Mtanganyika
JF-Expert Member
- Jul 18, 2007
- 1,601
- 950
Kushughulikia mafisadi ni kazi ngumu - Pinda
2008-04-10 10:35:14
Na Joseph Mwendapole na John Ngunge, Dodoma
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, amesema kuwashughulikia mafisadi ni kazi ngumu inayohitaji umakini wa hali ya juu.
Aliyasema hayo mjini Dodoma jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali.
Bw. Pinda alikuwa akijibu swali aliloulizwa namna anavyowashughulikia waliohusika na wizi katika akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT.
Alitetea uamuzi wa serikali wa kuendelea kupokea fedha zinazorejeshwa na mafisadi hao bila kuwataja majina kuwa unamanufaa makubwa.
Aidha, alisema serikali inachotaka kwa sasa ni fedha na kwamba baada ya hapo ndipo itaangalia namna ya kuwashtaki waliohusika.
Alisema hata majina yao yatatangazwa baada ya shughuli ya kurejesha fedha hizo na uchunguzi kukamilika.
``Usipojipanga vizuri unaweza kukurupuka kuwashtaki na wakakushinda, hivyo utapoteza vyote, kesi umeshindwa na fedha hujapata, sasa serikali kwanza inaona cha muhimu ni kupata fedha zake, mambo mengine baadae,`` alisisitiza Bw. Pinda.
Alisisitiza kuwa kutaja majina ya waliochota fedha hizo ni kuvuruga uchunguzi unaoendelea.
Alisema hata yeye binafsi ana shauku ya kujua majina ya watu waliohusika katika sakata hilo lakini aliomba wananchi kuendelea kuvuta subira.
Bw. Pinda alisema atajitahidi kwenda na kasi aliyokuwa nayo Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa.
Alimsifu Bw. Lowassa kuwa alikuwa na kasi kubwa katika kusukuma mambo mbele na kwamba atajitahidi kufuata nyayo hizo.
``Na ndiyo maana nimemua kubaki na watu waliokuwa karibu na Bw. Lowassa ili wanisaidie kazi, wao wanajua mipango yote, watanisaidia kusonga mbele. Sitaki kuanza upya,`` alisema.
Pinda: Govt mulls measures against Richmond culprits
2008-04-10 10:05:15
By Lydia Shekighenda, Dodoma
Prime Minister Mizengo Pinda yesterday appealed for more patience as the government considered appropriate disciplinary measures to be taken against senior government officials implicated in the Richmond corruption scandal.
The officials include Attorney General Johson Mwanyika and Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) Director General Edward Hosea.
The premier, who was responding to calls for resignation of all those linked to the scam at a press conference here, said the government needed patience in dealing with ``the complicated and complex`` scandal.
``Resignation of these officials may not be a solution to corruption problems in state organs.``
Spika akasirika
Habari Zinazoshabihiana
• Wabunge waanza kufundishwa sheria 15.08.2006 [Soma]
• Zitto akana kulikejeli Bunge, Spika 01.01.2008 [Soma]
• Cheyo awasilisha ushahidi kwa Spika 14.07.2006 [Soma]
*Awajia juu wanaomzushia tuhuma kumchafua
*Asikitishwa bintiye kuandikiwa SMS chafu
*Rostam Aziz leo kuwekwa kitimoto bungeni
Na John Daniel, Dodoma
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Bw. Samwel Sitta, amewajia juu wanaomzushia tuhuma na kuwaita kuwa ni wanasiasa wa kiwango cha chini na majitaka huku akiwahakikishia wabunge kwamba ataendelea kuendesha Bunge kwa kasi na spidi inayotakiwa kwa maslahi ya Taifa bila kurudi nyuma.
Spika ambaye alionesha wazi kuhuzunishwa na tuhuma hizo, aliwapasha wabaya wake hao kuwa yuko tayari kujibu mashambulizi yoyote watakayoelekeza kwake, kwa kuwa ana uwezo wa kufanya hivyo.
Akizungumza muda mfupi baada ya muda wa maswali na majibu kumalizika bungeni jana, Bw. Sitta aliwataka watu hao kuacha mara moja kuwashambulia watoto wake na kuwajulisha rasmi kwamba aliyewakosea ni yeye na si Watoto wake, hivyo hakuna sababu ya kuwasumbua kwa maneno machafu kama walivyofanya kwa kumtumia ujumbe bintiye ambaye ameolewa.
"Waheshimiwa wabunge napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wote walionipa pole kwa yale yanayonipata, hata hivyo napenda kuwahakikishia kwamba nitaendelea kuimarisha Bunge hadi hatua inayotakiwa, hawa ni wanasiasa wa kiwango cha chini, ni wanasiasa wa majitaka," alisema Bw. Sitta na kuongeza:
"Ninachowaomba tafadhali wasishambulie Watoto wangu, binti yangu aliyeolewa anatumiwa meseji chafu, wanishambulie mimi, mimi ndiye nimewakosea si watoto wangu, ila niwahakikishie tu kwamba nina uwezo wa kuyakabili vizuri," alisema Bw. Sitta.
Conclusion:
Kila ninapojaribu kuperuzi news za Tanzania ni vioja juu ya vioja, scandal juu ya scandal. Sasa swali ni moja tuu, jee ni kwanini walio ughaibuni warudi kuishi Tanzania? Nadhani huu ni muda wa kuchukua kinyago aka mkoba aka gamba la nchi uliyokuwepo. Kwani haito kuuma sana sababu hiyo nchi huna root nayo. Kurudi home unaweza jiingiza kwenye maamuzi mabaya bure, mfano kuingi msituni ukawa muasi.