi kabisa hawezi kushinda uchaguzi, Anachofanya ni kuivuruga tu Ukawa
Kumbe unalijua hilo kua chama chako nichakuhonga honga?
 
Mkuu unaweza kuwa sahihi kwa upande mmoja lakini kwa upande wa pili usiwe sahihi

Kama kwa namna yoyote ile cuf wanajaribu kwa makusudi mazima kuchelewesha na kuja kuukwamisha ukawa hapo mbeleni basi mada yako itakua na mantiki kubwa sana

Lakini kama mantiki yako ni ukubwa wa cdm na hawakuhitaji ukawa kufanikisha malengo yao hapo utakua unakosea sana

Kimahesabu ni majimbo mangapi ambayo ukijumlisha kura za wapinza na jumla ya kura alizoshinda mgombea wa ccm na ikawa kura za wapinzani ni nyingi ndio utajua hoja yako inakosa mantiki
Na ukichukua kura za Dr na Prof ukizijumlisha pamoja unaweza kuona ni jinsi gani ushirikiano huu unaweza kuwa na mntiki kubwa zaidi kuliko wakienda mmoja mmoja kivyake

Mnapotaka kushirikiana na mmoja akaanza kujiona yeye ni muhimu kuliko mwenzake basi hapo hakuna ushirikiano tena
 


Swali ni CDM watafanya nini?
 

Umeongea vyema sana, hongera.
 

Let me assure you CDM will break through this na kila jicho halitaamini...,

Some of us are determined and have set the course none shall make it different!
 
Mzee Mwanakijiji ktk vita MTU kma wwe huchelei kuitwa mhaini huu ni muda wa watu kuwa wamoja na sio kukatishana tamaa. Ukawa km ukawa wana nafas kubwa ya kushinda ni kuwasihi tu waache ubinafsi muungano huu ni muhim na mbowe pamoja na wanacdm wengine wameyajua haya sio kweli cdm in chama kinakubalika kanda zote LA hasha, Bali yapo maeneo ambayo yana kura nyingi kwa vyama vingine washirika na ccm ndio wanataka mfarakano wafanikiwe.

Ccm kwa sasa anatafuta turufu kubwa kwa hali na Mali na hana jinsi zaidi ya kutumia turufu ya udini (uislam na ukristo) hii unajua madhara yake hasa kwa taifa ambalo liko nusu kwa nusu na kura zote hzo zinahitajika. Na ukweli ni kwamba ukawa tu ndio wanaoushawishi wa kufanya hayo. Uwepo wa cuf na cdm ni alama kubwa na tosha ya kuua propaganda ya udini ambyo tukubali tukatae vyama hivi vinaonekana kusmamia pande flani za kidini kwa maono ya watu wengi sana. Hvo huna sababu ya kuona cdm anaweza kusmama peke , mathalan kama umemqoute lipumba kwa kuwaambia masheikh hakuna jinsi kwa 2010 kwa kumsaidia kikwete basi kama mtamuacha sa hv atatumia mbinu hyo hyo je huoni kama ana ushawishi kwa jamii Fulani.

Ukawa ni muhimu sasa kwa kuwa wanapambana na magufuli. Huyu ni kiongozi ambaye sio mwepesi mwepesi ana nguvu na anatajuka kwa wannachi sote ni mashahidi jamani na jua fika cdm katika moja ya ngome zake imara ni kanda ya ziwa na ujio was magufuli unaenda kugawa hyo kanda hakuna jinsi, na inafahamika kuwa kanda ya ziwa ina kura nyingi na hamasa za kikabila lzma zichukue nafas hizo ndio ghilba za ccm. Je? Huoni umuhimu wa kuungana utasaidia kucover kanda ya ziwa. Mathalani vyama washirika wana nguvu kanda ya kusini, magharibi,pwani na visiwani je kanda kama hzi kuwa moja huoni hata nguvu ya magufuli achukue kanda ya ziwa yote bado itakuwa imekula kwa ccm?

Ccm iko scattered kwa sasa i.e lowassa team na nguvu pekee ya upinzani ambao umejenga imani kwwenye katiba na sasa uchaguzi ndio sulihisho kuna wanachama wengi na wapigakura hawajielewi lkn nguvu ya umoja utasomba sana hizo undecided vote hasa zile kura 20m.

LA mwisho na la msingi Mzee mwanakijiji we haupo field unatanguliza sana hisia baadala ya ukweli kaka acha fununu fununu hawa akina mbowe c wapumbavu kuona hakuna njia mbadala zaidi ya umoja huuu na ukweli ni kwamba ccm ni mwamba mgumu bila ya haya kwa ghilba zao hakuendeki.

Cdm ni chama chenye wafuasi wengi na ushawishi kwa upinzani lkn bila ukawa nchi hii ni kitendawili, nawasihi wanaukawa wamentain umoja wao na kuomba wasiwe vipande vipande, mtafika ccm furaha yao ni kupasuka kwenu maana hata waliondani na wanataka kutoka wanaangalia nguvu yenu kwanza.
 
Last edited by a moderator:

Sijui kama wenzetu hata mnaangalia haya mambo kwa kina kinachostahili. Kwanza, hakuna mgombea wa "UKAWA" kwa sababu moja tu nimeeleza huko juu; UKAWA siyo chama cha siasa na hakina uwezo au hata haki ya kusimamisha mgombea yeyote hata wa kijiji. Mgombea wa Urais atatoka kwenye chama; na kwa vile Rais wa Tanzania ni mtendaji hawezi kutoka tu alimradi ametoka kwenye chama chochote. Rais lazima atoke kwenye chama ambacho kinaonekana kwa kiasi kikubwa kukubaliwa na wananchi wengi zaidi na ambacho sera zake zinakubaliwa na wananchi wengi (hili linaonekana kwenye uchaguzi). Sasa ukimchukua mgombea kutoka NLD au NCCR unafanya kwa msingi gani? Kwamba " kwa vile wenzetu wamesimamisha wagombea wengi basi na sisi tupewe Urais? Hivi ndivyo mnavyoona?

Lakini kubwa zaidi ambalo hamtaki hata kulipa nafasi ni ukweli kuwa Rais anatawala akisimamishwa na Chama cha Siasa. Sasa ukiwa na RAis ambaye chama chake kina wabunge watano tu; halafu chama kingine kina wabunge hamsingi au mia; huyo Rais atasimamiwa na chama gani? Atajadiliana na chama gani? Si unajikuta unamlazimisha kutokuwa huru kutekeleza sera. Vipi akiamua kutekeleza sera za chama chake kidogo utamwajibisha vipi?
 

Hivi hata kabla sijakujibu labda unisaidie jambo moja. Ni kwanini unafikiria UKAWA ni Muungano wa vyama vya upinzani Tanzania au inawakilisha "Umoja" wa vyama vya upinzani? Maana hayo mengine yote unayasema inaonekana yamejengwa katika msingi potofu - kwamba UKAWA ni umoja wa vyama vya upinzani.
 
Reactions: Ame

Unajua Lipumba alipata kura ngapi 2010 kulinganisha na kura alizopata 2005 na kwanini?
 

Kama unachukulia ukawa kwa muktadha unaotaka ww ni umoja wa katiba ya wananchi lkn kma tutachukua kwa dhamira nzr basi ukawa utakuwa kwa umoja wa vyama vya upinzani tanzania. Hoja ndio za kujadili na lzma tukubali ukweli kuwa mwenyekiti na associates wake hawakukosea kuingiza cdm ukawa wao wako kwenye field na wanajua zaidi nini umuhim wa huo unaoitwa umoja.
 
CUF wabinafsi sana, tamaa za wanachama wa CUF zinazoofisha UKAWA
Ata wakjitoa watz tutawaona hawakua na lengo la dhati ktk kuleta mabadiliko nchi....

Naiman wabunge wa CDM watazidi kuwa wengi zaid mwaka huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…