Nisaidieni nina roho ya kukataliwa

Nisaidieni nina roho ya kukataliwa

Gawa K kwa sanaa, utaona mishipa ya uso inalegea utaanza kutabasamu na utaacha kununanuna mtt. mwanamke kutabasamu bidada!
 
Kwanini lakini uwe mkimya kiasi hicho kwa watu?? kuna matatizo mengine tunayatengeneza sisi binadamu kwa kutaka...!

hapo madam unaweza ukakuta unataka ukae mwenyewe tu 24hrs hata kuongea na watu japo stori za hapa na pale ukawa hutaki, unadhani hata kama ni mimi, ntakuchangamkia from nowhere kabisa???

kumbuka hata mbwa nae hatikisi mkia kwa mtu asiye mjua!!!! hivyo hivyo na binadam nae, hawezi kumchangamkia mtu mwenzie ambae hachangamkii wengine!! BADILIKA SISTER.. JARIBU KUWA KARIBU NA BINADAM WENZIO!!!!

UNAWEZA UKAPIGIWA MAOMBI MARA MIA, LAKINI BADO UKAWA NA TATIZO LILE LILE!!!! WANGAPI WAMEOMBEWA, LAKINI BADO WAKASHINDWA KUPONA?.. MATATIZO MENGINE YANASABABISHWA NA MWANADAMU MWENYEWE NATURALLY SIO SHETANI!....!!!!

mi nakwambia ukweli kabisa!! kimya kingi kina mshindo!!!!

ITAFIKIA KIPINDI MPAKA WATOTO WADOGO AMBAO TUNAWAITA NI MALAIKA, WATAKUWA WANALIA WAKIKUONA!!!!

changamka uchangamkiwe...!
 
Gawa K kwa sanaa, misuli ya uso itaanza kulegea utaanza kutabasamu na utaacha kununanuna. Mwanamke ucheshi dada vipiii?
 
Gawa K kwa sanaa, misuli ya uso itaanza kulegea utaanza kutabasamu na utaacha kununanuna. Mwanamke ucheshi dada vipiii?

Hebu fikiri kuwa wewe ndiye Mleta thread unayehitaji msaada/ ushauri kutoka kwa Wadau. Halafu unapewa ushauri kama huo ulioutoa; ungejisikiaje?

Jitahidi kuwa Muungwana, heshima hainunuliwi, na haikugharimu chochote ukikaa kimya.
 
Pole sana,ila kama ulivoshauriwa kusali na kufanya toba unaweza ukawa unamadhambi makubwa yanayokunyima wepesi katika moyo wako kama uchawi,kuua,wizi,kutoa mimba na vitendo vyote visivyo mpendeza Mungu, nenda katubu kama unashida ya hivi roho yako itakuwa nyepesi.
 
kuishi na mtu kama wewe ni tabu make muda wowote ukiamua unanuna zako hapo ni kupeana maswali kumkichwa huyu nimemkosea nini....pole acha gubu!!!
 
Mi nina ushauri tofauti kidogo. .. anza kunywa pombe
Najua utaupuuza but at the last utajaribu alafu utajilaumu kwa nini ulichelewa kuanza..
Tatizo lako ni la kibiolijia wala sio kiroho...
Inhibition
Alcohol inhibits the inhibition

Nilikuwa sina mpango wa kuandika kitu ila hii baiolojia imenifanya nicheke saaana.

Anyway Pombe mkuu itamungezea matatizo na kuwa addicted kwa mana ya kwmba kwa hali aliyonayo kila akitaka kufanya kitu itabid apige glass kadhaa ili ageini konfidensi.

Dada jiamini na kuwajali wengine. Lakini pia kataa hii hali mwenyewe kwanza hata kabla hujaenda kuombewa or kufanya chochote.

Bibilia inasema hivi "Tafteni kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemuona MUNGU asipokuwa nao"

Kwahiyo suala la kutafta kuishi kwa amani linaanza na wewe kwanza then MUNGU ataona juhudi zako na kukusaidia. Ongea na kila mtu na kutabasam. Pia bible inasema Jitahid kujionyesha kwamba umekubalika na MUNGU, so to everyone.

Mungu akusaidie dada mtoa mada.
 
Jifunze kucheka mda wote,maana ukikaa kimya wenzako wanajua umenuna...sawa!
 
Habari wanajamvi

Mimi ni mwanamke nina miaka 2, ni mpole, mkimya sio muongeaji sana.

Toka nikiwa o-level kila mtu ninayeishi naye lazima tununiane bila sababu ya msingi, nimeshawahi wauliza baadhi ya niliowahi kuishi nao kwa nini inatokea hivyo, wakadai mimi ndio chanzo cha kununa na wakati mimi najiona sina tatizo wao ndio wenye matatizo.

Nimekuwa nikijitahidi sana hii hali isitokee lakini bado inajirudia nifanyaje?

Maana huwa inanikosesha amani naweza maliza hata mwezi bila kuongea na mtu ninayeishi naye akijua mi ndo nimenuna na mimi kwenye mawazo yangu najua yeye ndo kaninunia.

Sasa hivi naishi na mke mwenzangu hatuongei hii wiki ya pili sasa kila mtu anafanya mambo kivyake.

Naombeni ushauri wenu tafadhali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom