Nisaidieni nina roho ya kukataliwa

Nisaidieni nina roho ya kukataliwa

Pole nyambogo inawezekana wewe ndio mwenye tatizo maana haiwezekani wote unaoishi nao wawe na tatizo moja, kama ni mtu wakununa na kuomba msamaha inakua ni issue kwako. Hata kama mtu kakukwaza mwambie "nimekusamehe" na usisubiri yeye aseme, kwavile unataka kuondoa tatizo usione tabu na wala hutapungua uzuri wako kwa kusema "sorry"
 
Last edited by a moderator:
mahisi nalielewa tatizo lako sana ,nimewahi kulipitia ,ni fellings za self rejection,yaani kuna hali fulani wewe kujikataa kabla ya hao unaohisi wanakukataa,tutafutane PM tuone tutasaidianaje,kwa kuanza jaribu kuwa mtu mwneye kujiamini na mwenye kujali wengine,uamini kama unakubalika na ujiamini hivyo na wengine watapata sababu ya kukuamini.

noted mrsleo!
 
habari wanajamvi! Mimi ni KE nina miaka 27, ni mpole, mkimya sio muongeaji sana. Toka nikiwa o-level kila mtu ninayeishi naye lazima tununiane bila sababu ya msingi, nimeshawahi wauliza baadhi ya niliowahi kuishi nao kwa nini inatokea hivyo, wakadai mimi ndio chanzo cha kununa na wakati mimi najiona sina tatizo wao ndio wenye matatizo. nimekuwa nikijitahidi sana hii hali isitokee lakini bado inajirudia nifanyaje? maana huwa inanikosesha amani naweza maliza hata mwezi bila kuongea na mtu ninayeishi naye akijua mi ndo nimenuna na mimi kwenye mawazo yangu najua yeye ndo kaninunia. Sasa hivi naishi na KE mwenzangu hatuongei hii wiki ya pili sasa kila mtu anafanya mambo kivyake..... naombeni ushauri wenu tafadhali.

bila shaka hujajitambua lakin ww unaweza kuwa chanzo cha matatizo hayo, haiwezekana watu wote wakuchukie ww tu...... Kuna haya: mbinafsi, dharau, kiburi na utakuwa unahali ya kujiona ww ni bora kuliko wengne kwahyo unataka wakuanze kukusalimia au hata ukikosea unataka ww ndio uombwe msamaha. Jaribu kujikosoa nafikir unautumia ukimya wako kudharau wenzio
 
Mapepo hayo dawa kuwa karibu na mungu tu
 
hivi makanisa ya Kiroho ni yepi na yasiyo ya kiroho ni yepi maana nimeona hapa huyu mleta mada anashauriwa akaombewe makanisa ya kiroho?
 
bila shaka hujajitambua lakin ww unaweza kuwa chanzo cha matatizo hayo, haiwezekana watu wote wakuchukie ww tu...... Kuna haya: mbinafsi, dharau, kiburi na utakuwa unahali ya kujiona ww ni bora kuliko wengne kwahyo unataka wakuanze kukusalimia au hata ukikosea unataka ww ndio uombwe msamaha. Jaribu kujikosoa nafikir unautumia ukimya wako kudharau wenzio
ushauri murwa kabisa .... sasa kumbuka nakudai usijisahulishe
 
Kwa kuwa umeshajibaini kuwa una ghubu suala ni kuacha ghubu. Umesema "...lkn mimi naona tatizo ni WAO..." sasa km leo umebaini kuwa wao ni wengi basi hilo ni tatizo laki.

Usipende kuwa juu, mshindi wa mahusiano ni yule anayeyanusuru yakaendelea na sio aliyeshinda ubishi wa nani kakosea

Mkuu ghubu maana yake mwongeaji sana sasa yeye mkimya halafu wewe unasema tena ana ghubu! Au mie neno ghubu nalielewa ndivyo sivyo!!
 
Mi nina ushauri tofauti kidogo. .. anza kunywa pombe
Najua utaupuuza but at the last utajaribu alafu utajilaumu kwa nini ulichelewa kuanza..
Tatizo lako ni la kibiolijia wala sio kiroho...
Inhibition
Alcohol inhibits the inhibition
 
kila binadamu ana mapungufu yake hongera kwa kujua wewe ndo tatizo ndo ufumbuzi huo wa hilo.. ...
onana na watu wa saikolojia.
mtegemee MUNGU zaid na ufanye maombi ya kuvunja hiyo roho ya kununa bila sababu
 
Mi nina ushauri tofauti kidogo. .. anza kunywa pombe
Najua utaupuuza but at the last utajaribu alafu utajilaumu kwa nini ulichelewa kuanza..
Tatizo lako ni la kibiolijia wala sio kiroho...
Inhibition
Alcohol inhibits the inhibition

huu nao ni ushauri chanya japo mgumu kueleweka
 
Mi mwenyewe nakuona wewe ndio mwenye matatizo badilikaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom