Nisaidie Nidai Fidia Serikali

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Nilikamatwa nikashitakiwa kwa tuhuma za kukutwa na nyala za serikali. Miaka minne ya kesi, mwaka 2008 mahakama ikatoa hukumu kuwa sikuwa na hatia, upande wa jamhuri haukutoa ushahidi wa kuishawishi mahakama kunitia hatiani.

Nataka kudai fidia. Nifanyeje? Naomba msaada.
 
mh pole sana mi sina msaada si fani yangu lakini naamini wanasheria watakupa msaada. pole sana
 
Pole sana! Unachotakiwa ni kufungua shauri la madai kwa malicious prosecution uliyofanyiwa na Serikali. Hivyo unatakiwa kutafuta wakili atakayekusaidia kufungua shauri hilo. unatakiwa ufungue shauri hilo ndani ya miaka mitatu toka hukumu ilipotolewa. kwa kifupi unapaswa kutoa notisi ya siku 90 kwa serikali kabla ya kufungua shauri hilo. notisi hiyo itaipa muda serikali kutafakari madai yako na kuamua kukulipa fidia au la.
 
Kama nimekupata vema, inaonekana ushahidi ulitolewa na upande wa mashitaka ila mwisho wa siku ikaonekana hautoshi kukutia hatiani. Hapa ndipo ugumu unapokuja. i kila mara unapopelekwa courtini upatikane na hatia. Pia si kila kesi mtuhumiwa anaposhindwa anakuwa na haki ya kufungua shauri la madai. Sheria ya jinai inaeleza kuwa kama kuna "reasonable suspicion" kuwa mtu ametenda kosa la jinai basi na apelekwe court. Kwa uelewa wangu, mara nyingi ni vigumu kuthibitisha malicious prosecution labda uoneshe kuwa kulikuwa na nia mbaya na mashitaka dhidi yako yalitungwa. Lakini kama kweli yalikuwepo mazingira ya kukuhusisha wewe na nyara hata kama ki-ukweli (in fact) huhusiki, basi Jamhuri ilikuwa sahihi kukushtaki. Kupatikana na hatia au la ni suala lingine. Vinginevyo court zetu zingejaa case za malicious prosecution kama mtu yeyote anayeshinda kesi ana haki ya moja kwa moja kushtaki katika tort.
 
Ahsante kwa ushauri wenu na elimu mliyonipa. Mubarikiwe na Mungu aliye hai
 
Back
Top Bottom