Nisadieni ndoa yangu inavunjika

Nisadieni ndoa yangu inavunjika

Mambo ya kuoa mke wa pili sio kabisa.. kama vipi mega nje kishkaji ila hii ya kuongeza mke sio
 
Dah.. humu watu wanakwepa ukweli wa kisayansi. Mwanaume ana uwezo wa kupiga game siku zote 30 kwa mwezi lakini kwa mwanamke hazizidi 7 na kama atapiga game basi anajilazimisha tu na bado akishika ujauzito ndiyo balaa, sasa mwanaume apige pichu? Au umBJ? Shukuruni pale wanaume wanapowaletea wasaidizi muwajue kwa uwazi kwani wanawapenda
 
Kweli akili ni mali kila mtu ana zake, Kwahiyo kwako kua na kazi ndo kuwa na uwezo??? TV, cable, Ktianda, dressing yani kwahiyo story tu unaonekana unakamshaara cha kukidhi mahitaji ya msingi ndio maana ulinunua kwa zamu, vya mke mkubwa kwanza halaf vya mke mdogo, ni wazi bado rizki yako haijanyooka, labda ungetuambia una nyumba ngapi (hata ukifa wanao wajistiri), Una miradi ipi ili hata leo ukipata maradhi ikulinde kimaisha na familia yako, bank una kiasi walau wake zake wakiumwa kwa pamoja una uwezo wa kuwatibu au kuwaita familia zao waje wakao nae na uzilishe familia zote wakati wanahudumia mkeo au wake zako, au ndo wakiumwa warudishwa kwao halafu wapeleka 50000 kwa mwezi. KWANZA KUOA MKE WA PILI KUWA NA SABAB PIA , SIO KISA UMEPATA KAZI ATI UONGEZE MKE, MANA WEWE SIO KAM UNA UWEZO BALI UMEPATA KAZI TU. Pole sana.
 
Ndio maana wanawake wanataka wanaume wenye pesa, bora mtuseme tu, maana una hangaika na mtu kwenye dhiki akija akikpata anakuona hufai au una kasoro, wakati unaniachia 2000 tule kutwa nzima napiga hesabu mpaka nywele zakatika, ulionyesha mapenzi yooote, sasa unawezo wa kuacha 30,000 unatafuta wakuja kutumia na sisi, wakati unapaswa unifanyie mie kwanza mazuri ya kupendeza kiasi niweze sahau maisha yalopita, walau unijengee tuishi kweney nyumba kubwa nilizokuwa nikitamani awali wakati tuko chumba kimoja, unijazie mafriji chakula wakati unaniachia 2000, LEO UNAKWENDA ONGEZA MTU AJE AISHI KWA RAHA NA WEWE, NA MIE UKINILIPA MAUMIVU..Duh! hata hivyo huyo mke ana moyo, mie ningeshakuacha na kichwa chako tope.
 
dini imeruhusu lkn wanawake nao wanamoyo wa nyama ndg km wewe ambavyo ungeumia ndivyo hivohivyo kwa kipimo kilekile. think twice.. kuishi na wanawake wengi bila amani au mkemmoja kwa amani.
 
jamani hizi tamaa mbaya ona sasa unavyo muumiza mkeo ungebaki na huyo huyo ungebabuka ndio maana watu hatuendelei kwa mambo haya umepata kaz tu ushajiongezea majukumu hiyo pesa ulitumia kama mahari na unayoendelea kuitoa kwaajili ya matunzo kwa huyo mke mdogo siungeitumia katika kuongeza patolako ndani ya familia na kufanyia mambo mengine ya maana umeenda kuoa katoto ka nn sasa zaidi ya kuwa mzigo maana nae lazima katakuwa tegemez watu wengine bhana mnafanya mambo bila kufikirisha bongo khaa
mbaya zaidi ukute hana hata nyumba shida hizi
 
Tatizo ulioa ukiwa bado mtoto ulikua ujapevuka, na hata sasa hivi ujapevuka.
 
we umaskini ulikuwa umekuathiri mpk kwenye IQ yako
 
Sasa unaowaje wawili wakati ata kutatua tatizo dogo kama hili unashindwa mwambie nae atafute mme wa pili
 
kama ambavyo mwanaume hapendi kuwa na mume mwenza ndivo ilivyo kwa wanawake. Hakuna mwanamke anayependa kushare mume, japo dini inaruhusu hata akikukubalia kuoa ni unafiki. Yule sio dada yako bhana mpk afurahie ww kuoa. khaaaaa
 
Achen ma mila mila ya ajabu karne hii et dini inaruhisu akil ya kuambiwa changanya na ya kwako
 
Umeileta mahali siyo sahihi, hamna ndoa inavunjika hapo. Wewe endelea na maisha kama kawaida
 
Yaani wewe unaoneka ni slow motion kujiongeza huwezi maisha yalikuwa magumu mkeo kakuvumilia haya mmepata ahueni umeenda kuongeza mke wa pili.kwanini hutaki nafuu ya maisha unapenda taabu na masumbuko tuu ,kwa kujibu wa maelezo yako wewe bado hujakuwa kwenye nafasi ya kuoa mke wapili kiuchumi ,eti ukamnunuilia tv ina maana yeye kafata tv hapo kwako
Mwanaume unatakiwa kuwa na akili ya ziada wewe umetaka hii ndoa ivunjike na inaonekana ulijipanga tangu mwanzo maana ulimwambia mkeo mapema , waarabu wenyewe wanapesa na wengi wao wana mke mmoja mmoja na ni faimly oriented haswa makapuku sasa!mmh
Poor you naonea huruma huyo mkeo wa kwanza na huyo wapili kwa kuolewa na bozozo
 
Izi suna zingine tuziangaliege nazo maana suna zipo nyingi sana sio kuongeza mke to
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom