Wide Open EYES
Senior Member
- Jul 16, 2015
- 140
- 57
Wana JF,
Natumaini mnaendelea vizuri na maisha yenu ya kila siku.Nimekuwa msomaji mzuri sana wa posts za watu humu ndani kwa muda mrefu sana na nisiposema nimefaidika nitakuwa muongo,nikaona na mimi nijiunge nipate nafasi ya kusema yale machache ninayoyajua kuchangia discussions za humu ndani. Huu ni uzi wangu wa kwanza kuanzisha humu.
Mimi ni mwanamke niko kwenye late thirties, nilipata ujauzito nikiwa na miaka 18 ndio nimemaliza tu form 4 nikisubiri matokeo niendelee form 5, kijana aliyenipa ujauzito alikuwa anafanya kazi ya kuuza kwenye duka la muhindi Fulani huku akisubiri kwenda chuo kikuu.
Wazazi wa pande zote wakaamua tufungishwe ndoa ya haraka haraka na sisi hatukupinga kwa sababu tulipendana sana sana.Mwaka 1998 tukabarikiwa na mapacha wa kike na wa kiume tulifurahi sana na maisha yakaendela vizuri huku kila mmoja akitafuta nafasi ya kujiendeleza kimasomo.
Mume wangu akapata scholarship ya kwenda kusoma Australia, alipata wafadhili walioahidi kumsomesha degree ya kwanza na ya pili ingebidi ajitegemee. Tulifurahi sana nilimshukuru Mungu nikamruhusu aende tena bila kinyongo kwani nilijua huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mazuri ya familia yetu changa.
Mawasiliano yalikuwa sio kama wakati huu internet café ndio ilikuwa habari ya mjini lisaa la kutumia huduma ya mtandao iliweza kufikia elfu 5.Nilijitahidi sana kufanya mawasiliano naye angalau mara moja kwa wiki na yeye pia alifanya hivyo huku nikidhani mapenzi yetu yangedumu na angerudi tuendeleze maisha pamoja.
Alipoanza mwaka wa pili mawasiliano kwa upande wake yalipungua na nilipouliza niliambiwa masomo magumu na muda mwingi anatumia kusoma akifeli ingekuwa aibu na muda uliopotea.Sikupinga hilo na sikulalamika. Kuna wakati ulipita mwezi hajajibu email. Nilianza kupatwa na wasiwasi lakini nilivumilia na nikampa moyo afanye bidii kwenye masomo yake.
Miaka Minne ikaisha na akarudi nyumbani ila sikupewa taarifa. Habari nilizipata kwa mdogo wake wa kike ambaye tulikuwa marafiki sana kuwa amerudi akiwa na muke wa kizungu. Sikuamini masikio yangu nikafunga safari kwenda kwa wazazi wake ambako ndiko alikofikia na huyo mke wake mpya.
Nilipofika sikuwakuta, wazazi wake walinitimua kama mwizi huku wakiniambia sitaki mtoto wao awe tajiri. Ameshapata mzungu na walikuwa na mpango wa kufungua kampuni. Niliumia sana nikajaribu kila niwezalo kumrudisha mume lakini haikuwezekana, nikarudi kwa wazazi wangu na mapacha wangu mwaka 2003.
Baada ya kuona maisha yalikuwa yananiendea kombo. Nilishindwa kufanya kazi zangu na stationery shop yangu ikafungwa kwa kukosa uangalizi. Kwa kifupi nilichanganyikiwa. Wazazi wangu na wadogo zangu walinifariji na kunisaidia sana 2004 nikaanza biashara ya Stationery tena nikiomba Mungu na kufanya kazi kwa bidii nifaniikiwe ili walionitupa na kunidharau waone mafanikio yangu.
Shangazi yangu akanifundisha biashara ya mbao na hapo ndipo nilipouona mkono wa Mungu. Mambo yangu ya kifedha yakabadilika na mpaka sasa silalamiki. Nikaamua kujiendeleza kimasomo na sasa nina kadegree. Watoto wangu nao wako vizuri wameingia kidato cha tano mwaka huu.
Mwaka 2011 nikutana na mbaba mgane na tukaanzisha mahusiano, mpaka sasa tuko kwenye mahusiano. Watoto wetu wamekubaliana na hali halisi na tunaishi nyumba moja ingawa hatujafunga ndoa. 2014 nikaomba talaka kwa mume aliyeniacha kwa sababu ya mzungu akakataa huku akidai ndoa ya kikristu haivunjwi.
Sasa amerudi sijui nini kimempata na wala sitaki kujua anataka turudiane. Nimekataa kabisa, wazazi wake wamekuja kunibembeleza na kinisihi nimsamehe kijana wao na msimamo wangu ni ule ule. Jumamosi hii kuna kikao nyumbani kwa wazazi wangu, wameomba waje kwenye mazungumzo na mimi niwepo.
Hapa ndio nahitaji ushauri wenu. Niende peke yangu, niende na huyu mpenzi wangu wa sasa au nisiende kabisa. Msimamo wangu ni ule ule siwezi kurudiana.