Nisadieni ndoa yangu inavunjika

mahirtwahir

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
613
313
Habari zenu JF,

Ukweli mimi ni muislamu mwenye miaka 30 nimeoa mke mwaka 2007 na niko na watoto 2.

Shida toka naoa nilikuwa na maisha mabovu kiasi ila nilimuambia mke wangu siku zikinitembelea japo kwa uchache naoengeza mke wa 2 na kwa kua dini inaniruhusu.

Muda wote huo mke wangu hakuonyesha kutetereka na maneno yangu hadi ikawa ananiuliza vipi utafanya lini huo mpango wako na kuniambia nifanye ila nadhani alikuwa ananiambia kwa kua sikuwa na uwezo, Mungu mkubwa akanipa kiajira mwaka 2014 hali ikawa afadhali nikamuambia mke wangu nikimuona ataerizika namuoa hapa alionesha kutetereka maana alijua muda umekaribia masharti yakaja kama nikimuona basi mahari ya huyo nitakaemuoa na yeye nimpe hayo nikamjibu sawa.

Siku nilipompata nikadaiwa kitanda, godoro, kabati na dresing basi nikaanza kununua vya mke wangu taratibu yeye hakujua kua natimiza miadi nikaongeza kwake kwa TV na Friza na Cable ili nikiwa zamu kwa mke mdogo vimliwaze.

Baaada ya kufanya hayo kwa usiri nikaoa tarehe 22/4/2016 mama yangu baaada ya kujua kawa mkali matusi mtindo mmoja malalamiko na kusema kuwa sikumtendea haki kila nikimpoza na kunasihi basi kama moto niliomwagia petroli anasema kanivumilia katika ziki leo namlipa hili.

Mke wangu kwa kweli nampenda sana hadi najilaumu kuyaamini maneno yake hadi najisikia vibaya sana kwa maneno yake na kufikiria kumuacha mke wa pili ila nimuacheje na yeye hana kosa lolote mimi ndio nilimchagua na pia ni mtoto mdogo nimuweke mjane itakuwa sijamtendea haki na nitakuwa nimejitia aibu.

Naombeni msaada ili nizungumze na wote wanielewe na mke mkubwa atulie ingawaje toka nioe nimekua nampenda sana mke mkubwa kuliko mdogo.
 
Habari zenu JF
Ukweli mimi ni muislamu mwenye miaka 30 nimeowa mke mwaka 2007 na niko na watoto 2.
Shida toka naowa nilikua na maisha mabovu kiasi ila nilimuambia mke wangu siku zikinitembelea japo kwa uchache naengeza mke wa 2 na kwa kua dini inaniruhusu.

Hivi huwa Mnajua Jinsi Gani Wanawke wanaumia Sema Hawasemi tu... Mke Mmoja Kakushinda unataka Wa Pili

Muda wote huo mke wangu hakuonesha kutetereka na maneno yangu hadi ikawa ananiuliza vipk utafanya lini huo mpango wako na kuniambia nifanye ila nadhani alikua ananijejea kwa kua sikua na uwezo, Mungu mkubwa akanipa kiajira mwaka 2014 hali ikawa afadhali nikamuambia mke wangu nikimuona ataerizika namuowa hapa alionesha kutetereka maaana alijua muda umekaribia masharti yakaja kama nikimuona basi mahari ya huyo nitakaemuowa na yeye nimpe hayo hayo nikamjibu sawa .
Siku nilipompata nikadaiwa kitanda ,godoro ,kabati na dresing basi nikaanza kuninua vya mke wangu taratibu yeye hakujua kua natimiza miadi nikaengeza kwake kwa TV na Freza na Cable ili nikiwa zamu kwa mke mdogo vimliwaze.
Baaada ya kufanya hayo kwa usiri nikaowa tarehe 22/4/2016 mama yangu baaada ya kujua kawa mkali matusi mtindo mmoja malalamiko na kusema kua sikumtendea haki kila nikimpoza na kunasihi basi kama moto niliomwagia petroli anasema kanivumilia katika ziki leo namlipa hili.
Mke wangu kwa kweli nampenda sana hadi najilaumu kuyaaamini maneno yake hadi najisikia vibaya sana kwa manene yake na kufikiria kumuacha mke wa pili ila nimuacheje na yeye hana kosa lolote mimi ndio nilimchagua na pia ni mtoto mdogo nimueke mjane itakua sijamtendea haki na nitakua nimejitia aibu.
Naombeni nasaha ili nizungumze na wote wanielewe na mke mkubwa atulie ingawaje toka niowe nimekua nampenda sana mke mkubwa kuliko mdogo
 
Вфцф



Sawa dini yako inaruhusu, lakini navyo jua in hadi kuwe na sababu ya kufanya hivyo. Wewe sababu pekee ya kufanya hivyo ni kwakuwa umepata ajira. Kwa mwendo huu tutazidi kuwa masikini tu. Anyways ngoja nikuitie Kungwi mzoefu mstaafu FaizaFoxy
Kwakweli ni lazima kuwa na sababu ya msingi sana..sasa huyu kaka kuongeza now mwingine kafanya kwa ufahari na sio kwa kufuata dini.
 
Jamani hivi Wanawake hamuwahurumii Unajua Mnawaumiza sana Na Mambo ya Mke mWenza.. Hata Hao Wanawake wa Kiislam hawazipendi hizo ndoa.. Mlikuwa mnaishi Vizuri tu ona sasa ...Hizo hela za Mahari sijui kitanda si ungempa mkeo akafungua Kibanda Cha Nyanya Hapo...

Wanaume wengine Bhna
 
Eti TV na cable vya kumliwaza, wanaume sometimes hapana. Kwani wewe ni TV alitoka kwao Kuja kwako kuiangalia television?????
Ndio maana familia za kiafrica haziendelei, vifaa hivyo vitatu umenunua kwa kuunga unga halafu unajitia hapa una hela. Maisha haya familia mbili unaanzia wapi?
 
jamani hizi tamaa mbaya ona sasa unavyo muumiza mkeo ungebaki na huyo huyo ungebabuka ndio maana watu hatuendelei kwa mambo haya umepata kaz tu ushajiongezea majukumu hiyo pesa ulitumia kama mahari na unayoendelea kuitoa kwaajili ya matunzo kwa huyo mke mdogo siungeitumia katika kuongeza patolako ndani ya familia na kufanyia mambo mengine ya maana umeenda kuoa katoto ka nn sasa zaidi ya kuwa mzigo maana nae lazima katakuwa tegemez watu wengine bhana mnafanya mambo bila kufikirisha bongo khaa
 
Mambo ya ajabu sana haya. Sasa hiyo raha yenyewe unaipataje na maisha ya kuungaunga.
Bora uungaunge ukiwa na mke mmoja sasa wawili tena??

Anyways kwa mujibu wa imani yako huna kosa ngoja waje wataalam wa mambo haya sisi tunaweza kukukwaza.
Eti TV na cable vya kumliwaza, wanaume sometimes hapana. Kwani wewe ni TV alitoka kwao Kuja kwako kuiangalia television?????
Ndio maana familia za kiafrica haziendelei, vifaa hivyo vitatu umenunua kwa kuunga unga halafu unajitia hapa una hela. Maisha haya familia mbili unaanzia wapi?
 
Habari zenu JF
Ukweli mimi ni muislamu mwenye miaka 30 nimeoa mke mwaka 2007 na niko na watoto 2.

Shida toka naoa nilikua na maisha mabovu kiasi ila nilimuambia mke wangu siku zikinitembelea japo kwa uchache naengeza mke wa 2 na kwa kua dini inaniruhusu.

Muda wote huo mke wangu hakuonesha kutetereka na maneno yangu hadi ikawa ananiuliza vipi utafanya lini huo mpango wako na kuniambia nifanye ila nadhani alikua ananijejea kwa kua sikuwa na uwezo, Mungu mkubwa akanipa kiajira mwaka 2014 hali ikawa afadhali nikamuambia mke wangu nikimuona ataerizika namuowa hapa alionesha kutetereka maana alijua muda umekaribia masharti yakaja kama nikimuona basi mahari ya huyo nitakaemuoa na yeye nimpe hayo nikamjibu sawa.

Siku nilipompata nikadaiwa kitanda, godoro, kabati na dresing basi nikaanza kununua vya mke wangu taratibu yeye hakujua kua natimiza miadi nikaongeza kwake kwa TV na Friza na Cable ili nikiwa zamu kwa mke mdogo vimliwaze.

Baaada ya kufanya hayo kwa usiri nikaoa tarehe 22/4/2016 mama yangu baaada ya kujua kawa mkali matusi mtindo mmoja malalamiko na kusema kuwa sikumtendea haki kila nikimpoza na kunasihi basi kama moto niliomwagia petroli anasema kanivumilia katika ziki leo namlipa hili.

Mke wangu kwa kweli nampenda sana hadi najilaumu kuyaamini maneno yake hadi najisikia vibaya sana kwa maneno yake na kufikiria kumuacha mke wa pili ila nimuacheje na yeye hana kosa lolote mimi ndio nilimchagua na pia ni mtoto mdogo nimueke mjane itakua sijamtendea haki na nitakua nimejitia aibu.

Naombeni nasaha ili nizungumze na wote wanielewe na mke mkubwa atulie ingawaje toka nioe nimekua nampenda sana mke mkubwa kuliko mdogo
Samahani mkuu, Hivi kwa nini waisilamu wenye asili ya kiarabu huwa hawaoi wake wawili au zaidi hovyo?, mara nyingi naona waislamu wenye asili ya kibantu ndo kutwa kuongeza wake.
 
Namuonea huruma mke mkubwa, mke kaweza kukaa na wewe kwa maisha ya dhiki leo umepata badala ya kufanya sasa afurahi aanze kuvaa vzr na kupendeza na kuongeza ka mradi na yeye asimamie sas wewe umeleta balaa jingine??
Ifike mahali wanaume tujitazame vzr na kufanya maamuzi yenye tija kwa ustawi wa familia zetu.
jamani hizi tamaa mbaya ona sasa unavyo muumiza mkeo ungebaki na huyo huyo ungebabuka ndio maana watu hatuendelei kwa mambo haya umepata kaz tu ushajiongezea majukumu hiyo pesa ulitumia kama mahari na unayoendelea kuitoa kwaajili ya matunzo kwa huyo mke mdogo siungeitumia katika kuongeza patolako ndani ya familia na kufanyia mambo mengine ya maana umeenda kuoa katoto ka nn sasa zaidi ya kuwa mzigo maana nae lazima katakuwa tegemez watu wengine bhana mnafanya mambo bila kufikirisha bongo khaa
 
Duh.

Hivi kwenye maisha haya bado kuna watu wanaoa wake wawili??

Ili iweje??
Halafu usiku na mchana anaweza atunzeje familia, mwishowe tendo la ndoa sifuri kisa msongo wa mawazo, wanawake wake wanaanza kuchepuka hawezi kuwatosheleza kifedha na kindoa. Hata mimi ntachepuka tu, hakuna haja ya kuvumilia matatizo na shida za kujitakia
 
Jamani kiukweli oa mke wa pili kutokee kasoro kwa mke wa kwanza ambayo huyo mke wa kwanza hawezi kuitatua lakini siyo kuoa mke eti kwa sababu kipato kimeongezeka hilo ni kosa ktk ndoa
 
Kuna Wimbo wa Jabari la muziki Tanzania Hayati Marijani, "Ooooh ukeweza, ukeweza una matatizo, kwa kina baba ni kicheko, ila kwetu (kina mama) ni matatizo, oohh oohh matatizo".

Hapo mkeo hana kosa lolote bali mwenye kosa ni wewe. Na wahenga hawakukosea waliposema, "maskini akipata matako hulia mbwata". Pengine umeongeza mke wa pili pasipo hata huyo mkeo wa kwanza kumpatia Bima ya Afya.
 
Nawachukia nyie watu mnaochezea hisia za wenzenu, ni sababu ipi ilikufanya uongeze mke wa pili kwa kuwa umepata ajira? hivi una uhakika kuwa utadumu kwenye hiyo ajira milele? na je ajira ikiisha utamuacha huyo mke wa pili. Acha upumbavu kijana ukijiangalia hapo unaiishi uswahilini chumba kimoja cha kupanga
 
Hayo ya ndoa za mitala mie sijui chochote, ila hiyo mahali kiboko ndugu yangu, dressing table inakuaje sehemu ya mahali? Hizi mila za wapi?
 
Back
Top Bottom