Mdogo wako kanifundishaHahahahah toka linii shemela wewe na haya mambo mbona sijawahi kukuona
Nimeishia hapa.Sehemu ya 04.
Monalisa ndiye msichana ambaye alionekana kumpenda zaidi Richard kuliko wasichana wengine pale chuoni, licha ya Richard kumkatalia ombi lake la kuwa wapenzi lakini bado hakutaka kukubali hilo, aliamini kwa vyovyote iwezekanavyo ni lazima mvulana huyo angefanikiwa kummiliki.
Kuna kipindi kichwani mwake yalimjia mawazo ya jinsi ambavyo alivyofanikiwa kumpata Richard kisha wakawa wanayafurahia mapenzi yao katika ufukwe wa bahari ya Hindi, alizidi kulifurahia hilo katika moyo wake maradufu na hata pale mawazo hayo yalipomtoka kichwani alionekana kukasirika mno, hakutaka kuamini kama kweli alikuwa akiwaza kwa wakati huo.
Moyo wa mapenzi ukazidi kumuendesha vilivyo, alikuwa amezama katika dimbwi la mapenzi ya Richard mvulana ambaye na yeye moyo wake ulikuwa umekufa umeoza kimapenzi na msichana mwingine chuoni hapo.
“Kwanini Richard anashindwa kunikubalia hivi inamaana sina uzuri wa kumvutia au?” aliuliza Monalisa huku akiwatizama wale mashoga zake watatu walipokuwa hostel.
“Sio kwamba humvutii isipokuwa Richard ameshatekwa na Evelyne,” alijibu msichana mmoja huku akionekana kuwa bize na simu yake.
“Sitaki kumsikia huyo mpumbavu tena nitamkomesha mwanaharamu yule,” alisema Monalisa huku akionekana kuchukia mno baada ya kulisikia jina la Evelyne likitajwa na rafiki yake huyo aliyejukana kwa jina la Penina.
“Shoga yangu mimi nimeshachoka kumfuatilia huyo Richard kwani hakuna wavulana wengine hapa chuo kwani yeye nani?” aliuliza Mary.
“Jamani Richard ni Handsome mimi mwenyewe bado sijaona mvulana anayemfikia kwa uzuri hapa chuoni,” alisema Adela msichana aliyeikamilisha hesabu yao pale ndani, walikuwa wanne.
“Lakini lazima nitampata tu,” alisema Monalisa huku akijiapiza kumpata kwa vyovyote iwezekanavyo.
“Utatumia njia gani?” aliuliza Mary huku akimtazama Monalisa.
“Nitajua tu lakini lazima nimpate, nitahakikisha Richard anakuwa mali yangu,” alisema Monalisa.
Hahahaha wife bhana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Nimecheka sana unachokunywa au kuvuta usiache
Ukiweka muendelezo wa hii love story, naomba unitag tafadhar.Sehemu ya 18.
“Mungu wangu sijui Monalisa akipokea atamuambia nini?” alijiuliza swali hili katika mawazo yake.
Hakufahamu ni nini alichokuwa amedhamiria kukifanya Monalisa, alibaki katika hali ya sintofahamu huku asijue nini alitakiwa kukifanya kwa wakati huo.
Wakati akiendelea kuwaza mambo yote hayo lilimjia wazo kichwani, lilikuwa ni wazo la kumtafuta Evelyne kwa njia yoyote ili aweze kuzungumza naye, alipokumbuka umbali uliyokuwepo kati ya Mikocheni na Kigamboni alighairi kuchukua maamuzi hayo.
Alikumbuka kuwa Evelyne alikuwa akijulikana na Mama yake na alikuwa akipenda kuwasiliana naye mara kwa mara, hakutaka siku hiyo iweze kupita bila ya kuzungumza naye. Alichoamua kukifanya ni kwenda kumuomba Mama yake simu kisha akampigia, simu ya Evelyne ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa. “Mbona hapokei simu ni nini kimemkuta?” alijiuliza Richard baada ya kumpigia simu Evelyne zaidi ya mara tatu bila kupokelewa.
Hakutaka kukata tamaa, aliendelea kupiga huku akitegemea kuna muda Evelyne angeweza kuipokea simu hiyo lakini tukio hilo halikuweza kutokea. ****
“Punguza wasiwasi Richard yuko salama.”
“Nitapunguzaje na wakati hapokei simu yangu.”
“Labda yupo mbali na simu yake.”
“Sio rahisi.”
“Sasa unahisi atakuwa wapi?”
“Embu ngoja nijaribu kumpigia tena,” alisema Evelyne kisha akaamua kuipiga simu ya Richard kwa mara nyingine tena, safari hii simu ilikuwa haipatikani, akahisi labda mtandao ulikuwa unasumbua hivyo akarudia kupiga tena huku akijaribu kuzunguka huku na kule mule chumbani lakini majibu yalikuwa ni yaleyale.
“Hapatikani,” alisema kwa sauti ya unyonge.
“Hapatikani?” aliuliza Happy kwa mshangao.
“Ndiyo,” alijibu Evelyne kisha akakaa chini, nguvu zilikuwa zimeanza kumuishia kwa wakati huo.
“Mbona alikuwa anapatikana lakini?” “Mimi sijui ni nini kilichomkuta Richard wangu jamani.”
“Embu ngoja nijaribu na mimi kumpigia,” alisema Happy kisha akaichukua simu yake halafu akampigia Richard, hakukuwa na jibu lingine alilojibiwa kwa wakati huo zaidi ya kuisikia sauti ya msichana ikimuambia “ Mtumiaji wa simu unayempigia kwa sasa hapatikani, tafadhili jaribu tena baadae.
*
*
Je, nini kitaendelea?
Usikose toleo lijalo.
Asanteh mamaa!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jinga wewe