Nirudiane au nisirudiane na mpenzi wangu wazamani?

Nirudiane au nisirudiane na mpenzi wangu wazamani?

Then tulia mama fanya yako! !!
Tena hiyo jmosi, mpe bby wako mahaba yooooooote ili umtoe wasiwasi wa kumkimbia for the so called ndoa ya kikristu!

Unaposhikwa shikamana mama!

Tulishaambiwa USITUPE MBACHAO KWA MSALA UPITAO (sijui ndo hivo ) Ila watu hawaelew

Hahahaaahaaaa nimeipenda iyo (USITUPE MBACHAO KWA MSALA UPITAO!NALO NENO
 
Usharudi wangu nenda lakini wambie ukweli kuwa haiwezekani tena una mtu mwengine na uwakumbushe walipo kufukuza leo iweje maji yakisha mwagika hayazoeleki au pia bora usiende wambie wazazi wako kua huwezi kwenda watakuelewa maana wanajua walivyo kufanyia malipo ni duniani akhera huwenda hisabu tu
 
wana jf,

natumaini mnaendelea vizuri na maisha yenu ya kila siku.nimekuwa msomaji mzuri sana wa posts za watu humu ndani kwa muda mrefu sana na nisiposema nimefaidika nitakuwa muongo,nikaona na mimi nijiunge nipate nafasi ya kusema yale machache ninayoyajua kuchangia discussions za humu ndani. Huu ni uzi wangu wa kwanza kuanzisha humu.

Mimi ni mwanamke niko kwenye late thirties, nilipata ujauzito nikiwa na miaka 18 ndio nimemaliza tu form 4 nikisubiri matokeo niendelee form 5, kijana aliyenipa ujauzito alikuwa anafanya kazi ya kuuza kwenye duka la muhindi fulani huku akisubiri kwenda chuo kikuu.

Wazazi wa pande zote wakaamua tufungishwe ndoa ya haraka haraka na sisi hatukupinga kwa sababu tulipendana sana sana.mwaka 1998 tukabarikiwa na mapacha wa kike na wa kiume tulifurahi sana na maisha yakaendela vizuri huku kila mmoja akitafuta nafasi ya kujiendeleza kimasomo.

Mume wangu akapata scholarship ya kwenda kusoma australia, alipata wafadhili walioahidi kumsomesha degree ya kwanza na ya pili ingebidi ajitegemee. Tulifurahi sana nilimshukuru mungu nikamruhusu aende tena bila kinyongo kwani nilijua huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mazuri ya familia yetu changa.

Mawasiliano yalikuwa sio kama wakati huu internet café ndio ilikuwa habari ya mjini lisaa la kutumia huduma ya mtandao iliweza kufikia elfu 5.nilijitahidi sana kufanya mawasiliano naye angalau mara moja kwa wiki na yeye pia alifanya hivyo huku nikidhani mapenzi yetu yangedumu na angerudi tuendeleze maisha pamoja.

Alipoanza mwaka wa pili mawasiliano kwa upande wake yalipungua na nilipouliza niliambiwa masomo magumu na muda mwingi anatumia kusoma akifeli ingekuwa aibu na muda uliopotea.sikupinga hilo na sikulalamika. Kuna wakati ulipita mwezi hajajibu email. Nilianza kupatwa na wasiwasi lakini nilivumilia na nikampa moyo afanye bidii kwenye masomo yake.

Miaka minne ikaisha na akarudi nyumbani ila sikupewa taarifa. Habari nilizipata kwa mdogo wake wa kike ambaye tulikuwa marafiki sana kuwa amerudi akiwa na muke wa kizungu. Sikuamini masikio yangu nikafunga safari kwenda kwa wazazi wake ambako ndiko alikofikia na huyo mke wake mpya.

Nilipofika sikuwakuta, wazazi wake walinitimua kama mwizi huku wakiniambia sitaki mtoto wao awe tajiri. Ameshapata mzungu na walikuwa na mpango wa kufungua kampuni. Niliumia sana nikajaribu kila niwezalo kumrudisha mume lakini haikuwezekana, nikarudi kwa wazazi wangu na mapacha wangu mwaka 2003.

Baada ya kuona maisha yalikuwa yananiendea kombo. Nilishindwa kufanya kazi zangu na stationery shop yangu ikafungwa kwa kukosa uangalizi. Kwa kifupi nilichanganyikiwa. Wazazi wangu na wadogo zangu walinifariji na kunisaidia sana 2004 nikaanza biashara ya stationery tena nikiomba mungu na kufanya kazi kwa bidii nifaniikiwe ili walionitupa na kunidharau waone mafanikio yangu.

Shangazi yangu akanifundisha biashara ya mbao na hapo ndipo nilipouona mkono wa mungu. Mambo yangu ya kifedha yakabadilika na mpaka sasa silalamiki. Nikaamua kujiendeleza kimasomo na sasa nina kadegree. Watoto wangu nao wako vizuri wameingia kidato cha tano mwaka huu.

Mwaka 2011 nikutana na mbaba mgane na tukaanzisha mahusiano, mpaka sasa tuko kwenye mahusiano. Watoto wetu wamekubaliana na hali halisi na tunaishi nyumba moja ingawa hatujafunga ndoa. 2014 nikaomba talaka kwa mume aliyeniacha kwa sababu ya mzungu akakataa huku akidai ndoa ya kikristu haivunjwi.

Sasa amerudi sijui nini kimempata na wala sitaki kujua anataka turudiane. Nimekataa kabisa, wazazi wake wamekuja kunibembeleza na kinisihi nimsamehe kijana wao na msimamo wangu ni ule ule. Jumamosi hii kuna kikao nyumbani kwa wazazi wangu, wameomba waje kwenye mazungumzo na mimi niwepo.

Hapa ndio nahitaji ushauri wenu. Niende peke yangu, niende na huyu mpenzi wangu wa sasa au nisiende kabisa. Msimamo wangu ni ule ule siwezi kurudiana.

don't go....no way, do not go
 
Sioni sababu ya wewe kwenda,
Unakwenda kufanya nini?
Wakiuliza waambie umejadiliana na mwenzako hakuridhika na hicho kikao basi.
 
Natamani sana ningeweza kuishi kihalali na huyu mpenzi wangu wa sasa. Ndio maana nadai talaka. Ningejua angekuja kukataa ningedai mapema hilo wazo halikunijia wakati ule.

Dada yangu umeamua kujipa stress, wewe ulipaswa kufunga Ndoa yako mpya bila tatizo, ile ilikufa natural death kimwili na ulimwengu wa Roho,alivyooa Mzungu na Wazazi wake walivyokufukuza.nikuulize swali rahisi,angebaki Ulaya na yule Mzungu ungeomba talaka kwa nani?!! Mungu anajua yaliyokupata,chukulia kama Huyo Ex alishakufa hayupo,chapa lapa na Ndoa mpya,yeye ndo aende Mahakamani, ukienda wewe,utapoteza hela,mda na stress juu
 
Dada angu...stori yako inauma sana...ila nagundua kuwa bado kuna chembechembe zake ndani yako ambazo ndizo zinazokufanya uwe njia panda pamoja na msimamo wote ulionao....i wish ningekutana na wewe uso kwa uso ningeongea mengi zaidi....lakini kama alikunyima talaka...hebu kasome Mathayo 19:9....nami nawaambia ninyi,kila mtu atakayemuacha mkewe, ispokuwa ni kwa sababu ya uasherati.......sasa hapo haimuhusu yeye kukuacha hata wewe unaruhusiwa kumuacha maana amefanya uasherati, ndoa kuwa ya dini ya kikristo sio kama haivunjiki...kama kuna uasherati hapo katikati inavunjwa tu....(eee maana hamna namna nyingine) ....lakini hata hivyo huyu jamaa hakupendi wala nini, anataka kupata nafasi ya kukuharibia zaidi...angekupenda asingeweza kuvumilia wakati unaumia...na ni bora usiende kwenye hicho kikao maana maneno yananguvu sana ya kubadilisha hata huo msimamo ulionao....but mi nakwambia usitake vichache ukaacha vingi....
 
Then tulia mama fanya yako! !!
Tena hiyo jmosi, mpe bby wako mahaba yooooooote ili umtoe wasiwasi wa kumkimbia for the so called ndoa ya kikristu!

Unaposhikwa shikamana mama!

Tulishaambiwa USITUPE MBACHAO KWA MSALA UPITAO (sijui ndo hivo ) Ila watu hawaelew

Kasome Mathayo 19: 9 halafu nenda mahakamani kadai talaka yako....hana lolote la kukuzuia....
 
kuna wanaume wanaumiza sana.Hii post imenifanya nikumbuke mbali sana. Anyway we waheshimu wazazi hudhuria ila simamia msimamo.
 
Nenda na huyo mchumba wako mpya ili aone hata wewe una uwezo wa kupendwa kama yeye alivyopendwa.
 
Pole sn.huna haja ya kwenda na mpenzi wako wa sasa.show that ni masmuzi yako na siyo kusaidiwa na mpenzi wa sasa.ni kweli ni changamoto mana ndoa ya kikristo haivunjwi ila nakushauri consult wachungaji (wasomi)wakushauri kwa hili.
 
Japo Bibilia inasema alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe,mimi naamini juu ya Mungu ninaye mwamini hana unyama wa namna hiyo aliokutendea huo ufirauni.
Mie nakuunga mkono maamuzi yako ila kiukweli usiende huko.
 
Jibu langu na ushauri wangu ukikubali utakua Mende
 
Nenda kwa kuitika wito ila kakatae maneno!!!. songa mbele usigeuke nyuma.
 
Mi nakushauri usiende! Labda kama maongezi yangehusu wototo au mali lakini kurudiana' hiyo kitu hapana
 
mbele daima ukigeuka nyuma yatakukuta ya ruthu
 
usiende ukitaka kwenda nenda ma mumeo wa sasa fullstop
 
Nenda kawasikilize kwa heshima ya wazazi wako waliokubali kuwakaribisha kwenu, wakiomba msamaha waambie umesamehe lakini usikubali kurudiana kamwe na wasisumbuke kukutafutia vikao vingine maana hutatokea na hamna kitakachobadili maamuzi yako, kwanza hata kabla hamjakaa kikao waambie kabisaaa wazazi wako msimamo ulionao wala wasije kujitia kimbelembele kusimama na waomba msamaha, yani watulie kimya waachiwe ukumbi walioomba kikao, as a matter of fact mimi ninge raise issue ya talaka hapo hapo...
Na kama jamaa yako mpya anajua story nzima Huhitaji kwenda nae, he don't need all the drama just be strong. Wasijemvizia wakammwagia tindikali bure kwa kuwatosa kwako.
 
Yaani nimefikiria sana mateso uliyopitia plus twins on the top. You are a super woman ever. Binafsi ndoa naichukulia kama ni Wito lakini kaatika Wito huo kama mmoja wao amevunja or Kwenda kinyume na maandiko honestly I don't baby sitting ujinga kama huo. Yote yanavumilika but not Uzinzi and Abuse . Dear move on with your life. Mtangulize Mungu in your decision . Nenda kawasikilize because ni wazazi nenda na huyo mchumba wako Wa sasa ili asijisikie vibaya. Wasikilize watakachoongea hadi mwisho . Wakimalimaliza waambie wazazi nashukuru kwa mliyooyaongea but now what I want is my Divorce as mnavyoona I moved on with my life after your son abounded me with my kids. Nimeshasamehe yote mliyonifanyia but I can't take him back nataka talaka yangu for now that's it. Dada simamia msimamo wako. Na hii iwe fundisho kwa baadhi ya wanaume walio ughaibuni , waliooa bongo na watoto MTU umeshajijua una Familia why usishee na mama watoto wako the Truth uliyoikuta huko mkashauriana kwa pamoja either urudi home Tz or ubaki ughaibuni kwa muda ili utengeneze makaratasi ili uweze kufanya maisha bila kuuumiza Familia zao walizoziacha Tz. Wengi baadhi yao wanachanganywa na hao wazungu kwa ulimbukeni wakiwaona wazungu ni Mali kumbe hamna kitu matokeo yake walichokifuata hawakipati ahadi walizoahidiwa are empty wanaishia kurudi home with nothing . Hapo sasa ndio wanaanza kuyafuta Yale matapishi waliyotapika before wanasahau kuwa kuna different seasons ya kuyafanya Yale matapishi yawe bado mabichi or yawe yamekauka. So too bad kwa baba watoto wako matapishi aliyoyatapika yalikauka na kuzolewa now ni Gold . Kwa sababu you shine now he can see you . Hebu naomba ujiulize dear kama asingerudishwa aka Fanya business na huyo mzungu wake angekukumbuka? The answer is no . So darling move on with all blessings . Even God hates sexual immortals. Aliivunja ndoa mwenyewe . Thanks.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom