Nisaidieni wapi nikasome IT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni wapi nikasome IT

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by GAZETI, Feb 26, 2011.

 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,534
  Likes Received: 1,021
  Trophy Points: 280
  Kabla ya yote kwanza naomba ufafanuzi juu ya vitu hivi kama vina utofauti. IT, ICT & Computer science. Baada ya hapo naomba kufahamu ni wapi hapa Tanzania naweza kupata elimu nzuri ya masomo hayo, Nakusudia elimu nzuri na si cheti kizuri. Tena hata kama haitambuliki na serikali hiyo sehemu lakini kama elimu yake ni nzuri kuliko vyuo vya serikali naomba nielekezwe. Nahitaji kusoma kozi ya mwaka mmoja mpaka mitatu.
   
 2. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,534
  Likes Received: 1,021
  Trophy Points: 280
  Napenda kuongezea Gharama ya Kozidi isizidi Milioni 3 kwa Mwaka.
   
 3. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Kuna chuo kimoja kinaitwa New Horizon ni private ila wapo nondo sana ukipiga diploma pale miaka 2
  ata alietoka UDOM akuambii kitu man.Hiki chou wapo Dar,Arusha wapo fresh nakama kuna aliesoma hiki
  chuo ataweza dhibitisha nisemacho.
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  IT means information technology, ICT means information and communication technology, kwaufafanuzi zaidi watakuja wenyewe kudadafua.
  kwa gharama uliyotaja waweza soma chuo chochote tz iwe ifm, cbe, udsm, udom nk, pia waweza soma bachela,shahada,stashahada na cheti depending on your qualifications.
  Swala la chuo gani bora minadhani ni juhudi ya mwanafunzi mwenyewe kujua umefuata nini chuoni ingawa pia lina umuhimu wake
   
 5. Dubo

  Dubo JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 322
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inategemea unataka kuwa nani au kufanya nini na hiyo elimu yako.

  IT, ICT na Sayansi ya kompyuta ni vitu tofauti vinavyofanana.

  IT ni mojawapo ya applied CS kama ilivyo IS na ni subset ya Computer Science, inahusu novice and advance users na practical aspects of CS. Inafundisha jinsi ya kutumia teknolojia za kompyuta

  ICT ni mjumuisho wa IT na Communication technologies, inahusu practical.

  Computer Science ni nadharia na vitendo inajumuisha nyanja nyingi mfano networking,computer mathematics, IT, IS, ICT,utafiti n.k, inafundisha jinsi hizi teknolojia zilivyotengenezwa na jinsi ya kutengeneza nyingine, inaandaa watu wawe walimu na wafanyakazi, ila ICT na IT zinaandaa watu kuwa wafanyakazi tu.
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  Acharya Polytechnic College.......hawa jamaa ni hatari.....wapo Arusha na makao makuu ni India......jaribu kuwacheck
   
 7. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,534
  Likes Received: 1,021
  Trophy Points: 280
  Ahsante Manuu
   
 8. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huh?????
   
 9. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mtaalam naomba nitofautiane kidogo na maelezo yako naona umechanganya mambo

  Sio kweli kuwa IS ni subset ya computer Science. Computer science na IT ndio subset za IS.

  IS( Information system) inaweza kuwa mannual au automated. Mfano dafatari la maudhurio ya wanafuzi shuleni ni mfano wa IS ya manual. Shule ikiamua ku atomatae ndio inatengenzwa database hapo ndio mambo ya computer science na IT yanaingia. Huwezi kuwa na database bila computer............

  So kifupi maelezo yako umechanganya mambo

  Kurudi kwa Mada
  IT= Information Techology= Simu, computer, fax, website ni nyenzo za za IT
  ICT- Information and Coomunication Technology
  COmputer scince. Mtu aliye soma computer scince lazima ajue japo kidogo deteial za kompyuta kiundani . inavyofanya kazi na vifaa vilivyomo ndani. Mtu aliyesoma IT sio lazima ajue sana detail za technics za hardwareya computer/server

  Huwezi kutenganisaha ICT na IT sababu dhana nzima ya IT ni kurahishisha upatikanaji wa habari na mawasiliano. Kwa hiyo IT na ICT ni kitu kilekile.

  Soma hapa Information technology - Wikipedia, the free encyclopedia
  Computer science - Wikipedia, the free encyclopedia

  Kuhusu chuo Kizuri kwa Tanzania sijui yote inategema na jitihada zako. Vyuo vingi vinafundisha nadharia tu au topic amabzo haziendani na wakati. Hata singapore au india amabapo kwa budget zako unaweza kupata chuo kizuri lakini yote itategema jitihada zako.

  Kabla ya kutafuta chuo na kushauri kwanza jua unataka nini hasa. kuna

  • Networking,
  • Database
  • Programming
  • Electronics
  • General IT management , MIS
  Pili unataka kusoma kwa ajili ya kutafuta kazi au unapenda kujua mambo tu. kwa ajili ya shughuli zako ?

  Badala ya kutafuta chuo uamuzi mzuri unaweza kuwa ku kujifunza Certification course kama CISCO, Microsoft na nyingine nyingi tu. But kabla ya kufanya kozi hizi inabidi atleast uwe umesoma education course za computer basics japo kwa mwaka.

  Chuo chochote utakachochagua basi usiache kutumia internet kujifunza

  Pata ladha ya lecture za vyuo ambzao ziko free online

  Introduction to computer Programming

  Introduction to Computer Programming | Stanford Computer Science Lecture

  Mfano hii lecture No 5 pale stanford university  Web engeenerring

  HTTP | Harvard Computer Science Lecture

  Hii ni lecture ya Pili imetolewa pale havard kuhusu mambo ya web
  PHP | Harvard Computer Science Lecture

  Kwa hiyo ukichanganya chuo + na material yaliyo online +juhudi zako basi utafanikiwa

  Asikudangye mtu kuwa aliyesoma IFm ni bora kulikowa UD au wa UD ni bora kuliko wa UDOM au wa New Horizon no bora kuliko wa UCC. Tofauti inakuja kwenye jitihada za mwanafunzi mwenyewe.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Dubo

  Dubo JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 322
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Nakubaliana na wewe hapo kwa blue, lakini bado nina wasiwasi na kama "Computer science ni subset of IS"
   
 11. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Hautaki cheti unataka elimu nzuri sio? Basi nenda library ujisomee,alafu ufanye unachotaka. Lakini kama unataka uwe makini,tafuta cheti kizuri,soma sana. Watu wanasemaga eti sitaki cheti kizuri,utaishia kujichanganya.
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Jamaa nawajua nshapiga book pale pako juu saaaana tuuuu!!! na ntarudi tena very soon pale
   
 13. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimefurahishwa na thread hii. ni nzuri pia itasaidia sana, kwa watu kama wanajf technology and science. so OMBI LANGU KWA MOD. NAOMBA MODI UIWEKE NA HII THREAD IWE PARMANENT kama zile za modem unlocking. ili watu waadd ujuzi, then mwisho wa siku watu kama akina mimi tunaosoma, tukimaliza tujue tunaanzaje kushungulikia ndoto zetu.
   
 14. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Check na St Joseph College of Engineering and Technology,Wanatoka Chennai INDIA,wako Kibamba Dar!
   
 15. D

  Davies_007 Member

  #15
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiki chuo cha New Horaizon ni kizuri sana ila Serikali hua akikubali vyeti vya kutoka chuo hiki, kwa sababu hiki chuo kinatoa Advance Diploma kwa miaka Miwili wakati Serikali inakubali Advance Diploma ya Miaka Mitatu, sasa kitu cha Ajabu ni kuwa Nacte Imesajili hiki chuo wakati kinafahamu fika Advance ya chuo hiki ni miaka 2???????????????????????????????????????
   
 16. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,534
  Likes Received: 1,021
  Trophy Points: 280
  Labda ulikuwa hujanielewa kuna mtu nilikutana naye kasoma chuo kinachoheshimika kafaulu vizuri lakini mambo mengi yanayohusiana na IT hayajui. Kiutendaji ni mbovu tena wale waliosoma vyuo vinavyoitwa vya vichochoroni wako juu kuliko yeye. Lengo ni kujiajiri kwani tayari nina fani nyingine tofauti na IT
   
 17. newtonfox

  newtonfox Senior Member

  #17
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 196
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
 18. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  :hand::usa2:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Freelancer

  Freelancer JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 2,650
  Likes Received: 1,165
  Trophy Points: 280
  Computer Science is not equal to programming. Programming is not equal to software engineering.
  Computer science or computing science (abbreviated CS) is the study of the theoretical foundations of information and computation and of practical techniques for their implementation and application in computer systems.[1][2] Computer scientists invent algorithmic processes that create, describe, and transform information and formulate suitable abstractions to model complex systems (Wikipedia).
  An information system (IS) - or application landscape[1] - is any combination of information technology and people's activities using that technology to support operations, management, and decision-making.[2] In a very broad sense, the term information system is frequently used to refer to the interaction between people, algorithmic processes, data and technology. In this sense, the term is used to refer not only to the information and communication technology (ICT) an organization uses, but also to the way in which people interact with this technology in support of business processes.[3] (Wikipedia)
   
 20. K

  Kazabuti Member

  #20
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama unataka elimu nzuri kasome DIT utaiva kitechnologia mkuu.
   
Loading...