Nisaidieni cha kufanya baada ya mkopo

dr.bleeder

Senior Member
Oct 16, 2015
197
128
Ndugu zangu,

Mimi ni mfanyakazi katika moja ya Manispaa ya jiji la Dar-es-salaam, nilikopa katika benki ya Backleys mwaka 2009. Kwa makubaliano ya marejesho yatakuwa yakikatwa kutoka kwenye mshahara wangu huko huko hazina.

Makato yaliendelea mpaka nikamaliza deni na salary slip inadhihirisha hivyo,lakini cha kushangaza wamenitumia ujumbe kuwa bado nadaiwa kwa kuwa nilikuwa nachelewesha marejesho ya deni na hivyo system yao ilikuwa inafanya penalty, kwa hiyo hilo ni deni la penalty.

Sasa mimi najiuliza hilo kweli ni Kosa langu? Ningewezaje kuhakikisha marejesho anakwenda, wakati fedha zinakatwa hukohuko Hazina kwenye mshahara? Kutatua tatizo hili nifanyeje maana wamenizuia hata siwezi kukopa benki nyingine.
 
Pole mkuu, inabidi uende kuonhea nao kwa kina ili wakudadavulie kwa kina maana hawachelewi kukuibia, inasikitisha mkuu mimi nilichukua mkopo kwa miaka2 mwezi wapili mwakani ulitakiwa uishe lakini naambia banki haijapokea fedha yoyoye
 
Ni vyema kuwa tunafanya tafiti za benki sahihi ya kuchukua mkopo kabla, Ili kuwa na taarifa yakinifu. ili kuepukamaatizo kama haya.
 
Back
Top Bottom