Nisadieni ndoa yangu inavunjika

Nisadieni ndoa yangu inavunjika

Hivi huwa Mnajua Jinsi Gani Wanawke wanaumia Sema Hawasemi tu... Mke Mmoja Kakushinda unataka Wa Pili
Hayo ya ndoa za mitala mie sijui chochote, ila hiyo mahali kiboko ndugu yangu, dressing table inakuaje sehemu ya mahali? Hizi mila za wapi?
Namuonea huruma mke mkubwa, mke kaweza kukaa na wewe kwa maisha ya dhiki leo umezifanala ya kufanya sasa afurahi aanze kuvaa vzr na kupendeza na kuongeza ka mradi na yeye asimamie sas wewe umeleta balaa jingine??
Ifike mahali wanaume tujitazame vzr na kufanya maamuzi yenye tija kwa ustawi wa familia zetu.
Hizi dini hizi!!!!!!! Sijui !,! Kwa hiyo mtu anafanya maamuzi kisa dini hata kama uwezo wa kuhudumia hana, kunawakatikunawakati inabidi dini zifanye yake na mapenzi na yajitegemee.
 
Habari zenu JF,

Ukweli mimi ni muislamu mwenye miaka 30 nimeoa mke mwaka 2007 na niko na watoto 2.

Shida toka naoa nilikuwa na maisha mabovu kiasi ila nilimuambia mke wangu siku zikinitembelea japo kwa uchache naoengeza mke wa 2 na kwa kua dini inaniruhusu.

Muda wote huo mke wangu hakuonyesha kutetereka na maneno yangu hadi ikawa ananiuliza vipi utafanya lini huo mpango wako na kuniambia nifanye ila nadhani alikuwa ananiambia kwa kua sikuwa na uwezo, Mungu mkubwa akanipa kiajira mwaka 2014 hali ikawa afadhali nikamuambia mke wangu nikimuona ataerizika namuoa hapa alionesha kutetereka maana alijua muda umekaribia masharti yakaja kama nikimuona basi mahari ya huyo nitakaemuoa na yeye nimpe hayo nikamjibu sawa.

Siku nilipompata nikadaiwa kitanda, godoro, kabati na dresing basi nikaanza kununua vya mke wangu taratibu yeye hakujua kua natimiza miadi nikaongeza kwake kwa TV na Friza na Cable ili nikiwa zamu kwa mke mdogo vimliwaze.

Baaada ya kufanya hayo kwa usiri nikaoa tarehe 22/4/2016 mama yangu baaada ya kujua kawa mkali matusi mtindo mmoja malalamiko na kusema kuwa sikumtendea haki kila nikimpoza na kunasihi basi kama moto niliomwagia petroli anasema kanivumilia katika ziki leo namlipa hili.

Mke wangu kwa kweli nampenda sana hadi najilaumu kuyaamini maneno yake hadi najisikia vibaya sana kwa maneno yake na kufikiria kumuacha mke wa pili ila nimuacheje na yeye hana kosa lolote mimi ndio nilimchagua na pia ni mtoto mdogo nimuweke mjane itakuwa sijamtendea haki na nitakuwa nimejitia aibu.

Naombeni msaada ili nizungumze na wote wanielewe na mke mkubwa atulie ingawaje toka nioe nimekua nampenda sana mke mkubwa kuliko mdogo.
Na wapeni yatima mali zao, wala msibadilishe mazuri kwa mabaya, wala msile mali yao pamoja na mali yenu, hakika hiyo ni dhulma kubwa.
Na kama mkiogopa kwamba hamuwezi kufanya uadilifu katika mayatima, basi oweni mnaowapenda katika wanawake, wawili wawili au watatu watatu au wanne wanne. Na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu basi (oeni) mmoja au waliomilikiwa na mikono yenu, hii ni karibu zaidi na kutofanya dhulma.
 
Ningefurahi sana huu uzi wangechangia wahusika wakuu wa ndoa ya wake wengi ili wengine tujifunze mambo ya upande wa pili kuliko kumlaumu mleta uzi moja kwa moja
 
We lazima utakua mswahili mnawaza k.... tu!!
Kuna mswahili alitaka kumuoa dada yangu nilichokifanya ni kumuwaisha mbele ya haki tu maana sikua na jinsi ya kumsaidia ndugu yangu

Utakuwa mganga wa kienyeji mkuu
 
Hizi ndio zama za kuwa na wake wengi kama mlikua hamfahamu.
Kwanza wanawake idadi yao imeshatuzidi sana kulinganisha na idadi ya wanaume duniani.
Wanawake ambao hawajaolewa idadi yao ni kubwa kuliko ambao wamekwisha olewa.
Wanaume wachache wakiwa kwenye ndoa za mke zaidi ya mmoja kiuaminifu basi matokeo yake yatakua haya yanayofuata,

1.talaka kupungua (cz kuchepuka kutapungua sana
2.maradhi yatapungua pamoja na waathirika kupungua.
3.ukoo (family)yako kuwa kubwa na kutopotea kirahisi duniani tofauti na wale wenye kupanga uzazi(watoto wawili).
4.furaha ya ndoa itakuepo na kesi za ndoa kupungua.
Mengine mnaweza kuongeza kwa wenye elimu nayo.

NB: yote yaliotajwa hapo juu ni kwa wale wenye nia ya kweli na uaminifu kuwa kwenye ndoa ya zaidi ya mke mmoja.
 
Kwa zama hizi ukweli usiopingika mwanamke kuachwa au kuishi bila ya ndoa ni pigo na aibu kwake hata kama ana uwezo wa kifedha mwanamke mwenzie ni mwanamme kuna idadi kubwa ya wanawake wameridhia hata kuolewa awe mke wa tatu kwaajili ya kukàa ndani sana bila kuletewa posa hata ya bahati mbaya,na idadi inavozidi kuongezeka ya wanawake na wale wengine kukata tamaa ya kuolewa na kuwa uchu umewazidi wengi hushindwa kuvumilia na kubidi kufanya zinaa na hao waume za watu na wake za watu kulalamika waume zao wanachepuka kwasababu kuwakatalia waume zao kumiliki wake zaidi ya mmoja.
 
wajinga mjini hawaishi kweli teba khaaaa!!!!!!!!, this is amazing
 
Ndio maana daima naomba mwanaume asifanikiwe sana kimaisha, maana kama zereu zinazidi kama hizi. Unasema unampenda sasa kitu gani kilizidi uongeze mwengine........
 
Habari zenu JF,

Ukweli mimi ni muislamu mwenye miaka 30 nimeoa mke mwaka 2007 na niko na watoto 2.

Shida toka naoa nilikuwa na maisha mabovu kiasi ila nilimuambia mke wangu siku zikinitembelea japo kwa uchache naoengeza mke wa 2 na kwa kua dini inaniruhusu.

Muda wote huo mke wangu hakuonyesha kutetereka na maneno yangu hadi ikawa ananiuliza vipi utafanya lini huo mpango wako na kuniambia nifanye ila nadhani alikuwa ananiambia kwa kua sikuwa na uwezo, Mungu mkubwa akanipa kiajira mwaka 2014 hali ikawa afadhali nikamuambia mke wangu nikimuona ataerizika namuoa hapa alionesha kutetereka maana alijua muda umekaribia masharti yakaja kama nikimuona basi mahari ya huyo nitakaemuoa na yeye nimpe hayo nikamjibu sawa.

Siku nilipompata nikadaiwa kitanda, godoro, kabati na dresing basi nikaanza kununua vya mke wangu taratibu yeye hakujua kua natimiza miadi nikaongeza kwake kwa TV na Friza na Cable ili nikiwa zamu kwa mke mdogo vimliwaze.

Baaada ya kufanya hayo kwa usiri nikaoa tarehe 22/4/2016 mama yangu baaada ya kujua kawa mkali matusi mtindo mmoja malalamiko na kusema kuwa sikumtendea haki kila nikimpoza na kunasihi basi kama moto niliomwagia petroli anasema kanivumilia katika ziki leo namlipa hili.

Mke wangu kwa kweli nampenda sana hadi najilaumu kuyaamini maneno yake hadi najisikia vibaya sana kwa maneno yake na kufikiria kumuacha mke wa pili ila nimuacheje na yeye hana kosa lolote mimi ndio nilimchagua na pia ni mtoto mdogo nimuweke mjane itakuwa sijamtendea haki na nitakuwa nimejitia aibu.

Naombeni msaada ili nizungumze na wote wanielewe na mke mkubwa atulie ingawaje toka nioe nimekua nampenda sana mke mkubwa kuliko mdogo.

Huna akili
 
Kwani hiyo sheria yenu ya uislamu ni lazima kuitekeleza,!? Utapata dhambi usipoitekeleza? Kama c lazima kwann mnang'ang'ana na mambo ambayo magumu kuyatendea haki kwa maisha ya leo? Mbona mnawaka tamaa na mambo ambayo yanaleta mgawanyiko wa mahusiano badala ya kujenga? Nyie waislamu wanawake mnawafanya kama wanyama wasio na utashi wa kujua jema na baya? We ni muongo hujampenda huyo wa kwanza, kama unampenda wa kwanza na wa pili humpendi kama umpendavyo wa kwanza, sasa huyo wa pili ni wa kazi gani? Ni shiiidah sana......
 
Kijana Fanya subra hkn ndoa rahisi hasa za wake wawili hata sisi tulianza huko huko wht I advise u uwe strong dhoruba itapita na atazoea na hapo ndio utafaidi maana ushindani utakuwa mkubwa utajihisi mfalme. Haya nayaongea kwa experience
 
Ndio maana daima naomba mwanaume asifanikiwe sana kimaisha, maana kama zereu zinazidi kama hizi. Unasema unampenda sasa kitu gani kilizidi uongeze mwengine........
Nimeanza tu kucheka, ila umesema kweli kuna wanawake wanaomba Mungu waume zao wasifanikiwe sana, au mwingine anaomba tu mumewe apate maradhi ili angalau akae tu home mke amuone mwee

Gelofriend Evelyn Salt unakumbuka ile #teamrohombaya#
 
Habari zenu JF,

Ukweli mimi ni muislamu mwenye miaka 30 nimeoa mke mwaka 2007 na niko na watoto 2.

Shida toka naoa nilikuwa na maisha mabovu kiasi ila nilimuambia mke wangu siku zikinitembelea japo kwa uchache naoengeza mke wa 2 na kwa kua dini inaniruhusu.

Muda wote huo mke wangu hakuonyesha kutetereka na maneno yangu hadi ikawa ananiuliza vipi utafanya lini huo mpango wako na kuniambia nifanye ila nadhani alikuwa ananiambia kwa kua sikuwa na uwezo, Mungu mkubwa akanipa kiajira mwaka 2014 hali ikawa afadhali nikamuambia mke wangu nikimuona ataerizika namuoa hapa alionesha kutetereka maana alijua muda umekaribia masharti yakaja kama nikimuona basi mahari ya huyo nitakaemuoa na yeye nimpe hayo nikamjibu sawa.

Siku nilipompata nikadaiwa kitanda, godoro, kabati na dresing basi nikaanza kununua vya mke wangu taratibu yeye hakujua kua natimiza miadi nikaongeza kwake kwa TV na Friza na Cable ili nikiwa zamu kwa mke mdogo vimliwaze.

Baaada ya kufanya hayo kwa usiri nikaoa tarehe 22/4/2016 mama yangu baaada ya kujua kawa mkali matusi mtindo mmoja malalamiko na kusema kuwa sikumtendea haki kila nikimpoza na kunasihi basi kama moto niliomwagia petroli anasema kanivumilia katika ziki leo namlipa hili.

Mke wangu kwa kweli nampenda sana hadi najilaumu kuyaamini maneno yake hadi najisikia vibaya sana kwa maneno yake na kufikiria kumuacha mke wa pili ila nimuacheje na yeye hana kosa lolote mimi ndio nilimchagua na pia ni mtoto mdogo nimuweke mjane itakuwa sijamtendea haki na nitakuwa nimejitia aibu.

Naombeni msaada ili nizungumze na wote wanielewe na mke mkubwa atulie ingawaje toka nioe nimekua nampenda sana mke mkubwa kuliko mdogo.
Muache tu huyo mdogo baki na mkubwa, unadhani atakosa mwanaume? Tupo kibao. Mi siaminigi kwenye kuacha mke wa kwanza. Ukimuacha kazi yako itakuwa kuoa na kuacha. Labda akuache yeye. Pima maisha mliyoishi huko nyuma, kama mliishi vizuri tu na bado anakupenda basi acha huyo mdogo, ataolewa tu. Halafu usirudie kuoa eti kwa sababu dini inaruhusu, mjinga mkubwa wewe. Wanawake wa siku hizi si wale wa zamani eti unawarundika tu kama mifugo ebo! Kwanza watakuua.
 
Ila sasa mi nina problem kama yako ila sasa mimi sijaoa huyo mdogo. Dini hairuhusu. Mi nawapenda wote kwa namna tofauti, kila mmoja anasifa yake ambayo mwenzie hana! Ila sasa siwezi kumwambia mkubwa kwa sababu ataondoka aniache na ataumia sana. Bora niendelee kujifichaficha tu. Manake sasa!!
 
Mi nakushauri uwe mvumilivu maana umeamua kufuata sheria na misingi ya dini yako... bado wake wawili ukamilishe nguzo ya dini yako. Ila hili usililete hapa maana utatuchonganisha na walioleta sheria hii ya dini yenu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom