Nipo njiapanda, msaada wenu wanaJF

Kijana, sajili gari lako kwenye kampuni za Uber, bolt, taxify na little ride. Kwa kuwa huna ajira rasmi ni vema uendeshe mwenyewe, ukipata ajira inaliopa vizuri uza Hilo gari na uendelee na ujenzi.

Vv
asante sana mkuu kwa mawazo mazuri, ubarikiwe
 
Fungua genge kwa laki tano.Au tafuta dogo upate sehemu nzuri achome kuku utapiga pesa
 
Ukitaka kujua kwamba ushauli unaotolewa humu bado mwisho wasiku muhusika utatakiwa upambanue sana ugum wake ukoje sijaona mtualietoa ushauri unaoambatana naushuhuda hizo uber sijaona alieeleza namna inafanyika kuhusu vibari vyakufanyia biashara namengine mengi mm nafikiri usijilaum kununua gari maana hiyohela ungeweka tu sijui kama ingekuwepo
 
asante sana mkuu, ubarikiwe sana, nimejaribu kupitia nyuzi za ushuhuda kuhusu uber..kwenye nyuzi zinginezo naona kuna gharama nyingi za kujisajili uko.
 
Uza gari, kiwanja na iyo ela nyingine ongezea tuzamie south Africa maana mwezi ujao tarehe 6 tunasepa mwanangu

Dizonga si hatari sana kule? Risasi Nje nje ,New Variant wa UVIKO19?? S.A vijana wengi wanajiingiza kwenye hustle za snow.(Bimbwi).
 
Ukweli nikwamba kama hujawahi kufanya biashara ni ngumu sana halafu pia mzunguko wabiashara kwasasa sio mzuri sana labda biashara ndogondogo ambazo sio lasimi sana hofu yangu hilo gari nalo linahitaji mgawo kwenye hiyo milioni lazima utalitumia naukilitumia kwasasa litahitaji huduma kwanza linaweza kukufanya ushindwe kufanya kazi frani ambazo wengi wanaona zahovyo nakuomba jitahidi kujishusha jione wakawaida usiangalie hatua ulizokuwa umefikia anza upya hauko kwenye hatua mbaya sana
 
shukrani sana kaka, mungu akubariki sana
 
Kuuza gari na kuanza biashara mpya ni kazi sana..ni bora upige taxi kwa muda huku ukiendelea kusoma upepo..au mnadhani hii sio biashara?

Anaweza kuuza gari na kufungua biashara na isifanye fresh..mtaji ukapotea
 
Ucjari mkuu usiruhusu hofu ndani yako maisha nimagum kwawatu wengi sio peke yako .lichukulie umhimu tu mawazo mengi yametolewa hapa wengi wanania nzuri nawewe ila wazo kuu lazima litoke kwako ninaimani utatoka hatua hii mungu wetu ni mwema ukifanikisha hili usiache kusaidia wengine hata kuwatia moyo tunaokuombea utoke hatua hiyo niwengi pambana mkuu
 
Kuuza gari na kuanza biashara mpya ni kazi sana..ni bora upige taxi kwa muda huku ukiendelea kusoma upepo..au mnadhani hii sio biashara?

Anaweza kuuza gari na kufungua biashara na isifanye fresh..mtaji ukapotea
shukrani sana mkuu.
 
mungu akubariki sana mkuu, kwa nasaa yako kwangu.
 
Ingiza hiyo IST kwenye UBA....unatapata hela ya kula for a while...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…