Nisaidie mwanangu, muulize mama yako, kwanini ananinyima unyumba?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,833
Ugomvi wa baba na mama umekuwa ukiongezeka siku hadi siku. Nipo kijijini kwa mapumziko ya likizo ya siku 28. Hali hii imekuwa ikinikera sana hivyo nikaona kwasababu mimi ni mtu mzima nikae chini na Mzee Wangu tuyaongee, kwani shida ni nini?

Basi, kwa kuwa Mzee Wangu ni mtu wa kupenda maji machungu, nikaenda mnadani, nikanunua mbuzi dume, beberu kubwa, nikalipeleka nyumbani, nikawahuma vijana wamchinje tumchome.

Nikatoka kidogo nikaenda mjini nikanunua vinywaji mbalimbali, pombe za aina kwa aina, soda na maji na vyakula.

Nikarudi kijiiini na mzigo wangu wa mapochopocho. Basi baada ya mlo mida ya saa moja moja nimekaa chobingo na baba, mtu mbili tu, pambano la kiutu uzima, tunapiga story huku tukijitafuna na kusonsomola huku yeye akigida maji yake machungu.

Ndipo nikamuuliza, baba inakuwaje mara kwa mara unagombana na mpenzi wako, mchumba wako, mke wako ambaye pia ni mama watoto wako? Kwanini hali hiyo imekuwepo?

Mzee akanijibu, asante sana mwanangu kwa swali lako zuri, naona kwa kweli umekuwa mtu mzima hadi kiwango cha kujua mambo yangu ya ndani, mimi na mke wangu. Basi nakutuma kamuulize mama yako, kwanini ananinyima unyumba?

Nikajikuta nimeishiwa nguvu, nikaanguka miguuni, nikaanza kulia huku nikiomba msamaha, baba nisamehe, baba unisamehe, nimekosa mimi. Nikalia sana hadi alipo niinua kutoka ardhini.

Dah, nikajifunza somo kubwa sana.
 
Kina bi mkubwa huwa wanawahi kukinahi hayo Mambo,ndio maana utakuta wamekimbila chumba Cha wajukuu
Wanawake wakati mwingine hutengeneza mazingira ya wazee kuchepuka. Leo ninaumwa kichwa, kesho nimechoka sana mwili wote unawaka moto, kesho kutwa tumbo linaniuma kama myu ameshika kitu, halafu anakivuta huku anakimbia kwa kukatakata kona, siku inayofuata niko kwenye siku zangu, hapo mzee tayari ana siku kumi hajaosha dodoki
 
Ungesikiliza na upande wa pili. Sio sahihi kumjudge mama, ukute ana sababu za msingi.
 
Tatizo lenu mkishapata huto tu degree twenu feki na tuhela twa mshahara mnaanza kujiona mko sawa na wazazi wenu. Shame on you
 
Wadau mimi sijawaelewa kabisa, sioni hapo shida iko wapi. Je kama mke wako anakunyima unyumba utafanyaje? Au ingekuwa unashuhudia mama yako anakula kipigo kutoka kwa baba yako utakaa kimya eti huwezi kuingilia ugomvi wa wazazi??? Mimi hapana.

Kama mimi nitatafuta wazee au viongozi wa dini kisha mimi najiweka pembeni na sio kulia na kuanguka chini. Kwanza baba amenieleza kama mwanaume mwenzie na ni jinsi gani anauona ugumu na dhambi ya kwenda kuchepuka.

Ilishanikuta kwa x wife wangu, nilikuwa nanyimwa, kijana nikajiongeza nikawa napiga viwanja vya ugenini. Naamini wachngaji na ma ustadhi mumo humu, je ni sawa kunyimwa? Je ni sawa kuchepuka?

Nawasilisha..
 
Hapana sio kwamba mama anapigwa wew ukae kimyaa unakataziaa hata wakitukanana mnawakatazia shida inakuja wew mama yako anakwambia matatizo ya baba yako na weq unakurupuka kwenda kumuattack baba yako..!! Au anakwambia mama yako unaenda direct kumhukumu baba yako.. na kuna mengine ukiambiwa unayamezeaaa mkuu sio kila jambo linakupasa uliingilie. Mfano mama yako anakwambia baba yako ana mchepuko so wew utaenda kumuuliza mzee???
 
Asante mkuu wa kimasihara nimekuelewa vizuri mchango wako.
 
Wadau mimi sijawaelewa kabisa, sioni hapo shida iko wapi. Je kama mke wako anakunyima unyumba utafanyaje? Au ingekuwa unashuhudia mama yako anakula kipigo kutoka kwa baba yako utakaa kimya eti huwezi kuingilia ugomvi wa wazazi??? Mimi hapana.

Kama mimi nitatafuta wazee au viongozi wa dini kisha mimi najiweka pembeni na sio kulia na kuanguka chini. Kwanza baba amenieleza kama mwanaume mwenzie na ni jinsi gani anauona ugumu na dhambi ya kwenda kuchepuka.

Ilishanikuta kwa x wife wangu, nilikuwa nanyimwa, kijana nikajiongeza nikawa napiga viwanja vya ugenini. Naamini wachngaji na ma ustadhi mumo humu, je ni sawa kunyimwa? Je ni sawa kuchepuka?

Nawasilisha..
Soma ukiwa umevaa viatu vya mleta mada, je huu mstari umeuelewa vizuri?
naona kwa kweli umekuwa mtu mzima hadi kiwango cha kujua mambo yangu ya ndani, mimi na mke wangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom