Nisaidieni nakaribia kuumbuka

Kuoa ni tofauti na kuwa na mahusiano, kipato changu sidhani kama kinakidhi kuoa wake wawili, pia wao hawawezi kushare mwanaume na siku wakijua upuuzi wangu sipati picha
Kama vipi tafuta fedha ukiwa na mkwanja wa kuwahudumia watakubali tu kuoa wote maana ukiwapiga kila mm0ja na IST halafu ukawapiga na Nyumba Vyumba viwili,sebule jiko ,public toilet kila mmoja na biashara ya kuku/X-pesa etc hawachomoi ,Narudia Tafuta MTONYO KWANZA.
 
Acha povu wewe na mangeli yako peleka huko , kama ulielewa uzi uloandikwa kwa kiswahili kwanin usijibu kwa kiswahili? Una uhakika gani kuwa huyu mtu mwenye uzi anajua kiingereza?????

We jamaa, achana na huyo nanga hapo juu......... hii ni hatua ambayo wanamme wengi tunapitia japo si njema kabsa.

Watu wapo kwenye ndoa lakini bado wanavdem nje kama kawaida sembuse wewe tena bachela kabsa .....japo si point ya kujifariji,.

Ukweli humuweka mtu huru, chagua mmoja umuoe huyo mwingine mweleze ukweli aendelee na maisha yake ila muombe msamaha wa dhati maake utakuwa umemkosea sana.

Kingine kama upo vizuri kiuchumi... muwekee kias cha fedha kwenye akaunti yake itamsaidia, hyo itamuonesha unamjali ila ndo maisha yalivo.

Usuhuda;

Nilikuwa na kesi kama yako...... nilichokifanya Tuma nilimwachia hela zote nilizoweka nae kwenye vicoba kwa miez kumi, zikawa zake ni zaid ya 1M, nikamwambia hzo chukua ztakusaidia katika maisha yako ukurasa huo mpya... binafsi nikawa na amani yeye pia... hivi juzi nikamtumia wimbo wa Ambwene Mwasongwe ' patana na mshtaki' asikilize... akanambia ana amani ya kutoshamoyoni maisha yanaendelea.

Saiv nipo na mwnamke mmoja, nlikotoka sirudi tena.... wakristo tunasema nipo kanani sitarudi tena misri.
 
Nimependa sana mchango na jinsi ulivyotizama tatizo langu, kwakweli unahekima za kubalance mambo maana wengi wameishia kunilaumu na kuniombea mabaya ili nizidi kupotea na kuwa eti sistahili kuwa na mwanamke mwaminifu kwakuwa Mimi sikuwa mwaminifu, yaani Wana assume Kama Mimi nimeshakuwa shetani siwezi kubadilika na kuwa muaminifu

Ushauri wako upo wazi kabisa wala sitii shaka tena nitaufuata Kisha nitakupa mrejesho Mungu akipenda
 
Muda wa kuendelea kusaka mtonyo bila kuwa na mke nitakuwa najidanganya halafu kwa kazi na hadhi niliyonayo inanilazimu nioe kwasasa na umri ndo huoooo unayoyomaa, wadada wa watu wanazeekea nyumbani na pia nikijifanya kuvunga manyemera wataniwahi mkuu nitakosa woteee
 
Duuu, kwa iyo yawezekana kila mmoja ameusoma huu uzi na wasiweze kutambua kwamba huu uzi ni wao! daaaa.....
Inawezekana kabisa Kama wewe una dada au nduguyo wakike ningeweka picha zao hapa saa hizi tungekuwa tunaongea mengine lakini kwakua hujawafahamu amani inazidi kutawala
 
Sex is overated hamna jipya hata utoke Leo juma, kesho Ali, omary, Peter mwisho wa siku enjoyment huwa kwa yule mwenye connection and bond. Imagine mfano machangu. Kuna kufanya upizi na kufanya ile connection ya ndani
Hii inamake sense nakubaliana na wewe % kwa suala la sex lakini kwangu Mimi kuwa na wapenzi wawili nimeenjoy kuwa na faraja wakati wote kwakuwa ninapokosa faraja kwa mmoja Basi naipata kwa mwingine na hii inanifanya nijiamini sana na kujiona Mimi kidume mwenye akili nyingi kifupi mapenz nimeweza kuyaendesha na hayajaniendesha hata chembe
 
Authority wewe ni baharia wa kike au wakiume mbona Kama zile kanuni za kibaharia umezinywa halafu umebobea. Hii noma sana kaaaah
 
huwa inatokea,

chagua anayekujali na kukuheshimu zaidi ya mwingine, ndio awe mke. halafu punguza mawasiliano na huyo mwingine na hatimaye kata kabisa mawasiliano naye, ikiwezekana hama kama uko mtaa jirani naye
Wote wananijali na kuniheshimu sana na wote wako very serious na wanajua wanachokifanya sio wanawake wa hovyo hovyo hata Mimi nawaheshimu sana ndomana nipo makini sana kucheza na akili zao
 
Oa Ki Awamu ,anza na m1 kisha baadae utaoa mwingine,wewe ndio unaona hawatakuelewa lakini ukiwaweka chini vizuri wanaelewa sana!!
 
Daaaah mkuuu uko kama mm nina wawili sielewiii naoa yupi naachaa yupiii ilaaa mm kuna mmoja naona familia yao sio kubwa kvle kwa hyo nimepgaa calculations za future nisije nikawa na unecessary extended family ya kusomesha watoto wa wakwe,
At least nimepata companion
 
Mwanamke wa kwanza kunishauri bila kunilaumu.

Asante sana ubarikiwee
 
Sasa hapa umemuandikia trump ama?
Mtoa mada anakwambia kwa lugha nyingine ww unamjibu kwa lugha tofauti.

Hoja nzuri lakini umejuaje kama mtoa mada ataielewa lugha yako?
Hisia zinaweza kumfanya mtu abadili lugha. Jamàa alikerwa zaidi na vitendo vyangu vibaya akaona atumie lugha ambayo ni rahisi kuelezea hisia zake za ndani.

Ndomana walevi wakishalewa wanaongea ngeli
 
Hisia zinaweza kumfanya mtu abadili lugha. Jamàa alikerwa zaidi na vitendo vyangu vibaya akaona atumie lugha ambayo ni rahisi kuelezea hisia zake za ndani.

Ndomana walevi wakishalewa wanaongea ngeli
Yupi umetoka nae mbali? Kwan ulianza kudate nao sku moja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…