Nipo njiapanda

Nipo njiapanda

KUNI

Member
Joined
Sep 9, 2014
Posts
86
Reaction score
104
Habari zenu wanajukwaa,

Nina mpenzi ambaye nipo so commited kwake na matarajio yetu ni kuoana mwakani. Juzi kati hapa (mwaka jana) ilitokea nikazoeana na msichana mmoja mrembo mwenye asili ya kiarabu na kujikuta tumependana na kuwa wapenzi ingawa nilimwambia ukweli kuwa nina mpenzi tayari ambaye ndiye natarajia aje kuwa mke wangu.

Hilo alilielewa kirahisi hasa ukizingatia kuwa yeye ni muislamu damudamu nami ni mkiristo hivyo hata nisingekuwa na mpenzi mwigine kusingelikuwa na uwezekano wa mimi na yeye kuoana.

Mahusiano yetu na mrembo huyu wa kiarabu yaliendelea kwa kufanya michezo ya kimahaba bila ya kupeana tunda, kikwazo kikiwa ni huyo mrembo kwamba hawezi kufanya mapenzi kwani anapaswa kuja kuolewa akiwa bikira ingawa alikuwa akisisitiza ananipenda sana.

Nakumbuka siku moja aliniudhi sana kwa kushindwa kufika kwenye miadi kwa sababu zisizokuwa za msingi sana nikamtishia kumwacha nikimpa sababu kuwa kwa jinsi hali ilivyo inaonesha hanipendi.

Akanisihi sana nisimwache na akaomba kesho yake niandae mazingira mazuri alafu atakuja kunihakikishia kuwa ananipenda. Nami sikufanya ajizi nikambikiri hiyo kesho yake.

Ila baada ya kumbikiri ulizuka mgogoro mkubwa akidai anajutia kwani akija kuolewa atadharaulika kwa kukutwa hana bikira na akasema hataki kufanya mapenzi tena hivyo tuachane.

Ila baada ya wiki mbili hivi nikafanikiwa kumtuliza na kufanya naye mapenzi kwa mara ya pili.Safari hii alienjoy tendo na alikuwa na amani baada ya tendo.

Sasa juma chache baadaye (Alhamisi iliyopita) wakati tunachat akanidokezea kuwa ana mchumba aliyetafutiwa na mama yake. Na alimfahamu hata kabla yangu.

Kwa kuwa sikupendezwa na lugha aliyotumia kuwasilisha taarifa yake nikamwambia tuachane ili awe na Amani na huyo mchumba wake ambaye alidai anampenda pia.

Baada ya kunisihi kidogo tusiachane,akakubali tuachane. Tatizo ni kuwa siku moja tu baadaye hasira zilishuka na kujikuta namfeel zaidi huyu binti wa kiarabu na kujikuta sipo tayari kuachana naye kwa sasa.

Nikampigia kumsihi tureview uamuzi tuliochukua akakataa katakata akidai bora tumeachana kwani nimekuwa nikimuumiza mara kwa mara kwa hasira zangu na kumlimbikizia makosa.

Saizi hataki mawasiliano ya aina yoyote na mimi name bado nampenda tena sana. Sasa wadau kuna dalili kweli za kumrudisha huyu mrembo kwenye himaya yangu? Na kama uwezekano upo, nitumie mbinu gani kumrudisha.

Naomba mawazo yenu juu ya hili.Natanguliza shukrani.
 
ukimrudia utamuoa?
na yule mwingine yuko wapi na mahusiano yenu yakoje? ukijibu haya nitajua nikupe ushauri gani`
 
Wee potezea !! tafuta wengine.. wanawake wazuri bado wapo !! Na uache kuharibu mabinty za watu!!
 
Ni kweli wanawake wazuri wapo, lakini kwa jinsi navyomfeel huyu motto kwa sasa imefanya mwili uwe na ganzi kwa warembo wengine.
 
Kamhadithie mchumba wako wa kwanza kwamba mchepuko anakusumbua sana!
 
kaka oa yule uliemkusudia acha kumharibu na kumhadaa dada wa watu bana unatia hasira kweli wewe
 
Ni kweli wanawake wazuri wapo, lakini kwa jinsi navyomfeel huyu motto kwa sasa imefanya mwili uwe na ganzi kwa warembo wengine.

mchepuko sio dili kaka kama dada wa watu huna time usimuoe endeleee kufeeel weeee ukichoka utaoa
 
Nilitamani ungekua karibu nikupe vibao viwili vya shavu, japo najua sina uwezo huo
 
Back
Top Bottom