Nirudiane au nisirudiane na mpenzi wangu wazamani?

Nirudiane au nisirudiane na mpenzi wangu wazamani?

Uwiiiii nimecheka hapa kama chizi. Hapana hana rasta.. kwa nini umeuliza?
Nilikua naomba kuuliza, Huyo mume wako wa zamani, karudi na nywele za rasta? Hilo sio swali la kizushi ila naomba unijibu Kama unaweza.
 
Nenda na Mpenzi wako was sasa ili update ujasiri wa kuwapa za uso.Huyo mwanaume na wazazi wake Si watu wazuri, kipindi we we unalilia ndoa yako ilikuwaje wasikuhurumie? Halafu Leo watake wewe umhurumie huyo Mpuuzi? Timua kabisa huyo mwehu.
 
pole dada ila hapo sioni maana ya kikao kama una msimamo wako basi usiende ili wajue msimamo wako subiria wazazi wako ndo wakuite....!!!
wakat wanakufukuza hawakuona thaman yako sasa kama ilivyo kwao na wewe usione thaman yao usiende fanya shughuli zako tu.....!!!!!
 
unastahili kupongezwa hongera saana mdada. Binafsi sidhani kuna maana yoyote ya kufanya uende kusikiliza wapuuzi kama hao. Kama pesa ipo kale bata tu midada na njemba wako
 
Ushauri wa miss chagga umetulia sana,stick kwenye huo ushauri,kifupi alikuona wa nn tena ktk kipindi kigumu wa nn tena sasa?au umebadilika nn mpk akuone wa maana?endelea na maisha yk achana na hizo propaganda za wazee c kila wanachokitaka wazazi ni kizuri vingine bomu,fuata moyo wako
 
kama ni kweli ulichopitia pole sana mwanamke mwenzangu.sioni sababu ya kuruhusu watu kukuamlia maisha yako.uende kufanya nini wakati alisha ku-delete?unachotakiwa kufanya ni kum-delete completely.kama ulivyosema msimamo wako ni uleule basi hatakwenye kikao usiende.wanawake tuwe na misimamo.unadhan wewe ungemfanyia mwanaum hivyo angekua hata anatime na wewe?why?kwasabab wanaume wanamisimamo ukisha haribu tu basi.
 
kawasikilize ila ujue kwa sasa wamechanganyikiwa maana hata mzungu wao alishampa mtoto wao talaka,ww ulionekana fisi alipokuwepo mzungu,ndoa ni ndoa pale inapopewa thamani kama mmoja wenu hajali sio ndoa,Ukristo haumtumi mtu kwenda kuchezea mbunye Australia alafu arudi aseme ww mke wake hiyo haipo achana nae akatafute mwanamke mwingine.
 
Niliuliza Kama karudi na nywele za rasta manake kuna jamaa mbongo ila kaishi Australia muda mrefu, yaani Ana tu rasta hivi tuchafu chafu. Yaani kwenye biashara ni tapeli wa kufa mtu. Yupo bongo likizo isiyoisha, yaani Huyo ni mwingi wa Maneno ila biashara ni zero, tapeli wa kufa mtu. Nilifikiria ni Huyo manake Kaliza wengi sana kwenye mambo ya pesa na biashara kwa ujumla.
 
Yaani pole sana kwa yaliyokukuta. Na hongera kwa kuweza kuyashinda.
Nimekupe saaana kwa jitihada zako...Mungu azidi kukubariki.
Kwenye Kikao usiende kabisa na namba ya cm ya huyo ex mume iblock ...kama ni mawasiliano awasiliane na watoto wake tu. Kwako anatafuta nini kgeni? Ni mkatili na pia ni muuwaji.
Usiende kwenye kikao tafadhali
 
HALELUYA MOSHI haujakosea kuna watu wanaweza kuyeyusha mawe kwa maneno tu.

Then tulia mama fanya yako! !!
Tena hiyo jmosi, mpe bby wako mahaba yooooooote ili umtoe wasiwasi wa kumkimbia for the so called ndoa ya kikristu!

Unaposhikwa shikamana mama!

Tulishaambiwa USITUPE MBACHAO KWA MSALA UPITAO (sijui ndo hivo ) Ila watu hawaelew
 
Last edited by a moderator:
Natamani sana ningeweza kuishi kihalali na huyu mpenzi wangu wa sasa. Ndio maana nadai talaka. Ningejua angekuja kukataa ningedai mapema hilo wazo halikunijia wakati ule.

Wide Open EYES

Nakushauri Usiende,usihangaike na kudai talaka,endelea kuishi na anayekuliwaza,fanya maendeleo yako.Huyo ex wako sio wa kuaminiwa wala hayuko responsible. Funga vioo,wakija kwako wakimbize kama walivyokukimbiza,naye Huyo mtoto wao adate kama wewe ulivyochanganyikiwa.Ukileta huruma na kuhudhuria vikao vya familia kama wanaokushauri,utavuna mabua,hata uliyenaye,atakosa imani na wewe, utarudia kudata tena.Hata kumwongelea kama mume,hana sifa alishapoteza alipokata Mawasiliano na kukutelekeza.
 
Last edited by a moderator:
Natamani sana ningeweza kuishi kihalali na huyu mpenzi wangu wa sasa. Ndio maana nadai talaka. Ningejua angekuja kukataa ningedai mapema hilo wazo halikunijia wakati ule.
Nenda mahakamani ukadai taraka ana ni pm nikupe maelekezo yote jinsi ya kufanya ili upate taraka yako.
 
Ukristo sio DINI, Ni uhusiano wa Mtu na Kristo. (Christianity is not a religion, Its a RELATIONSHIP)

Waambie waache ujinga, Ukristo haubariki UASHERATI. Once uasherati unapoingia, ndoa inaweza kufikia ukomo kihalali kabisa na kimaandiko.

Kama hawakubali, Wakale malimao.!!! maana hakuna namna nyingine sasa


Pinda kaacha legacy sana...., na yeye 'akakatwa tu'...
 
Hakufai dadangu hata aje akitambaa hakufai ,nenda na mpenz wako baaadhi ya wanaume nawachukia Mungu anisamehe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom