Nisadieni ndoa yangu inavunjika

Nisadieni ndoa yangu inavunjika

Namuonea huruma mke mkubwa, mke kaweza kukaa na wewe kwa maisha ya dhiki leo umepata badala ya kufanya sasa afurahi aanze kuvaa vzr na kupendeza na kuongeza ka mradi na yeye asimamie sas wewe umeleta balaa jingine??
Ifike mahali wanaume tujitazame vzr na kufanya maamuzi yenye tija kwa ustawi wa familia zetu.
kwakweli sometimes muwe mnafikir kabla ya kutenda saa nyingine maamuzi mnayoyafanya mnawaumiza wake zenu usifanye kitu kwa kuiga hapo mke alitegemea atapata unafuu baada ya mume kupata kaz kumbe ndio kwanza mume hajitambui anachokifanya hakijui
 
Halafu usiku na mchana anaweza atunzeje familia, mwishowe tendo la ndoa sifuri kisa msongo wa mawazo, wanawake wake wanaanza kuchepuka hawezi kuwatosheleza kifedha na kindoa. Hata mimi ntachepuka tu, hakuna haja ya kuvumilia matatizo na shida za kujitakia
Ni kweli aisee.

Jamaa inaonekana bado kiuchumi hayuko stable, kwanza ndio kapata kikazi, badala hata ya kufikiria kununua kashamba hata afuge kuku kujiongezea kipato tayari kakimbilia kuongeza mke wa pili na ndio kwanza ana miaka 30.

Hajui ameongeza wigo wa watafuna kakipato kake.?? Akichapiwa na watoto wa mujini atalalamika??

Nashindwa kuelewa kabisa hizi fikra vijana huwa wanazipata wapi.

Mimi huwa nawakubali sana wachaga, akipata kamwanya ka kupata hela mahali baada ya miaka miatu utakuta ana bonge la mradi unaomuongezea kipato, mswahili wa Pwani akipata ka mwanya ka kupata pesa utamkuta ana bonge la foleni la wanawake "waliojaaliwa", halafu wanalalamika maisha magumu kipato hakitoshi.
 
Hayo ya ndoa za mitala mie sijui chochote, ila hiyo mahali kiboko ndugu yangu, dressing table inakuaje sehemu ya mahali? Hizi mila za wapi?
ha ha ha huko kutakuwa ukanda wa Pwani tu aisee.

Mchaga akipata kazi ya kamshahara kazuri anawaza kuongeza kamradi na kusomesha watoto wake shule nzuri, mtu wa Pwani akipata kikazi anawaza kuongeza mke wa pili, sasa ana watoto wawili hajawahi hata kujiuliza watasoma vipi, keshakimbilia kuongeza mke wa pili.

Usikute hata nyumba anayoishi ni ya vyumba vitatu kimoja chake, kingine cha watoto kingine ni sebule, hata kujenga labda hata hajajenga, leo anakimbilia kuoa mke wa pili?? kijana wa miaka 30??

Dah, aliyeturoga waafrika kweli alituweza na bahati mbaya kafa.....
 
Nina uhakika kabisa kuwa hili suala la kuongeza mke wa pili hukumshirikisha ipasavyo....bali uliamua baada ya kuona kidogo mambo yamekunyookea....hii si nzuri kwani umesababishia sononeko huyo mkeo wa kwanza ambaye ninaweza kusema kuwa ni chanzo cha mafanikio kwani alikuvumilia kipindi huna kitu na umefika wakti wa yeye kufaidi matunda ya uvumilivu wake wewe tena unamletea dhiki ya moyo....hii sio haki hata kidogo......sononeko la mkeo wa kwanza linaweza kufanya ndoa yako mpya kujaa visa na mikasa au mabalaaa......

Ninchokushauri ni kuwa wanawake ni viumbe waelewa sana na ni viumbe ambao ni wepesi wa kusamehe.....kaaa chini na mkeo mkubwa na kama kuna sehemu ulimkwaza muombe msamaha na muendelee na maisha.......ni hali yenye kuchoma moyo.....jaribu kuvaa uhusika wa mkeo alafu uone ni jinsi gani inavyochoma na kuumiza......
 
Du,kwa hiyo kipato kikiongezeka tena unaoa mwingine?hatari sana
 
Halafu usiku na mchana anaweza atunzeje familia, mwishowe tendo la ndoa sifuri kisa msongo wa mawazo, wanawake wake wanaanza kuchepuka hawezi kuwatosheleza kifedha na kindoa. Hata mimi ntachepuka tu, hakuna haja ya kuvumilia matatizo na shida za kujitakia
Pole yake mimi si mchepukaji lakini ktk hali hii ni bye bye ntachepuka na kumsahau huyo mme maana nimekuwa na wewe kwenye shida zote sasa unapata hela unachukuwa mwingine hata nikupendeje sitakuvumilia
 
Siwezi kuielewa hii case, naona maluweluwe. Wenye dini kama yako watakushauri vizuri.
 
life is unfair.. treats some as royals others as shits... hii mada imeniharibia siku...
 
Tuanzie apo kwenye Tv, friza na cable umeweka kwa mke mkubwa tu imuliwaze ama na mke mdogo umemununulia?? Pili huna zaid ya miaka 2 kazini na umeongeza mke wa 2. Jiandae tu kuishi kama mzuka, usitarajie kuendelea kuona upendo na furaha kutawala maisha yako na mke mkubwa kama zamani. Hapo umejiongezea stress, pressure na kukarbisha uzeee. Ukimwacha mke mdogo hautabaki salama na mke mkubwa akiondoka pia hautabaki salama.
 
Habari zenu JF,

Ukweli mimi ni muislamu mwenye miaka 30 nimeoa mke mwaka 2007 na niko na watoto 2.

Shida toka naoa nilikuwa na maisha mabovu kiasi ila nilimuambia mke wangu siku zikinitembelea japo kwa uchache naoengeza mke wa 2 na kwa kua dini inaniruhusu.

Muda wote huo mke wangu hakuonyesha kutetereka na maneno yangu hadi ikawa ananiuliza vipi utafanya lini huo mpango wako na kuniambia nifanye ila nadhani alikuwa ananiambia kwa kua sikuwa na uwezo, Mungu mkubwa akanipa kiajira mwaka 2014 hali ikawa afadhali nikamuambia mke wangu nikimuona ataerizika namuoa hapa alionesha kutetereka maana alijua muda umekaribia masharti yakaja kama nikimuona basi mahari ya huyo nitakaemuoa na yeye nimpe hayo nikamjibu sawa.

Siku nilipompata nikadaiwa kitanda, godoro, kabati na dresing basi nikaanza kununua vya mke wangu taratibu yeye hakujua kua natimiza miadi nikaongeza kwake kwa TV na Friza na Cable ili nikiwa zamu kwa mke mdogo vimliwaze.

Baaada ya kufanya hayo kwa usiri nikaoa tarehe 22/4/2016 mama yangu baaada ya kujua kawa mkali matusi mtindo mmoja malalamiko na kusema kuwa sikumtendea haki kila nikimpoza na kunasihi basi kama moto niliomwagia petroli anasema kanivumilia katika ziki leo namlipa hili.

Mke wangu kwa kweli nampenda sana hadi najilaumu kuyaamini maneno yake hadi najisikia vibaya sana kwa maneno yake na kufikiria kumuacha mke wa pili ila nimuacheje na yeye hana kosa lolote mimi ndio nilimchagua na pia ni mtoto mdogo nimuweke mjane itakuwa sijamtendea haki na nitakuwa nimejitia aibu.

Naombeni msaada ili nizungumze na wote wanielewe na mke mkubwa atulie ingawaje toka nioe nimekua nampenda sana mke mkubwa kuliko mdogo.
Watu kama nyinyi ni shida tuu. Yaani umeongeza mke wa pili kwa vile tu sasa kipato kimeruhusu? Kikishuka jee itakuaje??
Sisi wanaume[hata humu jamvini] tumekuwa msitari wa mbele kuwalaumu kina mama kwa mambo mengi tu ila udhaifu wetu wa kutembea na ma house girls, vimada, rafiki za wake zetu tunaona sawa tu. Hivi hufikirii kuwa sis ndiyo chanzo cha ndoa nyingi kubomoka??? Hebu fikiria mkeo amestahamili taabu wakati huna kitu [inawezekana alikosa vitu vingi tu] lakini leo umepata umemtafutia mwenza wale pamoja.
 
jamani lazina kwanza tufahamu kua dini imeruhusu mke zaidi ya mmoja sio kwa sababu tu mmoja anamatatizo.bali hilo ni jambo lakimaumbile kutokana na asili ya maumbile ya mwanaume haridhiki na mmoja.sasa ili kuzuia uchepukaji ndio ukawekwa mlango huo kwa mtu muadilifu.kiukweli ndugu umekosea sana kwa maamuzi yako yaliyo na uchache wa tafakuri japo sio muda wakukulaumu sababu tayari ishatokea.chakufanya kwa sasa ni kukiri mbele ya mkeo kwamba umemkosea na jitahidi kumuonyesha mapenzi zaid.lakini pia lazima kutakua na ustadh au sheikh ambae anamkubali sana,jaribu kumuomba sheikh ampe nasaha natumai itasaidia.pia muombe mungu alete utulivu kwenye ndoa yenu.ila siku nyengine usiwe mtu wakukurupuka.
 
Yani umeoa mke wa pili lakini unampenda sana mke mkubwa kuliko mdogo..Hapo mke mdogo hata mwezi tu hajamaliza..Hapa ndo uwa nashindwa kuelewa hii mantiki ya kuoa wanawake wengi..Ulioa ili iwaje sasa..
 
Yaani mwenzenu swala LA mime kuoa mke was pili mm wala silichukii iswear sijui kwann yaani nashukuru bcz naona kama amenipunguzia shurba za kupika kila Siku na kum take care, bora upate mwingne tusaidiane jamani ,hvi inakuaje MTU unataka ulale na mtu mmoja miaka nenda rudi kwa huchoki kila siku unamuona kila siku munalala na kuamka pamoja kaaah jamani binadamu tumeumbwa kukinai so mm mume wangu akitaka kuoa nakubali kwanza utapata radhi za mola wako unamueshia uzinifu na itapunguza magonjwa kwa wanandoa. Ongea tu na mkeo na hakikisha unatenda haki bcz usipokua muadilifu kwa Huyo mdogo usie mpenda humtendei haki
 
Pole yake mimi si mchepukaji lakini ktk hali hii ni bye bye ntachepuka na kumsahau huyo mme maana nimekuwa na wewe kwenye shida zote sasa unapata hela unachukuwa mwingine hata nikupendeje sitakuvumilia
Eti kamnunulia TV ajiliwaze, TV yenyewe usishangae ukikuta ni singsin. Akutukanaye hakuchagulii tusi. Kuchepuka muhimu, heri kuliwazwa na mtu kiwizi wizi kuliko kuliwazwa na TV
 
Ndivo mlivyo nyie mkeo yupo sahihi ila utafulia muda sio mrefu subiri mkeo na yeye akuletee mume mwenzako
 
we kweli mburula kweli kwhyo tv ndyo kupata maisha mazuri?mke wapili wann km cyo tamaako ya mwili au kuna faida yeyote ile?
 
Cha kufanya jaribu kumnunulia mke mkubwa gari anaweza akatulia.

Na asipotulia ajaribu kumjengea angalau kanyumba ghorofa moja. Hakuna namna....... ndo alichokuwa anakitafuta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom